Hali hii imeakuanza lini? Ni mara yako ya kwanza au huwa inakutokea mara kwa mara? Je, kuna tukio lo lote baya (mf. kufiwa na mzazi au mpendwa wako) ambalo limetokea au lilitokea kipindi hiki? Afya yako ikoje? Umeongezeka (sana) uzito au kukonda ghafla? Kazini kuna misukosuko? Maisha yako kimapenzi yamekaaje? Kuna mabadiliko yo yote hasi kiuchumi? Ulikuwa mfuasi wa CHADEMA katika uchaguzi uliopita? Kiroho umesimama imara?
Majibu ya maswali hayo juu (na mengineyo) yaweza kutoa fununu lakini pia yawezekana ni msongo wa mawazo (depression) umekuanza. Kama ni hivyo utahitaji msaada wa kitaalamu kutoka kwa daktari wako au watoa nasaha. Au yawezekana ni mvurugano tu wa homoni na makemikali mwilini na hali hiyo yaweza kujirekebisha yenyewe tu.
Kwa sasa jaribu kuwa karibu na watu wakupendao. Kama kuna mmoja unayemwamini mwambie unavyojisikia. Unahitaji faraja na watu wanaojali. Kama ni muumini yawezekana pia ikawa ni vita vya kiroho. Mbali na wewe mwenyewe kupambana katika maombi, jaribu kumshirikisha kiongozi wako wa kiroho. Kama upo katika kikundi cha maombi au jumuia waombe wawashe moto wa maombi kwa ajili yako. Epuka kuwaza mawazo hasi na jitahidi sana kufanya mambo uyapendayo na hasa hasa kusaidia wenye shida. Badala tu ya kujifungia ndani, kama unaweza, nenda hata hospitalini huko ukasalimie wagonjwa siku za wikiendi au wakati wo wote unapokuwa na muda. Saidia watoto katika vituo vya mayatima huko na matendo mengine madogo madogo ya wema. Naamini baada ya muda msukosuko huu utapita, moyo wako utatanzuka na furaha yako itarejea.
Na kumbuka tu kwamba
"you are fearfully and wonderfully made. Mungu Akubariki. [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
View attachment 1624935