Wanajamii amani kwenu!
Tumewahi kusema mara kadhaa bila mafanikiao, Ikulu ya Tanzania sio miongoni mwa ofisi za uenezi za CCM . Ikulu ya Tanzania ni mahali patakatifu (the holly land" Ikulu ya Tanzania sio kijiwe cha akina Paul Makonda na Polepole, Ikulu ndio mboni ya jicho letu kama Watanzania.
Mr Nay ameitwa Ikulu (a presidential invitee) hilo ni jambo moja ameitwa na nani/kwanini hili ni jambo jingine.
Tutafakari haya;
Tujiulize haya, Kama Ikulu pia ni ofisi za CCM Je Mr Nay kaitwa na Rais au na Mwenyekiti wa CCM taifa?
Kama ameitwa na Mwenyekiti wa CCM taifa Je nikipi kimemvutia mwenyekiti huyu kwenye wimbo huu wa "WAPO"
Je niule ubeti wa mwisho unaosema," Wewe mtu gani hutaki kushauriwa, hutaki kukosolewa umelogwa wewe............... Oya wanangu eeee! round hii mtanyooka hakiamungu naona kichaa kapewa rungu"
Je ni kweli maudhui ya wimbo huu yanamgusa (Ki-fasihi) mwenyekiti huyu jasiri kabisa
Nawaza kwa sauti, Je
1. Mwenyekiti huyu wa CCM anashaurika jibu? "HAPANA" kumbe YUPO
2. Mwenyekiti huyu wa CCM anakosoleka ? "HAPANA" kumbe YUPO
3. Mwenyekiti huyu kila tukio TV ( anakiki ) ? "NIKWELI" kumbe YUPO
Hongera Nay kwa kumtoa Nyoka Pangoni , Nay wewe ni Andanenga/Shaban Robert wa II, Najua hukumaanisha mtu yeyote, Najua maana ya fasihi, uchungu wa fasihi,mafunzo ya fasihi.
Huyu mwenyekiti wa CCM anayekuita ofisi za magogoni ni njia tu ya kutaka kukufarakanisa na wana CHADEMA wenzako.
Ushauri wangu kwa Nay kama ni kwenda uende na mwenyekiti wako Mh Freeman Mbowe,Katibu mkuu wako Dk Vicent Biyegela Mashinji sio mbaya kama utawachukua pia wajumbe wa kamati kuuhata wawili kama Mzee Edward Lowassa na Fredrick Sumaye
Umeandika kwenye ukurasa wako wa Instagram wanataka kukupoza "Usiogope" Walimuua Mwangosi,wakamuua Kamanda Mawazo,Ally Zona (Morogoro),Masood Nassoro(Igunga) Mbwambo aliyekatwa kicha kama ng`ombe Arumeru,akina Dennis Shirima wa Arusha kwani wewe ni nani hata uogope kufa, Yuko wapi Ben wa Saanane aliyependa kucheka mara zote.
Kwa wale mnapenda kejeli,dharau na matusi huu uzi hauwahusu, we are serious to help our undergoing country Tanzania.
Tuinge mifano ya akina Paschal Mayalla, Technicallity, quinene, Lizabon,OKW BOBAN SUNZU,Yericho, GJ Malisa,Mwanahabari huru,Goliath,JSM Mtatiro,Faizafoxy,Jidu la Mabambasi,Gentamycine na wengineo wenye kukosoa kwa hoja sio matusi wala dharau.
Msemakweli Mpenzi wa Mungu
"Tanzania is the only country we have