Nazeeka, naogopa!

Nazeeka, naogopa!

Uzee mbaya mweeh!

Lakini usikubali. Usibweteke na kujiona sasa hufai...eti umebadili na mavazi kisa uzee! Tutapambana nao tuuu siukubali kirahisi...cha kwanza utoe kwenye akili yako, vaa, fanya unavyojisikia na unavyopenda. Uzee usiufungulie mlango...pigana nao hadi uone sasa hata mguu hauinuki.
 
Uzee ni tunu....uzee ni baraka.....uzee ni kisima cha maarifa......uzeee ni zawadi kwani ni wachache sana wanaopata zawadi hiyo.......
Hutakiwi kuuogopa uzee....bali unatakiwa ujivunie uzee......


Ufanye uzee wako kuwa kisima na chem chem ya hekima kwa vijana.....wafanye vijana wajivunie kuwa na wewe karibu.....kwa kuwasambazia busara na hekima......

Epuka kuwa mtu mzima hovyo....kwa kufanya mambo yaliyo kinyume na umri wako.....

Sawa sawia ni kweli tena kweli. si unaona jinsi vijana sasa hivi wanavyopata (bold) kutoka kwa mzee wetu Prof. Haruna Ibrahim Lipumba. Hebu furahia uzee wako na sie vijana tukufaidi.
 
98046f33dc024ac61b9fc1921e316c9d.jpg
 
uzee mbaya kama hauna hela ila ujiwa na hela ni burudani tu. Hata watoto wakali utabeba bila shida.
 
Huenda tatizo lako ni kupenda kukaa na watu uliowazidi sana kiumri. Tafuta watu wa rika lako ufurahie maisha. Shikamoo ni makelele tu.
 
Ndugu zangu,

Nafikiri nipo katika wakati mgumu sana,nazeeka na nimeingiwa na hofu, nimegundua nauingia utu uzima, nimechukia, naogopa nahisi maisha ndio basi, kila nikipita nasalimiwa shikamoo, sipendi jamani wengine wananisalimia nawaona kama tunalingana,naogopa sana uzee.

Mvi zinabisha hodi kila kukicha, nimeanza kubadili mavazi niliyoyapenda sasa navaa kama mchungaji, sitaki lakini hakuna jinsi, mlioushinda uzee nitieni nguvu nahisi sipendwi tena nikipita hakuna anayenitazama kama zamani, naogopa kutongoza huenda nikatukanwa hadharani.

Mmh, mlioushinda uzee nisaidieni
Mkuu unapitia situation kama Yangu, Kuna watu wakiniamkia nanuna kabisa, naona kuwa sistahili shikamoo zao. Kweli ujana maji ya moto, Shikamoo uzee.
 
Sasa weye ndugu, usipozeeka maana hutaki wanao wakue? Wanao wakidumaa utafurahi?

Kama hupendi wanao wadumae basi kubali kuzeeka.

Vv
 
Lakini sista kuna stage unafikia kila unayekutana nae anakupa "shikamoo dada/kaka/uncle/aunt". Lazima ushtuke kuwa mshale umeshavuka saa sita. Ni kweli uzee ni vile unavyokiweka lakini......at 50+ I guess there's fear kiaina.
Eli, mi niko kwenye forties lakini naamkiwa na wazee mpaka naogopaga.
 
mtu mzima anAogopa kuzeeka? hata babu alikua kijana.....
 
Back
Top Bottom