Nchemba: Kazi za serikali zifanyike Dodoma ili kuwasogezea wananchi huduma

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba amesema kazi za serikali zifanyike makao makuu ya nchi, Dodoma, ili kuwasogezea Watanzania huduma.

“Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu mwelekeze Katibu Mkuu atengeneze timu ifanye tathmini ya majengo yote ya Serikali yaliyoko Dar es Salaam ambayo hayana matumizi ili tuyagawe kwa taasisi nyingine ambazo zimepanga, angalia Serikali ina majengo yasiyotumika”

Kadhalika Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema kwa kuwa Ofisi za Serikali zipo karibu, hivyo hakuna haja ya kuandikiana barua za masuala mbalimbali ya utekelezaji badala yake waweke mpango wa kutembeleana katika ofisi husika ili kutatua jambo lilikokwama kwa wakati”

Akizungumza na Watumishi wa Wizara ya Maji Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewataka kwenda katika hatua ya kukomesha kabisa upotevu wa maji. “Tunapokwenda kutekeleza dira mpya tunatakiwa twende na ustaarabu na miundombinu inayomuhakikishia mtanzania uhakika wa kupata maji”

Akizungumza wakati akikagua majengo ya Wizara ya Madini, mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewataka wataalam wa madini kuendeleza jitihada kwenye tafiti za madini ili kujua utajiri uliopo nchini.

Kwa Upande wake, Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya maamuzi ya kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi kubwa zilizowahakikishia watumishi mazingira mazuri ya ufanyaji kazi.

Naye, Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo umesaidia kutekeleza maagizo ya Rais Dkt. Samia ya kuhakikisha huduma zote zinatolewa katika eneo hilo, watanzania wote waliokuwa wanapata changamoto ya kupata huduma kwasasa changamoto hiyo imeondoka"
 
𝗧𝗨𝗡𝗔𝗧𝗔𝗞𝗔 𝗞𝗔𝗭𝗜 𝗭𝗔 𝗦𝗘𝗥𝗜𝗞𝗔𝗟𝗜 𝗭𝗜𝗙𝗔𝗡𝗬𝗜𝗞𝗘 𝗠𝗔𝗞𝗔𝗢 𝗠𝗔𝗞𝗨𝗨 𝗬𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜 - 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗪𝗜𝗚𝗨𝗟𝗨

Asisitiza Taasisi za Serikali zinapaswa kufahamu kwamba makao makuu ya nchi ni Dodoma

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa Serikali inataka kazi zote zifanyike makao makuu ya nchi ili kusogeza huduma karibu na Wananchi.

Amesema hayo leo Alhamisi (Januari 22, 2026) alipotembelea Ofisi za Wizara ya Maji na Wizara ya Madini zilizopo mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.

“Ninawapongeza sana, mmehamia Makao Makuu, taasisi zote za Serikali zinapaswa kutambua kwamba makao makuu ya nchi ni Dodoma, na huduma zote zinapaswa kutolewa hapa, hii sio kambi na wala hatutakuwa na Makao Makuu mbili zilizo sambamba”.

Pia, Mheshimiwa Mwigulu ameziagiza Taasisi zote ambazo zimeshakamilisha ujenzi wa majengo katika makao makuu kuyatoa majengo hayo kwa Taasisi ambazo haziwajibiki kuhamia Dodoma lakini bado zimepanga.

“Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu mwelekeze Katibu Mkuu atengeneze timu ifanye tathmini ya majengo yote ya Serikali yaliyoko Dar es Salaam ambayo hayana matumizi ili tuyagawe kwa taasisi nyingine ambazo zimepanga, angalia Serikali ina majengo yasiyotumika”

Kadhalika Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema kwa kuwa Ofisi za Serikali zipo karibu, hivyo hakuna haja ya kuandikiana barua za masuala mbalimbali ya utekelezaji badala yake waweke mpango wa kutembeleana katika ofisi husika ili kutatua jambo lilikokwama kwa wakati”

Akizungumza na Watumishi wa Wizara ya Maji Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewataka kwenda katika hatua ya kukomesha kabisa upotevu wa maji. “Tunapokwenda kutekeleza dira mpya tunatakiwa twende na ustaarabu na miundombinu inayomuhakikishia mtanzania uhakika wa kupata maji”

Akizungumza wakati akikagua majengo ya Wizara ya Madini, mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewataka wataalam wa madini kuendeleza jitihada kwenye tafiti za madini ili kujua utajiri uliopo nchini.

Kwa Upande wake, Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya maamuzi ya kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi kubwa zilizowahakikishia watumishi mazingira mazuri ya ufanyaji kazi.

