Tatizo Mwafrika hana Imani na cho chote kilicho chake ukisha ona mtu anajaribu mpaka kubadilisha mwonekano wake kwa kudhani sio mzuri (haupendezi), kutukuza utamaduni wa mtu mwingine basi ujue tatizo ni kubwa sana. Lakini kwa kifupi dini zote zimetokea kwenye matambiko alichokifanya Myahudi Abraham anasemekana kuwa ndio baba wa Imani kwenye kitabu cha historia kiitwacho Biblia, angekifanya Msukuma au Mnyakyusa leo Waafrika tungesema uchawi. Mambo kama al badri kwenye Imani za Kiislamu zina tofauti gani na ushirikina..?!! Wajapani na wengine wa Mashariki wana Imani zao tofauti kabisa na Ukristo au Uislamu na wanaendelea vizuri na wanakula neema hapa hapa duniani. Kipimo gani tunatumia kusema hizi Imani za ku import na nyingine tulifundishwa kwa nguvu eti ndio Imani za kweli?? Tatizo liko kwetu na usikute msoto huu unaonatupata Waafrika ukawa unatokana na kuacha Imani zetu na kuwatelekeza mababu zetu. Leo hatuna mbele wala nyuma shida, mateso na kudharaulika imekuwa ndio kitambulisho na Mwafrika na mtu mweusi popote pale alipo kwenye sayari hii. Hebu tusiwe wa haraka kupayuka kabla ya kufakari kwa kina bila uwogo tujiulize tatizo nini..!!