Nawezaje kuondokana na haya majeraha yanayo niumiza moyo wangu

Nawezaje kuondokana na haya majeraha yanayo niumiza moyo wangu

Nenda hospitali. Una shida ya kisaikolojia.

Wewe ni Mkristu kabisa, hauhitaji wachungaji watoa mafuta, wala vitambaa wala keki! Vizuri! Muombee huyo mchumba wako, mkumbuke kwa ibada na omba pia usahau!

Nenda kwa mchungaji Kimaro la kama weweni Mkatoliki nenda kwa Paroko wako.
Kimaro ni nani na yuko wapi kama anapatikana mitandaoni naomba account yake hapa nimfuatilie before sijaenda
 
"Kama una mchungaji unamfahamu ambae ana uwezo wa kuongea na Mungu direct na shidq yangu ikatatuliwa naomba mni comments hapA"

Nilipoanza kusoma hii palagraph nikawa na maswali kibao kichwani anyway. Pole sana bi dada kwenye maisha kuna mapito mengi sana na kila mmoja ana safari yake ya kipekee kwenye huu ulimwengu usijione mnyonge sana na mwenye huzuni kwa sababu hata mungu hayupo pamoja na wale wanaokata tamaa (La tahzan )

Nafikiri, unaweza ukaongea na mungu wako unae muamini direct bila hata kumtumia shangazi yako au baba na mungu hua ni msikivu na akajibu haja zako.

Kuna wale wanao funga, maombi, kuamka usiku, kukesha all in all ondoa mentality ya kwamba kuna mchungaji anaweza kuongea na mungu on your behalf.


Full stop.
 
Polee sanaa, hii hali ilinikuta mie kipindi fulani.
Nilikua na mtu, yule wa kushibana nae, kwa kifupi alifanya nione dunia nyepesi kwa upande fulani, kunisaidia kwa hali na mali, sijui nielezeje. Hatukua na mahusiano ya kimapenzi, ila mie nilikua na hisia nae, ile kumfungukia ndo nilishindwa.

Alikufa kwa ajari ya piki piki, kile kifo chake kilinitia kiwewe, yaan nlikua napitia wakati mgumu hatari, shida wa kumueleza situation ile na akaelewa, sikumuona.

Baadae niliamua kuwa wazi juu yangu, ku ukubali ukweli na kuacha maisha yaendelee.
Nilipona kwa kiasi chake had now.
Nashauri kubali ukweli, na epuka kumuwazia sana huyo ex, japo sio rahisi, ila amini hivyo na maisha yaendelee.
Asante kwa ushuhuda nitajitahidi na Mimi maisha yasonge
 
"Kama una mchungaji unamfahamu ambae ana uwezo wa kuongea na Mungu direct na shidq yangu ikatatuliwa naomba mni comments hapA"

Nilipoanza kusoma hii palagraph nikawa na maswali kibao kichwani anyway. Pole sana bi dada kwenye maisha kuna mapito mengi sana na kila mmoja ana safari yake ya kipekee kwenye huu ulimwengu usijione mnyonge sana na mwenye huzuni kwa sababu hata mungu hayupo pamoja na wale wanaokata tamaa (La tahzan )

Nafikiri, unaweza ukaongea na mungu wako unae muamini direct bila hata kumtumia shangazi yako au baba na mungu hua ni msikivu na akajibu haja zako.

Kuna wale wanao funga, maombi, kuamka usiku, kukesha all in all ondoa mentality ya kwamba kuna mchungaji anaweza kuongea na mungu on your behalf.


Full stop.
Asante mkuu
 
Tatizo ulilonalo wewe ndo unasababisha lionekane tatizo na kumbe siyo shida kubwa sana ya kufanya ushindwe kuishi, wewe unatakiwa ujichanganye na watu tu kawaida hayo mawazo ya kufiwa yaweke pembeni kila mtu anapita hapa duniani au unafikiri ungekufa angekuwa bado anaomboleza? Ungeshashaulika ndani ya miezi 6 keshaoa mdogo wangu.
Pili mahusiano unayokutana nayo unayaua mwenyewe kwa kulazimisha kubeba mawazo ambayo sio lazima uwe nayo, na hata kama uko nayo sio lazima mtu ajue unawaza nini.
Watu huwa wanafiwa na waume zao wanaachwa na mimba na wanapona maumivu wanaendelea, omba mwenyewe upate amani na usahau yote uanze upya na Mungu atakufungulia mapya.
Usipende kulazimisha kila unayekutana naye aibebe hali yako ya kumkumbuka dear ex tena inakera mno kwa wanaume maana ataona humpendi kama muda wote unamfanyia comparison na marehemu.
Hakuna mwanaume atakuwa tayari kuwa na wewe kisa una huzuni za kumuomboleza ex, hayupo na hatotokea. Yaani unavyomuwaza yeye chukulia na wewe utapita kama yeye kifo hakiepukiki, kuomboleza sana hakubadilishi kilichotokea wala hakisabanishi wewe kupendwa sana zaidi ya kuwakera na kuwafukuza wenye nia ya kukuoa
Nimekuelewa mkuu
 
Asipokuelewa tena hapa atazidi kuwaza hadi atamani kumfuata mtu ambaye hata hakuzaliwa nae, hajazaa nae wala hakumjua kwa undani.... Inawezekana kama huyo jamaa angekuwepo ungekuta siku hii ya leo huyu binti angeleta uzi wa kulalamika ndoa ngumu 😁😁
😒
 
Back
Top Bottom