Nawezaje kuondokana na haya majeraha yanayo niumiza moyo wangu

Nawezaje kuondokana na haya majeraha yanayo niumiza moyo wangu

Soma zaburi 51, alafu omba Toba na Rehema kwa ajili yako na ya mpenzi wako...

Kuna Roho ya mauti kwa ukoo wenu, hivyo omba Toba na Rehema pia kwa ajili ya familia upande wa baba na mama...

Utasahau yote

Utaolewa, Mungu ni mwema...
Mambo ya imani yanachekesha sana, kuna ukoo gani hauna roho ya mauti wote tuhamie huko?
 
Habari wakuu

Nimehangaika sana kukabiliana na hili jambo lakini kwa uwezo wangu wote imeshindikana kabisa nahitaji msaada na ushauri haswa wa kiimani

Lakini msaada huu sipendelei munielekeze kwa manabii wala mitume wala dini nyingine tofauti na ukristo
Kama una mchungaji unamfahamu ambae ana uwezo wa kuongea na Mungu direct na shidq yangu ikatatuliwa naomba mni comments hapA

Tatizo linalonisumbua ni hili

Mimi ni binti wa umri wa miaka 26.. mwaka fulani nilipata mchumba wa kutaka kunioa.. wakati yuko kwenye hatua za kuja nyumbani sijui niseme bahati mbaya ama ni nzuri yule kaka Alifariki,, ilikuwa kama ghafla tu

Katika maisha yangu nishaumia na mengi ila hili jambo ni jambo linalo niumiza sana yaani mno… nimejitahidi kulikubali na nikajifanya nina nguvu ya kulikabiri, mbele za watu najifanya ni strong sitaki kulialia ila ndugu zanguni ni uongo ninalia sana na nina umia ndani kwa ndani kila nimkumbukapo huyo kijana

Tangu tatizo linipate sijawai kupata mtu wa kunifanyia counseling wala maombi.. sijawahi kuonana na mtu yoyote wa kidini ambae labda angeomba na mimi

Hata nikitaka kuomba mwenyewe siwezi nakosa kuomba nakosa maneno ya kuongea

Ubaya zaidi tangu huyo kijana afariki mimi kwangu mahusiano ni changamoto kila ninaempata ninafanya comparison sana kiasi kwamba najikuta naachwa achwaa

Kwa sasa nina mahusiano mapya yana miezi 5 angalau kuna ka mwanga lakini nahisi huyu Kijana atanichoka maana nampa pressure sana.. asiponitafuta nakuwa naogopa,, siogopi kuachwa naogopa nisije pewa taarifa za msiba

Hili jambo linanitesa sana hofu ya kuachwa imenitawala… hata kuolewa naogopa maana kila nikikumbuka kuhusu ex wangu marehemu inaniuma sana
Unajua Hakuna kitu kinaniuma kama kifo chake.. yaani mwanaume niliekuwa nampenda tunapenda yupo tayari kunioa.. baada ya mawasiliano ya masaa mawili napewa taarifa ya kifo chake
Mwanaume ambae tulipanga mipango mingi ya baadae…nilishaamini kuwa angeenda kuwa mme wangu,, baba wa watoto wangu,, niliacha kila kitu changu kwaajili ya kujiandaa kuwa mke wake

Unajua namna inavyouma 😭😭
Ni kama vile nilipokonywa tonge mkononi

Nahitaji kupata ushaurii wowote haswa wa kiimani
NB:
Naomba ushauri wa kwenda kwa manabii ama mitume ama watu wafananao na hao sihiitaji… siitaji kulishwa keki wala mafuta wala chumvi wala kitambaa.. sihitaji waganga wa kienyeji

Mimi ni mkristo kabisaa
Nahitaji kupata mtu wa kweli wa Mungu anaeongea na Mungu direct najua Tanzania nzima hatokosekana
Nimesoma kisa kwa hisia. Mungu anakujali. Dai ahadi zake. Naamini msaada upo. Endelea na safari utaupata. Uoga ni natural, na usijali utashinda. Muda huponya mengi...

Kama utapenda naweza kukupa namba ya mama mmoja na mme wake (mchungaji) wanafanya counseling kwa wajane na waliofiwa (ingawa wewe sio mjane), na utapata suluhisho.

Nicheki PM
 
Pole Sana,

Ungekuwa muislam ningekuelekeza dua ya kuomba,

All in all, hakuna refu lisilo na mwisho, na hakuna usiku usio kuchwa,

Just hang in there, it will pass.

All the best
 
Uliacha kila kitu ukijiandaa kua mke. Sijui uliacha nini ila tafuta shughuli ya kukuweka busy hadi usipate nafasi ya kumuwaza. Kila mawazo ya huyo jamaa yanapokujia yareplace kwa mawazo mengine tofauti na yeye. Au waswahili walianza sema bwana harusi karogwa kafa??. Kua na imani sote tutakufa. Acha kumwazia mpenzi mpya kifo usije ukapata unachokiwaza.
 
Back
Top Bottom