Nawezaje kuondokana na haya majeraha yanayo niumiza moyo wangu

kadogo2

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
3,278
Reaction score
5,212
Habari wakuu

Nimehangaika sana kukabiliana na hili jambo lakini kwa uwezo wangu wote imeshindikana kabisa nahitaji msaada na ushauri haswa wa kiimani

Lakini msaada huu sipendelei munielekeze kwa manabii wala mitume wala dini nyingine tofauti na ukristo
Kama una mchungaji unamfahamu ambae ana uwezo wa kuongea na Mungu direct na shidq yangu ikatatuliwa naomba mni comments hapA

Tatizo linalonisumbua ni hili

Mimi ni binti wa umri wa miaka 26.. mwaka fulani nilipata mchumba wa kutaka kunioa.. wakati yuko kwenye hatua za kuja nyumbani sijui niseme bahati mbaya ama ni nzuri yule kaka Alifariki,, ilikuwa kama ghafla tu

Katika maisha yangu nishaumia na mengi ila hili jambo ni jambo linalo niumiza sana yaani mno… nimejitahidi kulikubali na nikajifanya nina nguvu ya kulikabiri, mbele za watu najifanya ni strong sitaki kulialia ila ndugu zanguni ni uongo ninalia sana na nina umia ndani kwa ndani kila nimkumbukapo huyo kijana

Tangu tatizo linipate sijawai kupata mtu wa kunifanyia counseling wala maombi.. sijawahi kuonana na mtu yoyote wa kidini ambae labda angeomba na mimi

Hata nikitaka kuomba mwenyewe siwezi nakosa kuomba nakosa maneno ya kuongea

Ubaya zaidi tangu huyo kijana afariki mimi kwangu mahusiano ni changamoto kila ninaempata ninafanya comparison sana kiasi kwamba najikuta naachwa achwaa

Kwa sasa nina mahusiano mapya yana miezi 5 angalau kuna ka mwanga lakini nahisi huyu Kijana atanichoka maana nampa pressure sana.. asiponitafuta nakuwa naogopa,, siogopi kuachwa naogopa nisije pewa taarifa za msiba

Hili jambo linanitesa sana hofu ya kuachwa imenitawala… hata kuolewa naogopa maana kila nikikumbuka kuhusu ex wangu marehemu inaniuma sana
Unajua Hakuna kitu kinaniuma kama kifo chake.. yaani mwanaume niliekuwa nampenda tunapenda yupo tayari kunioa.. baada ya mawasiliano ya masaa mawili napewa taarifa ya kifo chake
Mwanaume ambae tulipanga mipango mingi ya baadae…nilishaamini kuwa angeenda kuwa mme wangu,, baba wa watoto wangu,, niliacha kila kitu changu kwaajili ya kujiandaa kuwa mke wake

Unajua namna inavyouma 😭😭
Ni kama vile nilipokonywa tonge mkononi

Nahitaji kupata ushaurii wowote haswa wa kiimani
NB:
Naomba ushauri wa kwenda kwa manabii ama mitume ama watu wafananao na hao sihiitaji… siitaji kulishwa keki wala mafuta wala chumvi wala kitambaa.. sihitaji waganga wa kienyeji

Mimi ni mkristo kabisaa
Nahitaji kupata mtu wa kweli wa Mungu anaeongea na Mungu direct najua Tanzania nzima hatokosekana
 
Hakuna mtu anayeweza kuongea na Mungu direct kwa niaba yako. Huyo hayupo.

Mungu ashindwe kukusikiliza wewe amsikilize mtu mwingine? Hapo unaenda kupigwa.
Shikilia imani yako hiyo hiyo huko unapoabudu tafuta mtu mzima wa kukushauri. Sali kivyakovyako.

Tatizo lako lingine unawaza sana kuolewa nadhani unahisi muda umekutupa mkono. Haipo hivyo.
Tambua ya kwamba ex alifariki bahati mbaya na amemaliza kazi yake hapa duniani unapaswa kumsahau na kumove on.
Usiharakishe kuingia kwenye mahusiano mapya jipe muda, jikeep busy na mambo mengine mchumba atakuja kwa wakati wake.
 
Kwanza kabisa ni kukubaliana na yakiyotokea. That you cant change the past, samehe au jisamehe.
Anza kuhudhuria ibada kanisani or msikitini. Anza kurudi kwneye jamii, hudhuria misiba na harusi or sherehe nyingine

Mshirikishe mtu wa karibu yako kuhusu linalokuumiza
 
Polee sanaa, hii hali ilinikuta mie kipindi fulani.
Nilikua na mtu, yule wa kushibana nae, kwa kifupi alifanya nione dunia nyepesi kwa upande fulani, kunisaidia kwa hali na mali, sijui nielezeje. Hatukua na mahusiano ya kimapenzi, ila mie nilikua na hisia nae, ile kumfungukia ndo nilishindwa.

