Nawiwa kuongeza mke wa pili

Mzee wa old school

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
873
Reaction score
1,405
Habarini Wana jamvi.. mimi ni mkristo na muhudhuriaji mzuri sana kanisani na hata jumuia... Lakini Kuna baadhi ya Mafundisho Nina mashaka nayo sana hasa haya ya ndoa.... Eti mkristo kuoa mke mmoja,,,, mbona kwenye Biblia hakuna maelekezo hayo? Ninacho kumbukusha ni kwamba mtume Paulo alishauri ASKOFU AWE MUME WA MKE MMOJA... hakutaja umma kwa ujumla wake...


Ni hayo tu... Naamini watu wenye fikra tunduizi watatoa maoni... Sitarajii kejeli na udini nataka mjadala wenye hoja za msingi ili kupata muafaka/ suluhisho la mgongano wa uelewa juu swala hili
 
Sababu yako ya kuongeza mke wa pili ni Ipi? Tuanzie hapo kwanza.
 
Kisheria Hautaruhusiwa..
Kwa sababu wewe ni mkristo sheria ya ndoa ya mwaka 1977 haikuruhusu Kufanya Polygamy Inasema...Kama ukiendelea Kushika Imani ya Kiksrito basi Daima utakuwa Monogamy...

Ila Kidini Hakuna Zuio lolote
 
Aya unaijua vizuri sana, kwamba askofu asikengeuke awe na mke mmoja. Hata wewe uñatakiwa uwe na mke mmoja ili ukikengeuka ukaoa mke wa pili askofu awe na uwezo wa kukukemea na kukurudisha kwenye mstari. Sasa akiwa na mke zsidi ya mmoja atakukemeaje?
 
Wewe oa hata 700 kama Suleimani.
 
Biblia ya wapi unasoma,biblia imetoa mwongozo wa mke mmoja mbona
 
1 Wakorintho 7:2-4

[2]Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.

[3]Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.

[4]Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.
 
Kuna sheria, kanuni na best practices. Best practices ni vitu ambavyo haviko kisheria, wala kikanuni lakini vimeonekana kuwa na mwenendo au matokeo bora zaidi.

Hapa kanisa haliku base kwenye bible bali walitumia best practices. Maisha ni bora ukiwa na mke mmoja ambao mnaishi kwa amni na upendo.

Lakini mwisho wa siku chaguo ni lako.
 
Hizi ndio zile akili Mnemba😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…