Nay wa Mitego adai anatafutwa kuuawa

Nay wa Mitego adai anatafutwa kuuawa

Lumumba mnatumia nguvu Sana kutetea kauli ya Ney, vipi Kuna kitu mnajua tayari?

Nimemkumbuka Sana BeN.
 
Gvt ikishabikia udaku...haiwezi kufocus kwenye key macrroeconomic issues badala yake inaconcentrate kwenye micro comic stuff....uchumi unaenda upande kama umenyeshwa viroba
Mkuu natamani kama kila mtu angeelewa ulichokiandika hapa,big up sana.
 
Msanii mkubwa wapi nyie? Wacheni sifa za kijinga,, nani sue sisimizi? Eti walinzi ni sisi yaani tuache kazi zetu tumlinde wa mitego? Ina maana alivyoitwa ikulu alienda kutishiwa maisha?
 
Wanajamii amani kwenu!
Tumewahi kusema mara kadhaa bila mafanikiao, Ikulu ya Tanzania sio miongoni mwa ofisi za uenezi za CCM . Ikulu ya Tanzania ni mahali patakatifu (the holly land" Ikulu ya Tanzania sio kijiwe cha akina Paul Makonda na Polepole, Ikulu ndio mboni ya jicho letu kama Watanzania.
Mr Nay ameitwa Ikulu (a presidential invitee) hilo ni jambo moja ameitwa na nani/kwanini hili ni jambo jingine.
Tutafakari haya;
Tujiulize haya, Kama Ikulu pia ni ofisi za CCM Je Mr Nay kaitwa na Rais au na Mwenyekiti wa CCM taifa?
Kama ameitwa na Mwenyekiti wa CCM taifa Je nikipi kimemvutia mwenyekiti huyu kwenye wimbo huu wa "WAPO"
Je niule ubeti wa mwisho unaosema," Wewe mtu gani hutaki kushauriwa, hutaki kukosolewa umelogwa wewe............... Oya wanangu eeee! round hii mtanyooka hakiamungu naona kichaa kapewa rungu"
Je ni kweli maudhui ya wimbo huu yanamgusa (Ki-fasihi) mwenyekiti huyu jasiri kabisa
Nawaza kwa sauti, Je
1. Mwenyekiti huyu wa CCM anashaurika jibu? "HAPANA" kumbe YUPO
2. Mwenyekiti huyu wa CCM anakosoleka ? "HAPANA" kumbe YUPO
3. Mwenyekiti huyu kila tukio TV ( anakiki ) ? "NIKWELI" kumbe YUPO
Hongera Nay kwa kumtoa Nyoka Pangoni , Nay wewe ni Andanenga/Shaban Robert wa II, Najua hukumaanisha mtu yeyote, Najua maana ya fasihi, uchungu wa fasihi,mafunzo ya fasihi.
Huyu mwenyekiti wa CCM anayekuita ofisi za magogoni ni njia tu ya kutaka kukufarakanisa na wana CHADEMA wenzako.
Ushauri wangu kwa Nay kama ni kwenda uende na mwenyekiti wako Mh Freeman Mbowe,Katibu mkuu wako Dk Vicent Biyegela Mashinji sio mbaya kama utawachukua pia wajumbe wa kamati kuuhata wawili kama Mzee Edward Lowassa na Fredrick Sumaye
Umeandika kwenye ukurasa wako wa Instagram wanataka kukupoza "Usiogope" Walimuua Mwangosi,wakamuua Kamanda Mawazo,Ally Zona (Morogoro),Masood Nassoro(Igunga) Mbwambo aliyekatwa kicha kama ng`ombe Arumeru,akina Dennis Shirima wa Arusha kwani wewe ni nani hata uogope kufa, Yuko wapi Ben wa Saanane aliyependa kucheka mara zote.
Kwa wale mnapenda kejeli,dharau na matusi huu uzi hauwahusu, we are serious to help our undergoing country Tanzania.
Tuinge mifano ya akina Paschal Mayalla, Technicallity, quinene, Lizabon,OKW BOBAN SUNZU,Yericho, GJ Malisa,Mwanahabari huru,Goliath,JSM Mtatiro,Faizafoxy,Jidu la Mabambasi,Gentamycine na wengineo wenye kukosoa kwa hoja sio matusi wala dharau.
Msemakweli Mpenzi wa Mungu
"Tanzania is the only country we have
 
Huyo pasco mtoe hapo anasumbuliwa na u-regionalism full ukanda ! Pathetic.
 