Naye, Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo umesaidia kutekeleza maagizo ya Rais Dkt. Samia ya kuhakikisha huduma zote zinatolewa katika eneo hilo, watanzania wote waliokuwa wanapata changamoto ya kupata huduma kwasasa changamoto hiyo imeondoka"
 
Attachments

  • IMG-20260122-WA0018.jpg
    IMG-20260122-WA0018.jpg
    154.9 KB · Views: 28
  • IMG-20260122-WA0017.jpg
    IMG-20260122-WA0017.jpg
    113 KB · Views: 32
  • IMG-20260122-WA0020.jpg
    IMG-20260122-WA0020.jpg
    139.5 KB · Views: 27
  • IMG-20260122-WA0022.jpg
    IMG-20260122-WA0022.jpg
    181.9 KB · Views: 27
  • IMG-20260122-WA0023.jpg
    IMG-20260122-WA0023.jpg
    194 KB · Views: 25
  • IMG-20260122-WA0028.jpg
    IMG-20260122-WA0028.jpg
    198.5 KB · Views: 26
  • IMG-20260122-WA0027.jpg
    IMG-20260122-WA0027.jpg
    215.3 KB · Views: 41
  • IMG-20260122-WA0024.jpg
    IMG-20260122-WA0024.jpg
    207.8 KB · Views: 31
  • IMG-20260122-WA0026.jpg
    IMG-20260122-WA0026.jpg
    187.5 KB · Views: 31
  • IMG-20260122-WA0025.jpg
    IMG-20260122-WA0025.jpg
    186.8 KB · Views: 28
  • IMG-20260122-WA0019.jpg
    IMG-20260122-WA0019.jpg
    160.1 KB · Views: 26
  • IMG-20260122-WA0021.jpg
    IMG-20260122-WA0021.jpg
    156.5 KB · Views: 31
Nikisema huyu jamaa elimu yake inatilia mashaka, kuna watu hawanielewi. Nikisoma hii taarifa inashangaza sana kauli zake.

Unaposema kwa kuwa taasisi zipo karibu kwa hiyo inapotokea tatizo, wasiandikiane barua bali watu watoke, waingie kwenye V8 zao watembeleane wakamalize tatizo, hii ni kauli ya mtu mwenye akili timamu kweli?

Unaposema shughuli za serikali zifanyikie Dodoma pekee, ina maana gani? Juzi tulipohoji inakuwaje mamia ya watendaji wakuu walipelekwa Zanzibar wakati gharama kubwa imetumika kujenga Dodoma, tukajibiwa "Rais ana mamlaka inayomruhusu kufanya kazi popote. Kwanza kauli hiyo ya kwamba shughuli zote za serikali zifanyike Dodoma haina mantiki yoyote. Ofisi za serikali zilizopo maeneo tofauti ya nchi zifungwe watu wawe wanafunga safari kuzifuata Dodoma?

Anaongelea Sanduku la Posta, hivi uwekezaji wa mabilioni kwenye TEHAMA za serikali umefikia wapi hadi leo bado wanaongelea S.L.P au baada ya kuweka zile flat screen na ving'amuzi wakawa wamemaliza? Au kwa kuwa wanajua wanakata mitandao muda wowote wakijisikia kwa hiyo hawaiamini tena?

Ningeweza kuendelea ila nadhani mmenielewa.
 
Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba amesema kazi za serikali zifanyike makao makuu ya nchi, Dodoma, ili kuwasogezea Watanzania huduma.

“Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu mwelekeze Katibu Mkuu atengeneze timu ifanye tathmini ya majengo yote ya Serikali yaliyoko Dar es Salaam ambayo hayana matumizi ili tuyagawe kwa taasisi nyingine ambazo zimepanga, angalia Serikali ina majengo yasiyotumika”

Kadhalika Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema kwa kuwa Ofisi za Serikali zipo karibu, hivyo hakuna haja ya kuandikiana barua za masuala mbalimbali ya utekelezaji badala yake waweke mpango wa kutembeleana katika ofisi husika ili kutatua jambo lilikokwama kwa wakati”

Akizungumza na Watumishi wa Wizara ya Maji Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewataka kwenda katika hatua ya kukomesha kabisa upotevu wa maji. “Tunapokwenda kutekeleza dira mpya tunatakiwa twende na ustaarabu na miundombinu inayomuhakikishia mtanzania uhakika wa kupata maji”

Akizungumza wakati akikagua majengo ya Wizara ya Madini, mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewataka wataalam wa madini kuendeleza jitihada kwenye tafiti za madini ili kujua utajiri uliopo nchini.

Kwa Upande wake, Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya maamuzi ya kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi kubwa zilizowahakikishia watumishi mazingira mazuri ya ufanyaji kazi.

Naye, Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo umesaidia kutekeleza maagizo ya Rais Dkt. Samia ya kuhakikisha huduma zote zinatolewa katika eneo hilo, watanzania wote waliokuwa wanapata changamoto ya kupata huduma kwasasa changamoto hiyo imeondoka"
Ninaunga mkono hili,but he has to practice what he is preaching...
 
Dpdoma wapo wananchi ila dar wapo wageni wafanya vurugu kutoka nje!
 
Back
Top Bottom