Nayaona Maisha ya Gamondi Yanga kuwa mafupi sana

Na kwani Kuna ubaya huyo huyo Gamondi msimu huu mbinu zake zikamezwa na matokeo kuwa tofauti na msimu ukiopita ( ambao umekariri ww )??
 
Na kwani Kuna ubaya huyo huyo Gamondi msimu huu mbinu zake zikamezwa na matokeo kuwa tofauti na msimu ukiopita ( ambao umekariri ww )??
Mbinu zake ni zipi hizo unazozijua wewe? Ingekuwa mbinu za kocha zinajulikana basi kipa asingekuwa kafanya zile save zaidi ya 5 bali kusingekuwa na on target. Ila kilichotokea leo sio kutokana na Gamondi kuzidiwa mbinu bali ni kipa kuwa shujaa wa Ken Gold
 
U
Unaongea kishabiki ndio maana hatuelewani....na kamwe hatuwezi kuelewana.....ila binafsi nasubiria kuona plan B yake siku kitumbua kikiingia udongo
 
Title ipi mkuu?? Umesoma vzr??.....Unaujua mpr vzr?? Unaelewa kwenye mpira sio kila Kocha ana uwezo wa kubadili philosophy ya kile anachoamini?
Gamondi amebadili philosophy yake kadri anavyoona mpinzani alivyo. Tukiangalia msimu uliopita Yanga ilikuwa inacheza mchezo wa kutumia nguvu nyingi uwanjani kwa wachezaji kufanya high pressing na kuuchukua mipira kila wanapopoteza mpira. Ila mechi ya Yanga na Mamelodi, Gamondi kawa sio Gamondi yule watu waliokuwa wamemzoea. Gamondi akabadilisha mbinu na falsafa kwenye mechi zote mbili dhidi ya Mamelod.

Angalia Yanga ya msimu huu, haichezi ule mpira wa kufanya high pressing mwanzo mwisho bali wanacheza kwa vipindi, kuna muda watakuachia ucheze kuna muda wanaamua kufanya pressing na Yanga wamefunga kila aina ya goli kuna magoli ya counter attacks na magoli ya build up.

Yanga imecheza michezo minne kwenye klabu bingwa na miwili ya ngao ya jamii vs Azam na Simba na zote Yanga kashinda
Kwenye ligi Yanga imeanzia away na zote kashinda, mechi ya Yanga dhidi ya Kagera na hii ya leo dhidi ya Ken Gold makipa ndio waliofanya kazi ya ziada kuifanya Yanga isipate magoli mengi ila sio kuzidiwa kwa Gamondi kimbinu au mfumo. Mpira hata huko ulaya timu haiwezi kushinda kila mechi kwa idadi ya magoli mengi bali kuna siku utatoa sare, utashinda kwa tabu au kufungwa au kushindwa magoli mengi. Sio timu ikiwa ina buruza mkia ndio guarantee ya timu kubwa kama Yanga kushinda magoli mengi. Wewe hujui mpira ni shabiki mkurupuko
 
Kote umeongelea pressing....kasoro mechi hizo mbili walizocheza na MAMELODI hujasema wamecheza mfumo upi mkuu....unahisi hawakucheza pressing pia??.....kingine Mimi sijasema popote Juu ya mechi ya Leo kuhusu Yanga kupata ushindi finyu, thread yangu imelenga kuainisha wapi Yanga ilipotoka, ilipo , na kesho yake ( nimetaadharisha TU Kama maoni binafsi ) ukiwa chini ya Kocha Gamondi sawa dogo??
 
Unasikilizaga michezo mkuu??

Alishaulizwa kwann nini baleke hachezi??...jibu haingii kwenye mfumo wake

Hapo hapo alishawahi kusema mara nyingi ana kikosi kipana....jiongeze hapo mkuu utanielewa
Baleke Yanga walimchukua kwenye ile Simba ya kuunga unga,Simba walimwona hana kiwango,usijali wa Yanga ulikuwa wa kukomoa Simba tu sasa inakula kwao
 
Chai
 
Sasa mbona umehitimisha kuwa hana muda mrefu kwenye timu?

Kwa sasa bongo hakuna timu iliyokamilika kama Yanga, lakini pia ushindani kwenye mpira ni kawaida, usitegemee wao kushinda big kila wakati.
Nimesema hivyo baada ya kuona kuanzia alipotoka, alipo Sasa, kesho sijui ndio maana nikaandika anaweza akabadilika siwezi kushangaa maana ndio mpira, na haitakuwa mbaya maana nitajufunza kitu, nipo kujifunza pia
 
Mimi sijasema popote Juu ya mechi ya Leo kuhusu Yanga kupata ushindi finyu, thread yangu imelenga kuainisha wapi Yanga ilipotoka, ilipo , na kesho yake ( nimetaadharisha TU Kama maoni binafsi ) ukiwa chini ya Kocha Gamondi sawa dogo??

Kwahiyo uliposema kuhusu kocha wa Ken Gold kufungua njia kwa makocha wengine, hii mechi ya Ken Gold na Yanga ambayo ulioizungumzia kwenye uzi wako ilikuwani ya mwaka juzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…