Kumbe sisi watumia mtandao tuna bonge la impact kwenye jamii daah safi sana mpaka mkuu anawaza malaika waje waizime mitandao ya kijamii" i wish could be imformation minister mimi nisingeweka yale marekebisho ya sera ya habari
 
Kuna mmoja umemtaja hapo kwenye list kwa mitusi huyo ni balaa sijui ulitumia kigezo gani kumuweka.
 
Najiuliza, huyu Ney akihitajika kuuwawa kweli hivi itachukua dakika ngapi hadi roho kumtoka? Tuache utoto, na sipendi kufikiria kwa kutumia akili ndogo ya mtu kama Ney.
Kuua mtu haijawahi kuwa shida ,shida ni ku cover tendo lenyewe mkuu ndio kwenye tabu !binadamu sio nzi umuue then uendelee na shughuli zako?japo nakuunga mkono kwa lipialilolifanya Nay mpaka atafutwe kuuawa!
 
Guys the government can't do such a foolish and gibberish thing to kill a guy who had a conflict with it. Unless otherwise, he would have stated ,clearly who what kill him.
Sometimes , we need to keep out our government from such crazy issues and use our intelligence to analyse any information we come across with .

Also, anyone should be aware that if the government needs you to be nailed down they won't tell you nor get into a crush with you so as to avoid any finger pointing towards it.

Probably, his competitors in music industry wishes to use that arrest and talks he had with police and our president respectively to put him down.

Though, those who are closer to him they should give him some secret security follow up to realize who is behind such information he shared because, seems to be a bit strange!

But, our government shouldn't be involved to such a shit of a piace of information / or a situation.
You have spoken as if you have ultimate security with your life and you don't fear anything! By the way that is our way! Don't let others go first
 
Aache uongo auawe kwa kuimba tu mwimbo Au kuna kingine.masifa mengine ya kijinga sana
We weka tu picha yako na jina kamili kwenye profile uone kitakachotokea. Kitu kidogo kinacost
 
Najiuliza, huyu Ney akihitajika kuuwawa kweli hivi itachukua dakika ngapi hadi roho kumtoka? Tuache utoto, na sipendi kufikiria kwa kutumia akili ndogo ya mtu kama Ney.
Kumbuka Ney kamgusa bashite na kamchana wazi wazi.
Nape alijaribu ..kidogo tu akagaragazwa kibabe..na kabla vumbi halijatulia akaibuka dogo (kwa namna ya kupiga yaliyomkuta waziri wao).

Baada ya kutoa 'kibao' chake, chenye mistari ya kuchoma mioyo ya bashite, pingu zikaibuka ghafla na police escort ya nguvu ikiwekewa na naksi za press statement ya polis kuwa tunaye (hupigwi pingu kama hujawaudhi wenye nchi), Basata nao wakamrushia rungu la hatari...

Nay akaokolewa na hasira ya umma. Vijana wasanii wakatupa mikuki mikali dhidi ya serikali mitandaoni. Umma ukaja juu hali ikawa tete ghafla.

Mara wimbo wa Ney ukageuka asali ghafla...ukapendwa hadi na mkulu, tena Waziri Mwakyembe akatumwa kwa waandishi wa habari akauza sura na tabasam...alishangaza umma. Wenye serikali wakajidai hawahusiki. Ilikuwa 'bahati mbaya tu.'

Ghafla mialiko ya Ikulu na Dodoma ikawa mingi. Unadhani walienda kumwambia nini huko kama sio "watch it?" Au "SHUT UP?"
Jiongeze ndugu yangu...jiongeze tena afu uniambie kama walienda kumpa Ney mkono wa pongezi kisha wakampa na platform ya kuusambaza zaidi wimbo wake.

Na je Ney akikataa rai aliyoitiwa na serikali huku na kule yatampata yepi na hali hawawezi ufungia 'wimbo pendwa' mara mbili mbili?

Tusifanyane mazuzu humu jukwani.
 
tz ya viwanda inakaribia ,lakini wako bize na wanaowakosoa sijui 2020 watatudanganya nn ?
Na hasa ukizingatia mgombea wetu sasa hivi kasimamisha "HURUMA" yake ya kumwaga mabilioni makanisani na misikitini akisubiri 2020.
 
We ulijuaje hayo? Na kwann uuawe? hamna usiogope kwani umekosa nini? Mbona uliitwa kwa mkuu wa jumba ukaendaa usioogope, "kunywa maji mwanagu" na si ulikunywa maana yake yameisha na Mkuu akakuongezea na mistari ya kuimba
 
Back
Top Bottom