DOKEZO NBS toeni tamko: Ulipaji wa pesa za semina za Sensa kuna uhuni unafanyika

DOKEZO NBS toeni tamko: Ulipaji wa pesa za semina za Sensa kuna uhuni unafanyika

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kama sio upotoshaji basi watu wa aina ya ni wapuuzi wakubwa, posho ni kwa ajili ya kazi na kuna taratibu zake….. mtu halipwi kwa huruma eti hakuwa na ajira.

Alikuwa anaishije, acheni upuuzi…. bora turejeshe walimu tu.

Ni ajira ipi unalipwa kabla ya kazi?
Wee utakua mwalimu uliyekatwa kwenye maombi,mmeshazoea umaskini waoga kudai haki zenu
 
Nikiwa kwenye daladala Nimesikia wadada wanaoelekea IAA Uhasibu Arusha wakilalamika kupunguzwa na kuongezwa Hovyo hovyo Kwa makarani ambao hawakuwepo toka mwanzo.
Unayesimamia Hicho kituo Cha mafunzo zingatia weledi.
 
Sensa imekosa coordination,na serikali inapaswa kuingilia kati haraka kabla mafunzo hayajaharibika.
Uhuni wa Sensa upo hivi.

Ni zoezi pekee lisilokuwa na mwongozo wa malipo kwa wahusika,kama mwongozo upo basi Waratibu wa sensa Mikoa na wilaya wameificha.

Mazoezi yote ya kitaifa huwa yanaanza na kutaja maslahi ya washiriki kwa kika kundi,ili kuondoa sinto fahamu huwa wanansomewa siku ya kwanza.

Huwa inafanywa hivyo kwa mazoezi nyeti ya kitaifa.

Lakini kwenye hii Sensa kila mtu hana majibu.

Makarani kwenye mikoa yote baadhi wamesomewa na maeneo mengine hawajui watalipwa nini.

Mbaya zaidi Walimu wao ,yaani wakufunzi wa mafunzo hawajui watalupwa pesa Kiasi gani.

Yaani kika wilaya na Kila mkoa una malalipo yake.

Yaani ukiwauliza Mbeya ambayo ni jiji wanatofautiana na Dar es salaam ambao ni jiji na ni tofauti na Dodoma na Mwanza.

Ukiuliza Mtwara manispaa,ukalinganisha na Shinynaga,Kigoma na Tabora kila manispaa wana malipo yake.

Hakuna mwongozo wa kitaifa kwa zoezi hili kujua kila kundi lilipwe nini kwa utaratibu gani ambao utarahisisha ukaguzi wa hizo fedha za Umma.

Yaani malipo ya Makarani,Wakufunzi na ITs yanategemea huruma ya Mratibu wa Mafunzo wa Mkoa.

Kukosa mwongozo kunaweza kuwa kwa bahati mbaya au Mkakati wa wizi uliondaliwa kuanzia Ngazi ya taifa.

Mwigulu Nchemba anafanya kazi nzuri sana ya kutafuta pesa,lakini asipoingiliankati fedha itatumika na lengo halitafikiwa.


Sensa inaelekea kuharibika,Watu wa usalama wapo,Takukuru wapo ,saidieni serikali kudhibiti ujinga unaofanywa na baadhi ya Maafisa wa Serikali.

Mlisema Rais Magufuli alikuwa anafanya kika kitu yeye mwenyewe,alilenga kukomesha huu ujinga wa mazoezi ya kitaifa kukosa mwongozo uliowazi.

Raisa Samia kawapa uburu ili mumsaidie kwa kutumia elimu zenu,mnachofanya mnafanya watu wamuone kashindwa kuwasimamia.mnamuharibia.

Wizara ya fedha au Ofisi ya waziri Mkuu itie mwingozo haraka,watu walulwe kwa wakati kwakuea Bajeti ipo na fedha zimeshatolewa.