Alikufa kwa ajari ya piki piki, kile kifo chake kilinitia kiwewe, yaan nlikua napitia wakati mgumu hatari, shida wa kumueleza situation ile na akaelewa, sikumuona.

Baadae niliamua kuwa wazi juu yangu, ku ukubali ukweli na kuacha maisha yaendelee.
Nilipona kwa kiasi chake had now.
Nashauri kubali ukweli, na epuka kumuwazia sana huyo ex, japo sio rahisi, ila amini hivyo na maisha yaendelee.
 
Habari wakuu

Nimehangaika sana kukabiliana na hili jambo lakini kwa uwezo wangu wote imeshindikana kabisa nahitaji msaada na ushauri haswa wa kiimani

Lakini msaada huu sipendelei munielekeze kwa manabii wala mitume wala dini nyingine tofauti na ukristo
Kama una mchungaji unamfahamu ambae ana uwezo wa kuongea na Mungu direct na shidq yangu ikatatuliwa naomba mni comments hapA

Tatizo linalonisumbua ni hili

Mimi ni binti wa umri wa miaka 26.. mwaka fulani nilipata mchumba wa kutaka kunioa.. wakati yuko kwenye hatua za kuja nyumbani sijui niseme bahati mbaya ama ni nzuri yule kaka Alifariki,, ilikuwa kama ghafla tu

Katika maisha yangu nishaumia na mengi ila hili jambo ni jambo linalo niumiza sana yaani mno… nimejitahidi kulikubali na nikajifanya nina nguvu ya kulikabiri, mbele za watu najifanya ni strong sitaki kulialia ila ndugu zanguni ni uongo ninalia sana na nina umia ndani kwa ndani kila nimkumbukapo huyo kijana

Tangu tatizo linipate sijawai kupata mtu wa kunifanyia counseling wala maombi.. sijawahi kuonana na mtu yoyote wa kidini ambae labda angeomba na mimi

Hata nikitaka kuomba mwenyewe siwezi nakosa kuomba nakosa maneno ya kuongea

Ubaya zaidi tangu huyo kijana afariki mimi kwangu mahusiano ni changamoto kila ninaempata ninafanya comparison sana kiasi kwamba najikuta naachwa achwaa

Kwa sasa nina mahusiano mapya yana miezi 5 angalau kuna ka mwanga lakini nahisi huyu Kijana atanichoka maana nampa pressure sana.. asiponitafuta nakuwa naogopa,, siogopi kuachwa naogopa nisije pewa taarifa za msiba

Hili jambo linanitesa sana hofu ya kuachwa imenitawala… hata kuolewa naogopa maana kila nikikumbuka kuhusu ex wangu marehemu inaniuma sana
Unajua Hakuna kitu kinaniuma kama kifo chake.. yaani mwanaume niliekuwa nampenda tunapenda yupo tayari kunioa.. baada ya mawasiliano ya masaa mawili napewa taarifa ya kifo chake
Mwanaume ambae tulipanga mipango mingi ya baadae…nilishaamini kuwa angeenda kuwa mme wangu,, baba wa watoto wangu,, niliacha kila kitu changu kwaajili ya kujiandaa kuwa mke wake

Unajua namna inavyouma 😭😭
Ni kama vile nilipokonywa tonge mkononi

Nahitaji kupata ushaurii wowote haswa wa kiimani
NB:
Naomba ushauri wa kwenda kwa manabii ama mitume ama watu wafananao na hao sihiitaji… siitaji kulishwa keki wala mafuta wala chumvi wala kitambaa.. sihitaji waganga wa kienyeji

