Nchi iko pagumu sana. Trust me, tunajipa moyo tu

Nchi iko pagumu sana. Trust me, tunajipa moyo tu

Kuna kitu kinakula moyo wangu I finally must vent out.

1. Nimevuna gunia 200 baada ya kulima ekari 20 za mahindi nataka kupeleka sokoni bei ya gunia tshs elfu 30, so nitapata million sita nikiuza yote. Kweli jamani this is too much. The leadership is seriously imposing new tax? Mnashindwa kuadress market challenges kwa watu million 45 walioko Shamba? Really????

2. Kuna influx ya vyuo Vya afya now than ever before. Ni mwendo Wa lab technician's, nursing, pharmacy, medical assistance courses etc. Nimeproject in 5 years to come tutakuwa na mrundikano Wa wataalamu Wa afya kuliko kawaida watakaokuwa hawaajiliki. Utapeli utaanza, kila chumba kitakuwa hospital bubu, madawa kuuzwa ovyo nk hii imeshaanza njmeiona somewhere. Afya zetu zitakuwa rehani. Ni kama hakuna sekta nyingine za kutrain serikali na taasisi binafsi zote ziko huko now. Sioni influx ya trainee kwenye lead productive sectors.

3. Ajira hakuna, kila mtu sasa analima masoko hakuna, mbinu za kujenga uchumi unaokuwa sizioni serious. Kuna ahadi tu za kuendelea kujengewa majengo mengi ya huduma mbalimbali za serikali bila kujenga watu Vya kutosha.

4. Nikirudi kwenye mfumuko Wa bei bei za mafuta, visavis gharama za uzalishaji wa mazao tozo barabarani usumbufu wa wakaguzi mazao, matrafiki, nk nk naishiwa hamu kabisa.

5. Ukiwaangalia viongozi concentration haipo kudeal na 80 % ya walipo watz inadeal na vitu very Petty.....

6. Upigaji umerudi kwa kasi ya ajabu. Sasa hivi kila ofisi ya umma hasa hizi nyeti zisizokwepeka deal zinapigwa balaa

My question is....watoto wetu wataikuta Tanzania ya namna gani sijui.

Jamani eeeh sijui kama hii tabu naipata Mimi tu. Kuna majibu hapa

Its soo frustrating.
Its true, hasa nshu No. 2. Hususan hiz Lab zilizozagaa mitaan,,, Daaah yaan unakuta mtu anapimwa mRdt na unaona kabisa, haf majib unambiwa una Malaria tatu (3mps/200wbc).

Wanawake ndo kupigwa power safe kila kukicha, eeet una UTI sugu,,, duuh yaan wanasahau kuwa wao ndo wanakutengenezea usugu wa dawa kwenye Mwili wako.

Unakuta ki Lab kidogo, unaambiwa tunafanya Culture, Fbp, Uric acid, mara oooh tunaushirika na Hospital kubwa, na ww kwa kuwa hujui unalipa Cash,[emoji23] kumbe maskini ya Mungu Majibu yako yanapikwa,,,,
Yaan ni mwendo wa kuedit taari zako then unapewa majibu.[emoji23] [emoji23]

POLE YETU WA,,, TANZANIA
 
Nani wa kujenga? Hiyo ni Kazi ya sekta binafsi..Huyo unaemtaja hapa kajenga viwanda kwenye masoko sio wanakozalisha..

Unadhani sekta ya kilimo ni rahisi kama kuandika andika?
Mkuu, sijui ni hasira, au kutaka uonekane wewe ni mjuaji kuliko wengine kwa aina ya majibu unayowajibu wachangiaji wengine!

Chukulia mfano huu hapa. Kuna tatizo gani la kuweka kiwanda palipo na mazao ghafi halafu yakichakatwa yanapelekwa sokoni kwa walaji?

Eleza hilo kwa ufahamu wako bila ya kuonyesha ujuaji ili wengine wafaidi ujuaji wako.

Mbona hawa akina Bakresaa wanasafirisha bidhaa zao nchi nzima, inashindikana kutoa huko kwa wakulima na kusambaza kwingine walipo walaji? Mbona siku zote tunasikia miundombinu inatengenezwa ili kurahisisha biashara, hili halihusu bidhaa zilizo tayari kumfikia mlaji; tatizo ni nini? Eleza kwa utulivu nasi tukusome. Usidharau uelewa wetu. Tutakuelewa tu ukieleza vizuri.
 
