Ha ha haa
Raimundo, kweli wewe matata ila unasahau kitu kimoja kuhusu hesabu na hasa zile za shule ya msingi. Mbona hesabu hazidanganyi jamani, here we go...je, unakubali kuwa;
- kama chungwa moja ni shilindi ishirini, machungwa manne ni shilingi themanini?
- kama unatembea maili moja kwa dakika thelathini, kwa saa mbili utatembea maili nne?
- kama mtu moja unamaliza sahani ya ugali, watu wanne mtamaliza masahani mangapi?
- kama hatua moja ina urefu wa futi tatu, hatua nne zina urefu gani?
- Kama kwa dakika moja unafunga vikapu viwili, kwa dakika nne utafunga vikapu vingapi?
Nitarudi baadaye...!