Mimi ni mkristo kabisaa
Nahitaji kupata mtu wa kweli wa Mungu anaeongea na Mungu direct najua Tanzania nzima hatokosekana
Kwa kukusaidia Mungu hana dalali. Wewe ndie wa kumface na atakupa aman ya moyoni. Huo ndio ukubwa kadiri unavyokuwa wale wanaokuzunguka watakufa na hata yale usiyotarajia yatakukuta. Kikubwa usiwekee kitu chochote au mtu yeyote tumain. Ni Mungu tu ndie tumain la kweli. Kila mtu anaweza kukususa na kukusema vibaya Mungu pekee hata kukimbia . So muombe sana na usiweke sana akili zako kwa mtu hata huyo uliyenae. Usiamin kwamba nitaolewa na huyu natajenga life letu cjui nini. Hata akikukataa fresh tu we amin Mungu amekupangia mema mbele yako kazana pambana binafs mume mke atakukutana kwenye mapambana na hapo ndipo utakutana na alichokupangia Mungu na sio ulichopanga wewe. Acha kumpangia mungu cha kukupa au acha kuomba unachofikiri Mungu ni mwema anajua muda sahihi wa kukupa. Omba uwepo wa Bwana maishani mwako na ulinz wake. Omba asimame kukuongozq. Na uamke kupambana. Maisha ni mapambano sio kulialia. Simama uhesqbiwe
 
Hakuna mtu anayeweza kuongea na Mungu direct kwa niaba yako. Huyo hayupo.

Mungu ashindwe kukusikiliza wewe amsikilize mtu mwingine? Hapo unaenda kupigwa.
Shikilia imani yako hiyo hiyo huko unapoabudu tafuta mtu mzima wa kukushauri. Sali kivyakovyako.

Tatizo lako lingine unawaza sana kuolewa nadhani unahisi muda umekutupa mkono. Haipo hivyo.
Tambua ya kwamba ex alifariki bahati mbaya na amemaliza kazi yake hapa duniani unapaswa kumsahau na kumove on.
Usiharakishe kuingia kwenye mahusiano mapya jipe muda, jikeep busy na mambo mengine mchumba atakuja kwa wakati wake.
Dear sijui kama utakuwa umenielewa vibaya

Kuna wakati unatamani kuomba ila unashindikana unakosa ujasiri wa kuomba nguvu zinakuishia.. sijui kama umeshawahi kuondokewa na mpendwa wako

Kuna vitu ni vigumu kuvufanya peke yako lazima huitaji mtu wa pili na mimi ndio huyo ni nae mtafuta

Nina amini Mungu bado ameacha masalia yake kuna watumishi wanaoweza kuzungumza na Mungu moja kwa moja bila kuingiza uchafu wowote wa maigizo ya mafuta wala chumvi wala maji najua wapo

Nina amini kuna wachungaji ambao unaweza kufanya nao maombi na maombi yako yakajibika kwa urahisi

Dear mpk kufikia kuja hapa kuomba ushaurii nimeshajaribu kuomba mwenyewe vimeshindikana na siwezi kumchukua yoyote tu kwasababu namuona kanisani ni kaomba nae hapana

Suala la ndoa sina haraka nalo maana kama ningekuwa nataka ningekubali na hapa nilipo mtu akizungumza habari za kunioa ninaogopa situation ya niliyopitia inanirudia nawaza what if na huyu likamkuta hilo jambo

Na ndio maana natafuta uponyaji yamkini kuna sehemu nimeachia uwazi shetani akapata nafasi. What if hawa nao wakataa kunioa kumbe ni kazi ya ibilisi kuharibu
 
Kwa kukusaidia Mungu hana dalali. Wewe ndie wa kumface na atakupa aman ya moyoni. Huo ndio ukubwa kadiri unavyokuwa wale wanaokuzunguka watakufa na hata yale usiyotarajia yatakukuta. Kikubwa usiwekee kitu chochote au mtu yeyote tumain. Ni Mungu tu ndie tumain la kweli. Kila mtu anaweza kukususa na kukusema vibaya Mungu pekee hata kukimbia . So muombe sana na usiweke sana akili zako kwa mtu hata huyo uliyenae. Usiamin kwamba nitaolewa na huyu natajenga life letu cjui nini. Hata akikukataa fresh tu we amin Mungu amekupangia mema mbele yako kazana pambana binafs mume mke atakukutana kwenye mapambana na hapo ndipo utakutana na alichokupangia Mungu na sio ulichopanga wewe. Acha kumpangia mungu cha kukupa au acha kuomba unachofikiri Mungu ni mwema anajua muda sahihi wa kukupa. Omba uwepo wa Bwana maishani mwako na ulinz wake. Omba asimame kukuongozq. Na uamke kupambana. Maisha ni mapambano sio kulialia. Simama uhesqbiwe
Hiyo kuomba ndio aMbaya nahitaka lakini siwezi
 
tafuta msaada wa mtumishi wa Mungu uombe naye, hiyo ni roho ya uchungu inakusumbua.

Kuhusu mchumba, unatakiwa ujue huyo hayupo kabisa hata ukiendelea kulinganisha unajichosha bure na kujipotezea muda,
 
Back
Top Bottom