Tatizo ulilonalo wewe ndo unasababisha lionekane tatizo na kumbe siyo shida kubwa sana ya kufanya ushindwe kuishi, wewe unatakiwa ujichanganye na watu tu kawaida hayo mawazo ya kufiwa yaweke pembeni kila mtu anapita hapa duniani au unafikiri ungekufa angekuwa bado anaomboleza? Ungeshashaulika ndani ya miezi 6 keshaoa mdogo wangu.
Pili mahusiano unayokutana nayo unayaua mwenyewe kwa kulazimisha kubeba mawazo ambayo sio lazima uwe nayo, na hata kama uko nayo sio lazima mtu ajue unawaza nini.
Watu huwa wanafiwa na waume zao wanaachwa na mimba na wanapona maumivu wanaendelea, omba mwenyewe upate amani na usahau yote uanze upya na Mungu atakufungulia mapya.
Usipende kulazimisha kila unayekutana naye aibebe hali yako ya kumkumbuka dear ex tena inakera mno kwa wanaume maana ataona humpendi kama muda wote unamfanyia comparison na marehemu.
Hakuna mwanaume atakuwa tayari kuwa na wewe kisa una huzuni za kumuomboleza ex, hayupo na hatotokea. Yaani unavyomuwaza yeye chukulia na wewe utapita kama yeye kifo hakiepukiki, kuomboleza sana hakubadilishi kilichotokea wala hakisabanishi wewe kupendwa sana zaidi ya kuwakera na kuwafukuza wenye nia ya kukuoa