Nawezaje kutengeneza Internet?

Nawezaje kutengeneza Internet?

Ingia kwenye ntandao tafuta ujisomee kuhusu (LAN) Local Area Network na WAN.

Ni vitu vinawezekana. Ni upeo wako tu.

Sky is not "the limit" anymore.
Asante sana wewe kweli ulienda shule at least jibu lako linamwanga nini chakufanya

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Anataka LAN yake iunge kwenye WWW Ila asifanye malipo yoyote kwa service provider.
Hapo asimlipe hata ISP? Hapo itabidi atengeneze infrastructure zake mwenyewe.

Kuna majambo mawili anaweza kufanya..

1. Atengeneze WLAN na local DNS server then azipe majina ip addresses za devices zake ili iwe rahisi kuconnect kwa kutumia domain name instead of IP address. Locally only

2. Atengeneze Server yake kuhost website, ila bado atahitaji kufanya complex setup mfano Port Forwarding, nk, na pia atahitaji kununua public domain name ili aweze kupublish kwenye internet. Hapo atakuwa ameepuka gharama za kuhost tu.
Ila sio njia nzuri na gharama huwa kubwa kuliko akihost publicly
 
Napenda kuanza kwa kusema kuwa kutengeneza na kuuza huduma ya internet binafsi inaweza kuhitaji maarifa ya kiufundi na idhini kutoka mamlaka husika. Hapa kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua:

Unda miundombinu ya mtandao: Unahitaji kuwa na miundombinu ya mtandao inayoweza kutoa huduma ya internet kwa wateja wako. Hii inaweza kujumuisha kusimika vifaa kama minara ya mawasiliano au kutumia miundombinu iliyopo.

Pata leseni na idhini: Katika nchi nyingi, unahitaji leseni na idhini kutoka mamlaka ya mawasiliano au mamlaka inayohusika na teknolojia ya habari. Hakikisha unafuata sheria za nchi yako.

Chagua mfumo wa biashara: Fikiria jinsi utakavyotoza wateja wako, ikiwa ni pamoja na bei na mifumo ya malipo.

Weka usalama na utendaji: Hakikisha mtandao wako ni salama na unatoa huduma bora kwa wateja. Hii ni pamoja na kusimamia usalama wa data na kuhakikisha upatikanaji wa huduma kwa wateja.

Fanya masoko: Fikiria jinsi utakavyotangaza huduma yako kwa wateja watarajiwa. Unaweza kufanya masoko kupitia matangazo ya mtandaoni, mikutano ya kijamii, au njia nyingine za kufikia wateja.

Tathmini gharama na mapato: Hakikisha unaelewa gharama zote za uendeshaji wa biashara yako, pamoja na uwekezaji wa awali, na jinsi utakavyolipa bili zako na kupata faida.

Toa huduma bora kwa wateja: Kutoa huduma bora na kujenga uhusiano wa kudumu na wateja wako ni muhimu kwa mafanikio ya biashara yako.

Kumbuka kuwa kuanzisha biashara ya huduma ya internet binafsi inaweza kuwa ngumu na inahitaji uwekezaji mkubwa wa wakati na rasilimali. Pia, sheria na kanuni zinaweza kutofautiana kutoka nchi hadi nchi, kwa hivyo ni muhimu kushauriana na wataalamu na mamlaka za ndani kabla ya kuanza biashara
 
Mtoa mada anataka mautundu ya bwana Elon yule mmliki wa star link....

Kila ktu kinawezekana mkuu ni mtaji na mautundu tu....

Kwanza uwezo wa kurusha rada anga...mbali na kuitengeneza.

NB: ukiweza kukamilisha hayo yote utaweza kuwa Internet yko
 
Hautaki local internet unataka free internet wewe. Hakuwezi kukawa na free internet ya halali kwa vile internet inapatikana kwa kupitia infrastructure ambayo ni ya kulipia e.g mitambo ya kampuni ya simu au fiber connection za nchini na zile zinazotuunganisha na dunia nzima kupitia zile fiber za baharini au satelite. Hata nchi ambazo kuna maeneo kama library, vituo vya usafiri, shule zinatoa "free" internet ni kwamba inalipiwa na mtu mwingine, kodi etc.

Internet haiwezi kuwa local kwa definition internet ni kila kitu ukishafanya local hiyo sio internet.

Kutokana na makosa ya hapa na pale kwa upande wa providers unaweza kujikuta umepata internet ya "free" kwa trick za hapa na pale kama kuna providers walikuwa hawapimi baadhi ya ports so unaweza ukakuta bundle haiendi huku unapata mtandao ila hizo njia no za muda tu mpaka tundu linapozibwa.

Local network unaweza kutengeneza simply kwa kuwasha wifi router, device zote zinazoconnect hiyo wifi zipo kwenye local network na zinaweza kubadilishana data hata kama hakuna internet.
 
Back
Top Bottom