Nayapenda makabila yanayoenzi matambiko ya kimila kwani matambiko sio ushirikina

Nayapenda makabila yanayoenzi matambiko ya kimila kwani matambiko sio ushirikina

n
Maiti ni mboga hauna msaada wowote kwa maisha ya mtu aliye hai

Ni tafasiri yako hiyo sikupingi Mkuu.

Ila tambua kuwa kuna watu wanakuwa na msaada sana wakifa zaidi ya walivo kuwa hai.
Kuwadharau walio kufa ni kuwakosea adabu sana.
 
sijawadharau Mzee.
je mtu akifa akili yake inaendelea kufanya kazi?
Hapana haiendelei kufanya kazi , ila Roho ipo katika ulimwengu wa Roho na ndo inasaidia katika matambiko

Matambiko ni mhimu sana Mkuu
 
Bila shaka umeielewa mada hii ,ila matambiko yanakaribiana sana ushirikina tu . Mimi najua kabisa kuwa matambiko~ushirikina na hakuna wa kunipinga hilo atakaye pinga atakuwa kanikosea adabu sana. Kuacha kufanya, kufanyiwa, kushiriki matambiko ni kazi sana kama umeyakulia
Matambiko is equivalent to Ushirikina sema yanawekwa katika soft language.
 
Jua kutambikia sio ushirikina kivile, kutambikia unakuwa unazungumza na walio kutangilia wakusaidie. Ndo maana hata baba na mama ako wanawajbu wa kukutunza hivo hvo pia wakifa wanawajbu bado wa kukusaidia na kuhakikisha damu yao ipo salama. Kama wapo hao kizazi cha nyuma kinawajibu huo. Kutambikia unazungumza na wazee wa ukoo wakusaidie
Kama kutambika maana yake ndio hiyo haiwezi kuacha kuwa ni ushirikina maana haiwezekani waliokufa wamsaidie alie hai...isipokuwa tu kinachotakiwa kwa mfiwa unachotakiwa ni kuwaombea Rehema kwa Mungu waliotangulia na sio kuwaomba wao msaada au utegemezi ukishawaomba wafu msaada tayari huo ni ushirikina tena si mdogo
 
Just Awesome. You made my day. Najua wachaga wenzangu watapita na kusoma hapa kimya kimya .....
Wanafanya sana ila kwa siri sana, juzi kuna mzee alivulia mtoto nguo hadharani akavaa (iphilyikya) , akaenda tena mlangoni akauonyesha mlango wa nyumba ya mwanae tupu ya nyuma,

Hivo tukawa hatuna budi zaidi ya kumsara matulu (kuchanja makalioni katikati kupata damu ya huko na kuichanganya na ya kondoo/mbuzi iliyo kulia katika familia hiyo kwa Imani Kali) ili kuondoa nuksi katika familia
 
Nisaidie kuelewa kitu kimoja...... Mnaamini kabisa kuwa sasa nuksi katika hiyo familia zitakuwa zimeondoka kwa kuchanganya damu ya binadamu na ya kondoo/mbuzi? ....... Seriously??
 
Kama kutambika maana yake ndio hiyo haiwezi kuacha kuwa ni ushirikina maana haiwezekani waliokufa wamsaidie alie hai...isipokuwa tu kinachotakiwa kwa mfiwa unachotakiwa ni kuwaombea Rehema kwa Mungu waliotangulia na sio kuwaomba wao msaada au utegemezi ukishawaomba wafu msaada tayari huo ni ushirikina tena si mdogo

Kutambikia kuna raha yake bana, kama kumsara mtu kwa hiari yake, ili kuondoa ujinga wake ni raha sana

Wewe kama haufanyi ni wewe wengne wanaendekea kwa raha zao.

Ya kale ni dhahabu.
 
Anaesema matambiko ni ushirikina basi kwa wakristu ile altare wanayozunguka kwa mishumaa ni ushirikina tena wa kizungu . Zingatia tambiko lako la kiafrika
 
Nisaidie kuelewa kitu kimoja...... Mnaamini kabisa kuwa sasa nuksi katika hiyo familia zitakuwa zimeondoka kwa kuchanganya damu ya binadamu na ya kondoo/mbuzi? ....... Seriously??
Yes seriously tunaamini hivo, cha mhimu wakati unafanya tambiko usiwe na shaka uwe na IMANI

Unajua kwa nn watu wengi wanamuomba Mungu, Mungu hasikii maombi yao?. Ni kwa sababu ya kukosa Imani. Hata kwenye matambiko Imani Kali sana ni mhimu kushinda chochote kile

Ya kale ni dhahabu
 
Kutambikia kuna raha yake bana, kama kumsara mtu kwa hiari yake, ili kuondoa ujinga wake ni raha sana

Wewe kama haufanyi ni wewe wengne wanaendekea kwa raha zao.

Ya kale ni dhahabu.
Kweli kabisa hata ushirikina wanaofanya wanasema hivyohivyo kwamba wanafanya kwa raha zao lakini haimaanishi kuwa inampendeza Mungu
 
Kweli kabisa hata ushirikina wanaofanya wanasema hivyohivyo kwamba wanafanya kwa raha zao lakini haimaanishi kuwa inampendeza Mungu
Ni raha sana Mkuu

Sasa kama haujii kufanya matambiko, utakuwa mtu gani sasa?

Ukipata nafas jifunze hata tu jinsi ya kufanya tambiko moja la kumrejesha ndani mwanamke aliyepigwa na mumewe hadi kutolewa damu ,baada ya kumsamehe

Ili hyo mwanamke aweze kupikia watoto, na mume aweze kula chakula cha mkewe

Ukipata nafas jifunze utaweza Mkuu japo ni ngumu ila jikaze

Ya kale ni dhahabu :
 
Na ule udi unaofukizwa kanisani (wakatoliki) ni nini?
Au kwaya na mapambio, si matambiko nayo?
Hapo sijawaelewaga sana kivile :

Ila jua tu kwamba matambiko ni mhimu sana :

Tumshukuru mdau Kwa kutukumbusha :
 
n

Ni tafasiri yako hiyo sikupingi Mkuu.

Ila tambua kuwa kuna watu wanakuwa na msaada sana wakifa zaidi ya walivo kuwa hai.
Kuwadharau walio kufa ni kuwakosea adabu sana.
Sasa huo uwezo wa kusaidia wanaupata vp na kutoka kwa nani baada ya wao kufa?
 
Back
Top Bottom