Tukiendelea na hiki kilimo cha kufunga mipaka ipo siku nchi itaingia kwenye njaa kubwa sana. Maana mwakani mtu kama wewe hutalima, wezee tu ndiyo watabaki kulima.

Inabidi upelekwe mswada Bungeni ambao itakuwa ni marufuku serikali kumzuia mkulima kuuza mazao yake atakako. Ukienda South Sudan, Congo au Kenya huwezi kuta gunia 30 elfu.

Kiufupi nchi yetu inaendeshwa kwa mazoea, hakuna cha ubunifu wala mipango yenye akili.
Hao watoto wa watumwa walilima wapi ili kuelewa maswala ya kilimo?
 
Its true, hasa nshu No. 2. Hususan hiz Lab zilizozagaa mitaan,,, Daaah yaan unakuta mtu anapimwa mRdt na unaona kabisa, haf majib unambiwa una Malaria tatu (3mps/200wbc).

Wanawake ndo kupigwa power safe kila kukicha, eeet una UTI sugu,,, duuh yaan wanasahau kuwa wao ndo wanakutengenezea usugu wa dawa kwenye Mwili wako.

Unakuta ki Lab kidogo, unaambiwa tunafanya Culture, Fbp, Uric acid, mara oooh tunaushirika na Hospital kubwa, na ww kwa kuwa hujui unalipa Cash,[emoji23] kumbe maskini ya Mungu Majibu yako yanapikwa,,,,
Yaan ni mwendo wa kuedit taari zako then unapewa majibu.[emoji23] [emoji23]

POLE YETU WA,,, TANZANIA
Haya ni matatizo madogo sana.
Lakini nataka nimjibu mleta mada kwa pamoja nitakapomaliza kusoma yote yaliyowekwa kwenye mada yake.
 
Simu yng haiwezi kufungua hiyo attachment, nifikishie ujumbe wako kwa namna nyingine.

Hata hicho kifungu cha Bible sijakuelewa, sijui muda Nchu idumupo mala majira.
1631651244948.png
 
Dunia Tunapita... Tengeneza Kesho ilio bora sababu ndio Makazi ya Kudumu...
1. Huko ikiwa shida Ya milele
2.Huko ikiwa Rah Ya milele.
 
Kuna kitu kinakula moyo wangu I finally must vent out.

1. Nimevuna gunia 200 baada ya kulima ekari 20 za mahindi nataka kupeleka sokoni bei ya gunia tshs elfu 30, so nitapata million sita nikiuza yote. Kweli jamani this is too much. The leadership is seriously imposing new tax? Mnashindwa kuadress market challenges kwa watu million 45 walioko Shamba? Really????
Na wewe mkuu inakuwaje unalimwa ekari 20 halafu unaishia gunia 200? Maanake ni gunia 10 kwa ekari! Utakuwa ulilima kienyeji!
 
Watu wapo bize kugawana vyeo,halafu mwisho wa siku wanakuzuia kuuza nje ya nchi kama vile kwenye kulima walikusaidia
Mi nadhani ni 'complicated' zaidi ya hii misemo ya "...wanakuzuia kuuza nje ya nchi..." tunayokimbilia kuitumia kila mara kama ndicho kielelezo cha tatizo ambalo kikiondolewa hali ya mkulima itaneemeka hapo hapo!
 
Serikali haina ya kukwepa kuhusu hili,unafikiri serikali ikiamua inashindwa?

Kwanini serikali na viongozi wake wanawahimiza vijana kwenda shambani wajiajiri wakati kuwatafutia masoko shida?

Tantrade na sijui taasisi inaitwa MAZAO mchanganyiko zinafanya nini? Serikali ina taasisi nyingi zinazoshughulikia MASOKO lakini wanakula mishahara tu na bi mkubwa anawaangalia

Serikali ina mkono mrefu na ngumu kukwepa hili mkuu.
Mkuu 'misasa', tunazunguka tuuu na maneno mengi lakini nadhani sote tunajua tatizo lilipo.

