Naytrueboy, mwanamuziki aliyewahi kuwa maarufu na tajiri amefilisika baada ya kujiunga CHADEMA

Naytrueboy, mwanamuziki aliyewahi kuwa maarufu na tajiri amefilisika baada ya kujiunga CHADEMA

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Watanzania tuna cha kujifunza, huwa tunasikia watu wanasema "Niko tayari kufa", "Niko tayari kufanya lolote".

Mabadiliko ni process ambayo hutakiwi kuibeba peke yako, ni zao la jamii kwa ujumla na kwa pamoja, usije ukaumiza familia yako na kazi zako ukiamini wewe pekee utaweza.

Kama jamii bado inaamini katika hali ilivyo (status quo), tembea na biti za jamii. Wema usizidi uwezo. Ukidhurika ni wewe na familia yako, hutamuona yule kiongozi mkuu wa chama au taasisi, ni wewe na wanao.

Usiharibu carrier yako, let nature take it's course.

Pole Ney, punguza mizinga kwenye baa, rudia fani yako. CHADEMA hakualiki hata katika matamasha yao, hata ukiitisha shoo Arusha, au Kilimanjaro au mbeya, ngome za CHADEMA, ukumbini utakuwa peke yako.

Jifunze kwa Sugu, na Prof. Jay, wamezilinda fani zao, na wamezitenga na Siasa, kwani Sugu au Prof. Jay unadhani hawawezi kuimba nyimbo kwa mlengo wako? Akili kichwani.

Omba kolabo na mwanamuziki mkubwa uone kama atakubali, hata Sugu na Prof. hawatakubali.

You are done and dusted!
Screenshot_20230729-143934.jpg
 
Jua kutofautisha kukimbiwa na kufilisika, vitu viwili tofauti kabisa

Hivi hapa bongo ukiachana na Diamond kuna msanii tajiri ?

Nay ana hali za kawaida tu ila si haba ana nyumba, kausafiri, biashara zake nje ya muziki, n.k., uzuri huwa hafeki maisha anaishi maisha yake.

Kilichokufanya ulete hii post ni wazi kabisa ni miguno ya maumivu dawa inapoingia,
 
Anasimamia anachokiamini..ww je!? Umaskini nini,kwani ukiwa tajiri haufi?
 
tatizo kubwa kaitukana serikali kwa kejeli vijana tiini mamlaka namna hii hamtaweza kuishi na wazee
 
Mambo ya kupambana na Mamlaka haya.

Unabaki peke yako,mwisho anaanza kuona watu wabaya.
 
Yes sure. Prof Jay alipoumwa alitibiwa bure kwa msaada wa serikali ya CCM. Chadema wenzake walitoweka, wakamtelekeza wakamuacha 'afe peke ake'. Wengine walisha anza kummezea mate mke wake mrembo.
 
Hizi habari za uongo. Halafu hawa CCM ni waongowaongo miaka yote.
 
Jua kutofautisha kukimbiwa na kufilisika, vitu viwili tofauti kabisa

Hivi hapa bongo ukiachana na Diamond kuna msanii tajiri ?

Nay ana hali za kawaida tu ila si haba ana nyumba, kausafiri, biashara zake nje ya muziki, n.k., uzuri huwa hafeki maisha anaishi maisha yake.

Kilichokufanya ulete hii post ni wazi kabisa ni miguno ya maumivu dawa inapoingia,
Mkuuu
Unaweza kututajia hizo biashara
 
Nay Juzi si amevuta Range Rover Vogue? Au kufirisika una maanisha nini?
 
Kuna yule anayejifanya naye mwanaharakati alafu anaimba nyimbo yupo nje ya nchi (Roooomaaa) fimbo ya mbali haiui nyoka,,,,,
Big up the True Boy
 
Back
Top Bottom