Nchi ikiongozwa na mtu kama Rais Samia lazima watu wake wawe na furaha na biashara zitashamiri kama ilivyo sasa

Nchi ikiongozwa na mtu kama Rais Samia lazima watu wake wawe na furaha na biashara zitashamiri kama ilivyo sasa

Ubepari sio jambo baya kama taifa litakuwa na idadi kubwa ya wasomi na wataalamu kama nchi kama china na India
Ubepari mzuri mwanzoni. Fursa kibao watu wanasonga maisha. Baadaye utajiri na fursa zote zinaangukia kwenye mikono ya wachache. Hata hao masomi wanaishia kuwa vibarua na manamba. Tena sasa ubepari umejigeuza kuwa kitu kinaitwa Technofeudalism ambacho ni hatari zaidi.
 
Watanzania tuachane na mentality za kijamaa zakuwapa majimbo watu wasio na nyumba wala utajiri wowote. Tuwakatae watu wasio na business mind kuongoza nafasi za kisiasa nchini kwetu.

Kuendelea kuwa na viongozi wa kisiasa wanawaza kila saa kwamba wanaibiwa nikukosa exposure. Tuwe na viongozi wanatake risk katika kufanya maamuzi.

Tukiendelea kuwa na viongozi wanaohubiri umaskini tunakosesha Taifa baraka na kudidimiza uchumi wa wenye nacho hasa pale wanapolazimika kufanya kazi wawalishe wengine.

Tumeona mama Samia anavyotoa uhuru kwa matajiri kukaa viti vya mbele huku akiwakawakutanisha na matajiri wa ulimwengu wa kwanza. Mama anafanya kila awezalo anaposafiri aambatane na watu kadhaa atakaowapa connection kwa sababu anajua wakipata watamsaidia kupunguza tatizo la ajira nchini.

Mimi binafsi nampongeza na nitazidi kumpongeza mama kwa kufungua nchi. Hii miaka mitatu ya utawala wake nimejitokeza kumpa maua yake.

Mtu yeyote anayejituma kwa utawala huu lazima atoboe.....ila kama unaishi kwa kubeti utasubiri uzeeke uwe mchawi na kuona wenye mafanikio freemason

Mama endelea kutuletea watu waliostaarabika lakini piga chini wateule wake wanaotumia mwanya wa kiti chao kulazimisha matajiri wawaheshimu wakijidai usipomtoa atakufix.

Ukisikia mteule wake anakuambia watu flani ni wezi muulize kwanini awapo polisi? Muulize kwanini ajawafisha TRA na TAKUKURU?

Mama teua matajiri walinde utajiri wetu kuliko kujazana na maskini wanaowaza kukwamisha waliofanikiwa.

Kila la kheri mama piga kazi matajiri tupo nyuma yako
Utakuwaje na furaha wakati huna kila kitu halafu wanafaidi wengine kwa wizi? Majizi ndo yana furaha
 
Hamna shukran ndio mana awamu ile mli ipatapata sijui mnatka mtu ashuke mbinguni ndio muone mmepata kiongozi bora

watu km nyny ndio mnosababisha kupata kiongozi km awamu ile sababu ham elweki
Yaani mimi na akili zangu timamu niwe na shukrani na kiongozi wa ccm! Ananisaidia ni katika maisha yangu ya kila siku! Wewe utakuwa na matatizo upstairs bila shaka.
 
Zaidi ya robo tatu ya watanzania ni maskini.Biashara wakianzisha zinakufa kutokana Kodi kubwa za TRA.Andiko lako kundi hili halikuelewi
 
Back
Top Bottom