Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Nichukue fursa hii kuwaambia watanzania kwamba huenda future yetu si nzuri sana. Hii ni kwa tafsiri ya kwamba pasipo na haki popote amani haiwezi kupatikana. Kama ipo amani ni ya kulazimisha tu kwa maana ya uvumilivu.
Haiwezekani mtu anaamka anaamua kuvunja katiba ya nchi makusudi kabisa kwa vile yeye ni kiongozi wa mhimili.
Spika Ndungai hawezi kuamua kuingiza wabunge ambao hawatambuliwi na chama chochote cha siasa bungeni.
Si kazi ya spika kutambua uhalali wa mbunge, ni kazi ya mahakama kutafsiri sheria ya uhalali ikiwa chama kimemkataa. NEC haina mamlaka kisheria kurejesha au kupeleka jina la mbunge ambaye hatambuliwi na chama cha siasa, inatakiwa kupokea jina kwenye chama na kuiwasilisha bungeni.
Narudia tena si kazi ya spika kutambua uhalali wa mtu kuwa mbunge.
Asijivike majukumu yasiyomhusu, afuate katiba ya nchi. Awaache wao wakitafuta haki yao mahakamani, katiba haiseme spika atetee kila mbunge, kuna uutaratibu wake.
Mbona hakusimama kumtetea mama Sophia Simba alipoulizwa ubunge na uanachama CCM?
Hili taifa kuna waliovuja jasho na kulala nje mpaka tukapata uhuru na katiba ya nchi. Tusilichezee taifa hili mwisho wa siku tukalaumiana wakati wanaoliharibu wanaweza kudhibitiwa.