Halaiser
JF-Expert Member
- Apr 3, 2014
- 4,230
- 6,653
Yeye mwenyewe baada ya hayo yote kakimbilia wapi hivi sasa?? Walikokimbilia nje ya nchi na vijijini bado wako hai wanadunda. Yeye yuko wapi??Wataweza wapi? Mshike mshike wa JPM wa miaka 3 tu wengi wao wakakimbia nchi, walioshindwa kukimbia nchi wakakimbilia vijijini kulima na kufuga
Soma Hadithi hii kisha jitafakari:
Baada ya mwenye nyumba kuona panya anamaliza nafaka zake, aliamua kununua mtego na akamtega.
Panya lile jambo lilimpa huzuni sana, akapiga mbiu kuwatahadharisha na wengine akina kuku, mbuzi na ng'ombe kuwa waungane kuutegua mtego huo.
Alianza kwa kusema "..Kuna mtego humu ndani, baba mwenye nyumba kaweka mtego jamani.."
Kuku akahoji: "Mtego wa nini?"
Panya: akajibu "ni wa panya"!!
Kuku akasema huo ni mtego wa panya mimi haunihusu.
Ng'ombe na Mbuzi nao walijibu kama kuku alivyojibu kuwa " kwa hiyo we Panya pambana na hali yako kwani huo mtego hautuhusu sisi Bali ni wako"
Basi panya hakupata masaada ilibidi ajihadhari mwenyewe kutokamana na mtego husika.
Usiku mmoja nyoka alipita karibu na ule mtego na kuugusa ndipo akanaswa mkiani.
Mwenye nyumba akajua mhalifu wake ashampata, akapeleka mkono gizani achukue mtego na panya alienaswa, ghafla akang'atwa na yule nyoka.
Mwenye nyumba ilibidi kupelekwa hospitali kwa matibabu, wakati anaendelea na matibabu kuku alichinjwa kwa ajili ya kitoweo cha mgonjwa.
Baadae mwenye nyumba alifariki, mbuzi na ng'ombe walichinjwa ili watu waliokusanyika kwenye ule msiba wapate chakula.
"..Mtego wa panya ulioua ng'ombe, mbuzi na kuku.."