Tatizo lipo huko huko kwenye hiyo serikali unayosema "ina mkono mrefu", lakini haina uwezo wa kuutumia mkono huo mrefu kwa manufaa ya wananchi wake.

Tatizo ni nini? UZEMBE.

Nchi hii hata kutafuta na kuweka takwimu sahihi tu ni shida tupu!
Serikali katika hali ya kawaida kabisa ingeweza kuwa na uwezo wa kujua kiasi cha mazao yanayotegemewa kuzalishwa katika msimu fulani, kabla hata mazao hayajavunwa.
Serikali inao uwezo wa kupata taarifa za masoko duniani kote kabla ya mazao hayajavunwa; na kujua ni nchi gani zitakuwa na uhitaji mkubwa wa mazao hayo, kabla ya msimu wa mazao husika. Hii siyo kazi ya kubahatisha unayoanza kuifanya wakati tayari mazao ya wakulima yakiwa ghalani!

Serikali ina uwezo wa kujenga maghala ya kuhifadhia mazao ya ziada ili kama soko hali siyo nzuri mazao ya wakulima yahifadhiwe, yasiharibike ili soko likipatikana yauzwe.

Serikali ina uwezo kabisa wa kufanya mipango ya kuwakaribisha wawekezaji ili kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa kwa ziada. Mfano. Mahindi siyo chakula cha binaadam pekee. Mahindi yanatoa mafuta ya kula, nasi hapa tunao uhaba mkubwa wa mafuta ya kula, mbona hatutumii mahindi kutuzalishia bidhaa hiyo?
Mahindi yanatengeneza "ethanol' inayoweza kuchanganywa kwenye petroli ili tupunguze gharama za uagizaji wa mafuta, n.k., nk..
Kama kuna malighafi ya kutosha na ya kuaminika (mahindi) itashindikana vipi kuwapata wawekezaji wa kuitumia malighafi hii?

Hebu angalia, kuna wakati ilipigwa kelele nyingi kuhusu zao la mihogo na utengenezaji wa wanga. Kiwanda kikajengwa, nadhani Ruangwa kwa Majaliwa. Wakulima wa mihogo nao sijui ilikuwaje, kiwanda kikasuasua hadi leo hakisikiki

Serikali, kama ulivyosema, ina wajibu wa kuyasimamia mambo haya, si swala tu la kuyapigia kelele kwa msimu na kuyaacha yafe!

TATIZO LIPO SERIKALINI, SIYO KWA WAKULIMA.
 
Mkuu haka kauzi ni kazuri sana.
Kuhusu hili la afya asee baada ya muda tutaona hasahasa kwenye phamacy na nursing.
Yameshanikuta.
Mimi mfugaji wa kuku. Kila nikipeleka kuku mgonjwa unaambiwa dawa yake hii hapa. Unawapa kuku ndio wanazidi kufa.
Kuku nimewapa kila aina ya chanjo Kama nielekezavyo na Hawa makanjanja, kuku wamekufa Banda Zima.
Kuna maabara nyingi sana ambazo wanapima damu, mavi, mkojo na kutoa ushauri. Huku ndio ambako maskini wa kitanzania wanakopewa ushauri wa kuondoa uhai wao.
Walah kwenye hizi maabara lazima uonekane na tatizo. Especially. UTI, TYPHOID NA NYEGE
 
Nchi anayoongelea Hapo ni Ardhi (Land). Soma Biblia ya Kiingereza
 
Kwamba
Aisee gunia zote hizo lazima umetumia gharama kubwa,
Anamaanisha kwamba hela moja inatoa gunia 10 sio au nakosea???? Wakulima hebu mje tujadili hili na ametumia mbegu gani aisee?
 
