Nchi gani hapa Afrika Mashariki ni bora kwa kuanzisha maisha?

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
2,317
Reaction score
7,808
Wakuu Niko serious naomba nielekezwe Kwa wale ambayo wamefanikiwa kutembea nchi mbalimbali, nilifanikiwa kufika Nairobi miaka Fulani nyuma, lakini lifestyle Yao sikuipenda ni nchi ambayo vurugu na Fujo ziko juu sana, kiasi kwamba mbeleni wanaweza kuwa kama AFRICA KUSINI TU,

Nimefikiria hovyo kwasababu naangalia nchi ambayo inakuwa na utawala wa Sheria, ambayo Kwa nchi nyingi hapa EA hamna, hii nchi Kila Kona ni malalamiko tu, hakuna kupumua yaani any startup katika field yoyote ile chance ya kufirisika ni kubwa kuliko kufanikiwa, haimaanishi kwamba hakuna kufanikiwa lakini moto lazima uuone,

Sitaki nchi ambayo ni maskini, wananchi wake wamechoka wanashindwa kuafford basic needs ila wao wanazidi kuongeza Kodi na kujisifia wameongeza Kodi bila kujali wanaokamuliwa, wanaongeza Kodi kwenye magari used wakati wananchi wake hawawezi kununua magari mapya.

Nchi ambayo viongozi wanaishi kama malaika, wanakamua wananchi alafu wakikutana wanagonga cheers wakiwa mbele ya public ni kueneza propaganda na kujifanya wana uchungu na nchi.

Nipo tunduma, navuka boda kwenda Zambia, Botswana, then Namibia, nipo na ujuzi mkubwa wa umeme wa magari, hope mambo yatakuwa vizuri.

Nitatoa update Kwa Kila nchi nitakayoitembelea, labda nitarudi 2040.
 
Nenda Zambia apo Ndola upige tungi mkuu, maisha ndo hayahaya
 
Sasa mkiondoka wote sisi Tanzania tunabakije
 
Nenda Rwanda hutajuta.
Umeshawahi kufika Rwanda?
Nilikuwa kule miaka ya mwanzoni mwa 2000 kibiashara, Nilifikia maeneo ya Majerwa...
Huko ndio kuna yardi ya magari makubwa yote yanapofikia na kushusha mzigo,,,
Kuna hoteli na mabar yamechangamka....
Wiki ya kwanza ilienda poa, ni kula maburusheti na primus....
Wiki ya pili, jioni tunavinjari, mara Landcruiser kama kumi zilitokea na kufunga mitaa, tunashtukia tunaambiwa tukae chini, wajeda wa kitusi wako full masi nondo na mijegejo,
Kila mmoja wetu alitakiwa kujieeleza na kutoa kitambulisho, yaani eneo lote lilipigwa lockdown
Uzuri nilikuwa na paspoti yangu kwenye mfuko wa shati imegongwa border, wakaniachia....
Baada ya hapo unasikia tu stori wabongo kibao wako jela kwa kuishi bila makaratasi.
Sijui sasa kukoje, ila pia mwenyeji wangu alikuwa mbongo kalowea huko na mtoto wa kinyarwanda na wana familia, lakini bado alikuwa anasumbuliwa na Chef de Masion yaani balozi wa mtaa bila sababu ila jamaa anasema ni kwa kuwa kaoa mnyaruanda mtusi.
 
Nenda popote ila epuka kuishi hizi nchi, Tanzania, Uganda, burundi, Congo, Msumbiji, Zimbabwe.
Nchi ikishakosa uongozi mzuri automatic hata fursa kwa wageni kuzifaidi huwa ngumu.

Ewe raia kama unao uwezo wa kusepa hii nchi we sepa ikiwezekana kusanya na nduguzo muondoke
 
Back
Top Bottom