DOKEZO NBS toeni tamko: Ulipaji wa pesa za semina za Sensa kuna uhuni unafanyika

DOKEZO NBS toeni tamko: Ulipaji wa pesa za semina za Sensa kuna uhuni unafanyika

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wakuu pesa ipo, kitu ambacho serikali imefail ni kushindwa kulipa kwa wakati ila kila mtu atalipwa, songea leo kila karani kapewa ela 10000+ ya nauli tu , na ile ya siku 5 ambayo lak 2, sasa watu 900 mara 10000 shngap ,ela ya ziada tu hyo naul ambayo hata wasingetupa tusingelalamika
 
Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa wamelipa tayari jana kwa baadhi ya kata sina uhakika kwingine ila hela mbovu 40 per day plus nauli 10k ujanja janja tu
 
Ndugu zangu,
Posho ni 30,0000 kwa siku. Kati ya hizo mzabuni wa chakula analipwa 10000 kwa chai na chakula cha mchana.
Ni 40,000 per day na chakula wanalishwa.
Wapi huko wanalipwa 30,000?
 
Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu, semiza zianze ni siku ya kumi na moja Leo kuna baaadhi ya halmashauri hazijalipa hata senti moja. Swali, hao wanasemina wanaishije, usafiri, nk?

Angalizo, kuna uhuni unaendelea watu wanawatoa watu wamekaa siku nane semina wanaleta watu wao zile siku nane wanajiandikia wao.

Wito, kama mtu kafukuzwa alipwe pesa yake, na kwanini watu wakae semina siku zaidi ya tano bila malipo? Huo si uhuni na mazingira ya upigaji?

Mama Makinda watch out! Kuna uhuni unaendelea kama hamjatoa pesa semeni.
CCM hii haina ridhaa ya wananchi hivyo lazima ienda kilaana laana tu na haita faulu chochote.Mpaka itakapojua kwamba sauti ya wengi ni sauti ya MUNGU.
 
Umeandika mawazo yako kwa hisia zako tu, kama na wewe ni mmoja wa waliofurushwa kutokana na kufeli mafunzo usilielie….. malipo siku zote ni baada ya semina.
Watu wanaongea serious issue wewe unaleta porojo hapa, tulia tena tulo hivi unaijua hii nchi wewe, wewe kenya kenua meno zoezi litaisha mtaishia kuomba msaaada ukiona watu wapo serious na vitu tulia
 
Unatakiwa taarifa yako iwe na maelezo kamili ya halmashauri gani imefanya hivyo na lini na nani msimamizi wa kituo na idadi ya walio fukuzwa ili iweze kufanyiwa kazi
Tarifa za kintalijensia hazipo hivyo kaa JF ujifunze vitu vingi utaokoka sema amen
 
Kwa akili ya kawaida tu unamuwekaje mtu mafunzo kuanzia asubuhi mpaka jioni kwa kumpa chai na chakula cha mchana siku kumi hata mia ujampa je kama uyu mtu ana familia na mwangaikaji si unaumiza familia yake je kama anatokea umbali wa kilometa ishirini mpaka eneo la semina hiyo nauli kuja na kurudi si uhuni huu kama walikuwa hawajipanga wangeaacha siyo kuweka watu ten days hata mia ujawapa uzalendo gani huo

Uhuni mwingine wanambiwa mtalipwa kupitia bank, haya bank gani eti yoyote Ile wewe leta account bank 😂😂😂 si wanapigwa hawa huo mchakato wa kuandaa playlist upeleke CRDB watu nane uende NBC watu kumi uende NMB watu ishirini 😂😂 dah yani unawaza unaona hapa Kuna usanii
Mkuu utatokaje kilometer 20?wkt kwenye tangazo la kuomba kazi lilisema uombe eneo husika unaloishi yaan uwe mkaz wa pale,ndo maana mwenyekiti wa Kijiji lazima athibitishe na upigiwe muhur na kitongoji au Kijiji,,hao wanaosema wanatoka mbali wapi
 
Back
Top Bottom