Yameshanikuta.
Mimi mfugaji wa kuku. Kila nikipeleka kuku mgonjwa unaambiwa dawa yake hii hapa. Unawapa kuku ndio wanazidi kufa.
Kuku nimewapa kila aina ya chanjo Kama nielekezavyo na Hawa makanjanja, kuku wamekufa Banda Zima.
Kuna maabara nyingi sana ambazo wanapima damu, mavi, mkojo na kutoa ushauri. Huku ndio ambako maskini wa kitanzania wanakopewa ushauri wa kuondoa uhai wao.
Walah kwenye hizi maabara lazima uonekane na tatizo. Especially. UTI, TYPHOID NA NYEGE
Jamaa mmoja aliniambia hao madaktari wa wanyama na hizo maduka za dawa Kuna uhuni huwa inafanyika, let me explain;

Unakuta mfugo wako anaumwa ugonjwa fulani, unamuita daktari wa wanyama, anakuja anamuattend mnayama wako then anakuandikia dawa kama sita hivi.

In short unakuta dawa hapo labda inayotibu ugonjwa ni moja au mbili tu Ila inabidi afanye dili auze na nyingine nyingi ili wapate hela.

Ni sawa na binadamu anaumwa dokta anajua kabisa hii ni mafua Ila ankupa lundo la madawa ili tu wauze dawa. Maana unakuta hauna labda homa, au huujapoteza appetite Ila atakupa antibiotics, analipa Panadol au paracetamol hata kama hauumwi kichwa au hauna homa, atakuandikia na piriton, anaweka na sijui dawa za mafua kuzuia makohozi Yani inapigwa dozi ya kufa mtu wakati hayo mengine hata hauumwi.

Nyingine unakuta wanaweka maji kwenye zile dawa anakuja anajifanya anazichanganya kumbe ulimpa dawa za laki yeye ananunua za 30,000 anamix na madude anayojua so mnyama wako anakuwa hapati Ile doxi kamili.

Am not saying wote wanafanya hivi Ila kiukweli malalamiko ni makubwa sana kutoka kwa wqfugaji so let's be awake.
 
magunia 200 kwa eka 20 ni sawa na gunia 10 kwa eka -kiwango kidogo mno.Ukizingatia kanuni za kilimo bora -mbegu ,mbolea,pest control unavuna hadi magunia 30 kwa eka maize zones.
 
Kuna kitu kinakula moyo wangu I finally must vent out.

1. Nimevuna gunia 200 baada ya kulima ekari 20 za mahindi nataka kupeleka sokoni bei ya gunia tshs elfu 30, so nitapata million sita nikiuza yote. Kweli jamani this is too much. The leadership is seriously imposing new tax? Mnashindwa kuadress market challenges kwa watu million 45 walioko Shamba? Really????

2. Kuna influx ya vyuo Vya afya now than ever before. Ni mwendo Wa lab technician's, nursing, pharmacy, medical assistance courses etc. Nimeproject in 5 years to come tutakuwa na mrundikano Wa wataalamu Wa afya kuliko kawaida watakaokuwa hawaajiliki. Utapeli utaanza, kila chumba kitakuwa hospital bubu, madawa kuuzwa ovyo nk hii imeshaanza njmeiona somewhere. Afya zetu zitakuwa rehani. Ni kama hakuna sekta nyingine za kutrain serikali na taasisi binafsi zote ziko huko now. Sioni influx ya trainee kwenye lead productive sectors.

3. Ajira hakuna, kila mtu sasa analima masoko hakuna, mbinu za kujenga uchumi unaokuwa sizioni serious. Kuna ahadi tu za kuendelea kujengewa majengo mengi ya huduma mbalimbali za serikali bila kujenga watu Vya kutosha.

4. Nikirudi kwenye mfumuko Wa bei bei za mafuta, visavis gharama za uzalishaji wa mazao tozo barabarani usumbufu wa wakaguzi mazao, matrafiki, nk nk naishiwa hamu kabisa.

5. Ukiwaangalia viongozi concentration haipo kudeal na 80 % ya walipo watz inadeal na vitu very Petty.....

6. Upigaji umerudi kwa kasi ya ajabu. Sasa hivi kila ofisi ya umma hasa hizi nyeti zisizokwepeka deal zinapigwa balaa

My question is....watoto wetu wataikuta Tanzania ya namna gani sijui.

Jamani eeeh sijui kama hii tabu naipata Mimi tu. Kuna majibu hapa

Its soo frustrating.
Kifupi tutazamie tozo zikiongezeka zaid! Hakuna nafuu
 
Back
Top Bottom