Nchi 15 duniani zinazoogopwa kwa uchawi na ushirikina

Nchi 15 duniani zinazoogopwa kwa uchawi na ushirikina

Wabongo leo lazima watatafta namba za simu za walofanya utafiti huo, kisha waanze kulia ni hujuma, inakuwaje tz haijawai nambari moja? 😀
 
Uwe unasoma vizuri na sio kukurupuka tu kama kichaa , ndio maana huwa mnafeli kijinga mitihani, wapi hapo umeona Tanzania ni ya Pili????
Atakua ni mchawi [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Oya yakhe! Sisi ni wateja tu, nyie ndio viwanda kabisa hadi dunia inawafahamu. Kwanza kipindi cha kampeni ndio albino wanakipata pata aise, wananyofolewa viungo bila huruma Tanzania yote, na kwamba inatendeka sana wakati wa kampeni za uongozi wa nchi, ina maana ni shughuli inayofanywa na viongozi wenu.

Anyway nia haikua kuelekeza kidole, maana hili tatizo lipo Afrika yote, ni aibu sana hata SA ambayo tulitegemea ituongoze kwenda kwenye first world na wao wanatajwa kwenye upumbavu huu. Dark continent with dark people in darkness.....
Haya nimerudi, lakini kifupi ni hivi, uchawi ni sawa na rushwa. Mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni wala rushwa. Hivyo mtoa huduma ya uchawi na mtumia huduma ya uchawi wote ni washirikina.
 
Haya nimerudi, lakini kifupi ni hivi, uchawi ni sawa na rushwa. Mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni wala rushwa. Hivyo mtoa huduma ya uchawi na mtumia huduma ya uchawi wote ni washirikina.

Hehehe!! Sielewi mbona unatumia nguvu nyingi kujitetea hivyo, nilishakubali kwamba Afrika tumelaaniwa. Kwa kifupi ninaelewa kahaba na mnunuzi wote malaya hakuna wa kumcheka mwengine. Hili la ushirikina linaniuma Afrika yyangu hii, japo nyie bana kuchinja albino hapo huwa mnapitiliza, bora mngeishia kuyafanya kama wenzenu Wanigeria na kwengineko, lakini kusaka watoto albino na kuwachinja kinyama wakati wa kampeni ili viongozi washinde kwa kura, ni aibu tupu.

Ushirikina umeghubika hili bara lote, watu hawataki kuanza biashara bila kupitia kwa mganga. Hapo Bongo nilishangaa kampuni ya kiteknolojia, yaani ICT lakini mmiliki anaamini kwa haya mambo, alikua mama fulani, yaani asubuhi na mapema anaamka na kupasua nazi kwenye milango ya ofisi huku akifoka maneno ya kiajabu ajabu. Nilikua nimealikwa kuwasaidia kwenye masuala ya kiufundi lakini vioja vya huyo mimi viliniacha hoi bila kujua aidha nimcheke au nimhuzunikie.

Hatimaye alifunga biashara kwa kufilisika, ilikua kampuni ya kusambaza huduma za internet na simu, yaani a very advanced infrastructure lakini mtihani.
 
Hehehe! Bonyeza link uone zimepangwa kuanzia namba 15 hadi moja ya chini.
Umekurupuka mkuu,hiyo list kukosekana kwa senegal,nigeria na india inaonyesha ni jinsi gani ulivyokurupuka
 
Naaamini hata ungechukua top ten, Tz tungekuwemo!

Inamaana Nigeria hawapo?
Duh! Ninamashaka na utafiti
 
Hehehe!! Sielewi mbona unatumia nguvu nyingi kujitetea hivyo, nilishakubali kwamba Afrika tumelaaniwa. Kwa kifupi ninaelewa kahaba na mnunuzi wote malaya hakuna wa kumcheka mwengine. Hili la ushirikina linaniuma Afrika yyangu hii, japo nyie bana kuchinja albino hapo huwa mnapitiliza, bora mngeishia kuyafanya kama wenzenu Wanigeria na kwengineko, lakini kusaka watoto albino na kuwachinja kinyama wakati wa kampeni ili viongozi washinde kwa kura, ni aibu tupu.

Ushirikina umeghubika hili bara lote, watu hawataki kuanza biashara bila kupitia kwa mganga. Hapo Bongo nilishangaa kampuni ya kiteknolojia, yaani ICT lakini mmiliki anaamini kwa haya mambo, alikua mama fulani, yaani asubuhi na mapema anaamka na kupasua nazi kwenye milango ya ofisi huku akifoka maneno ya kiajabu ajabu. Nilikua nimealikwa kuwasaidia kwenye masuala ya kiufundi lakini vioja vya huyo mimi viliniacha hoi bila kujua aidha nimcheke au nimhuzunikie.

Hatimaye alifunga biashara kwa kufilisika, ilikua kampuni ya kusambaza huduma za internet na simu, yaani a very advanced infrastructure lakini mtihani.
Ha haaaaa! Nguvu nyingi wakati nimeandika aya moja yenye maneno kama 30 tu?

Haya tuyaache, kiukweli suala la mauaji ya albino lilitutia doa kubwa. Sasa hivi limeisha lakini kwa sababu lina historia ya kutokea ni kama bado lipo kinadharia. Hilo kiukweli lilitia doa taifa hili, itatuchukua miaka kufuta kovu hilo.

Masuala ya ushirikina kama ulivyosema hapa Africa ilishakuwa kama fashion. Yaani ni aibu kabisa na ndo maana inarudisha nyuma maendeleo.

Ila huwa nadhani baadhi ya wachina nao ni washirikina, inasemekana eti huwa wanapenda kujenga madaraja usiku tu. Sijui hili ni suala la kikandarasi au niaje, me sio mhandisi so sijui
 
Back
Top Bottom