Sensa imekosa coordination,na serikali inapaswa kuingilia kati haraka kabla mafunzo hayajaharibika.
Uhuni wa Sensa upo hivi.
Ni zoezi pekee lisilokuwa na mwongozo wa malipo kwa wahusika,kama mwongozo upo basi Waratibu wa sensa Mikoa na wilaya wameificha.
Mazoezi yote ya kitaifa huwa yanaanza na kutaja maslahi ya washiriki kwa kika kundi,ili kuondoa sinto fahamu huwa wanansomewa siku ya kwanza.
Huwa inafanywa hivyo kwa mazoezi nyeti ya kitaifa.
Lakini kwenye hii Sensa kila mtu hana majibu.
Makarani kwenye mikoa yote baadhi wamesomewa na maeneo mengine hawajui watalipwa nini.
Mbaya zaidi Walimu wao ,yaani wakufunzi wa mafunzo hawajui watalupwa pesa Kiasi gani.
Yaani kika wilaya na Kila mkoa una malalipo yake.
Yaani ukiwauliza Mbeya ambayo ni jiji wanatofautiana na Dar es salaam ambao ni jiji na ni tofauti na Dodoma na Mwanza.
Ukiuliza Mtwara manispaa,ukalinganisha na Shinynaga,Kigoma na Tabora kila manispaa wana malipo yake.
Hakuna mwongozo wa kitaifa kwa zoezi hili kujua kila kundi lilipwe nini kwa utaratibu gani ambao utarahisisha ukaguzi wa hizo fedha za Umma.
Yaani malipo ya Makarani,Wakufunzi na ITs yanategemea huruma ya Mratibu wa Mafunzo wa Mkoa.
Kukosa mwongozo kunaweza kuwa kwa bahati mbaya au Mkakati wa wizi uliondaliwa kuanzia Ngazi ya taifa.
Mwigulu Nchemba anafanya kazi nzuri sana ya kutafuta pesa,lakini asipoingiliankati fedha itatumika na lengo halitafikiwa.
Sensa inaelekea kuharibika,Watu wa usalama wapo,Takukuru wapo ,saidieni serikali kudhibiti ujinga unaofanywa na baadhi ya Maafisa wa Serikali.
Mlisema Rais Magufuli alikuwa anafanya kika kitu yeye mwenyewe,alilenga kukomesha huu ujinga wa mazoezi ya kitaifa kukosa mwongozo uliowazi.
Raisa Samia kawapa uburu ili mumsaidie kwa kutumia elimu zenu,mnachofanya mnafanya watu wamuone kashindwa kuwasimamia.mnamuharibia.
Wizara ya fedha au Ofisi ya waziri Mkuu itie mwingozo haraka,watu walulwe kwa wakati kwakuea Bajeti ipo na fedha zimeshatolewa.
Kendelea kukaa kimywa wakati kuna manung'uniko kwenye madarasa yote ya Mafunzo,mtaharibu zoezi.
Bado mnaweza kuweka vizuri Mambo na watu wakarudi kwenye marali ya kufundisha na kujifunza.
Mliopo karibu na Mwigulu na Waziri Mkuu mfikishieni huu ujumbe.