Polee sanaa, hii hali ilinikuta mie kipindi fulani.
Nilikua na mtu, yule wa kushibana nae, kwa kifupi alifanya nione dunia nyepesi kwa upande fulani, kunisaidia kwa hali na mali, sijui nielezeje. Hatukua na mahusiano ya kimapenzi, ila mie nilikua na hisia nae, ile kumfungukia ndo nilishindwa.
Alikufa kwa ajari ya piki piki, kile kifo chake kilinitia kiwewe, yaan nlikua napitia wakati mgumu hatari, shida wa kumueleza situation ile na akaelewa, sikumuona.
Baadae niliamua kuwa wazi juu yangu, ku ukubali ukweli na kuacha maisha yaendelee.
Nilipona kwa kiasi chake had now.
Nashauri kubali ukweli, na epuka kumuwazia sana huyo ex, japo sio rahisi, ila amini hivyo na maisha yaendelee.