Kendelea kukaa kimywa wakati kuna manung'uniko kwenye madarasa yote ya Mafunzo,mtaharibu zoezi.
Bado mnaweza kuweka vizuri Mambo na watu wakarudi kwenye marali ya kufundisha na kujifunza.

Mliopo karibu na Mwigulu na Waziri Mkuu mfikishieni huu ujumbe.
You have nailed it.Tatizo la mama yangu, she is too humble, anadanganyika kirahis...sio sceptical kabisa. Anamwamini mtu haraka sana.
 
Billion 350+ ni pesa ndogo kuelekezwa kwenye malipo tu achilia mbali vifaa na logistics zingine? Kwa Nchi maskini kuelekeza mapesa yote hayo kwa kazi ya mwezi unaita hela ndogo? Hahahaha you cant be serious!!
Ushapima umuhimu wa hiyo kazi ya mwezi mmoja?
Sensa ndio dira ya Maendeleo kwa miaka kumi ijayo.
 
Ushapima umuhimu wa hiyo kazi ya mwezi mmoja?
Sensa ndio dira ya Maendeleo kwa miaka kumi ijayo.
Dira ya maendeleo kama katiba mpya itakuepo.Tumeshuhudia watu au MTU kujiamlia kufanya au kutofanya kitu Fulani Kwa manufaa binafsi.
 
Ilikuwa wapewe elf 10 ya chakula kwa siku badala yake wanawalisha ubwabwa wa buku.
Mbongo ashavuta percent yake.elf 7000 anaweka mfukoni. Wapeni watu pesa zao watajua wenyewe jinsi ya kula
 
Hapo data zitapikwa,na picha itaishia hapo,eti mama anataka watu wanaosukumwa kufanya kazi toka mioyoni mwao,hawajui viongozi wa Tanzania nini?
Anajizima data huyu,ndio maana mwamba akutaka kabsa kucheka na kima.
 
Poleni nyote mnaolalamika na kunung'unika, ila chanzo kikuu ni kutokuwekwa wazi kwa mikataba na usimamizi mbovu uliopo,
Kunatime naweza kuilaumu serikali iliopo madarakani ila nafsi nyingine inaniambia hakuna malaika mbele ya pesa huo ndo mwiba mkubwa kwa wanadamu wote,
kila mtu anawaza kujikusanyia bila kujuwa familia ya jirani yake inateseka kwa njaa
Tanzania punguzeni tamaa
 
Nchi yetu mambo mengi tunayafanya kienyeji,jambo la kuwa serious tunalichukulia poa kama watu wa Bongo movie tu
 
Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu, tangu semiza zianze ni siku ya kumi na moja Leo kuna baaadhi ya halmashauri hazijalipa hata senti moja. Swali, hao wanasemina wanaishije, usafiri, nk?

Angalizo, kuna uhuni unaendelea watu wanawatoa watu waliokaa siku nane semina wanaleta watu wao, zile siku nane wanajiandikia wao.

Wito, kama mtu kafukuzwa alipwe pesa yake, na kwanini watu wakae semina siku zaidi ya tano bila malipo? Huo si uhuni na mazingira ya upigaji?

Mama Makinda watch out! Kuna uhuni unaendelea, kama hamjatoa pesa semeni.
Viongozi wengi wa Tanzania wana njaa kali.
 
Kuna roho inaniambia ni sawa. Na kuna nyingine inaniambia siyo sawa.

Anyway, sipingani na kucheleweshewa pesa ila napinga katakata watu kufukuzwa wakati wamehudhuria semina zaidi ya wiki.
Wanafukuzwa kwa nini
 
dah wilayani kwangu kama nawaona vile watakavyodata wasipolipwa maana saa kumi na mbili na nusu watu wanaburuza miguu kwenda shule x kufanya semina yao ikifika jioni saa kumi na mbili wanaburuza tena miguu kirudi kwenye mapango yao na ukipishana nao wanakuona kama kapuku flani usie na kazi wao ndio wanakula mema ya nchi
 
Back
Top Bottom