Uchaguzi 2020 Nchi imeamka ikiwa na huzuni kubwa sana, Kwamba wabunge wote Bara 100% wameshinda wa CCM

Uchaguzi 2020 Nchi imeamka ikiwa na huzuni kubwa sana, Kwamba wabunge wote Bara 100% wameshinda wa CCM

This is too much. Hata sisi wana-CCM hatujafurahia. Level ya ubunge ngoma ingeachwa fair at least tukawapata wabunge cream kutoka na upinzani. Ambao kwa ukweli wamekuwa na mchango mkubwa sana sana toka 1992. Leo hii tunaingia kwenye bunge ambalo wabunge wote ni CCM 100%kutoka bara. Labda wa ACT kutoka Pemba kuingia bunge wa JMT, ila napo it depends na kama watakubali au itakuwa kama last time.

Kwa hakika ni uzuni. na wananchi tusishangilie hili. Nchi imeingia katika majaribio makubwa sana. kwa wale slow learners mtaanza kuona madhara yake not even far just 2022.
P
 
Akili kama hii ndio tatizo la nchi hii. Kwani hata waliobaki waliufanyia nini mpaka ukajiona ni bora leo kuliko mwaka 2014?? Hujui hata nyakati tulizopo, mbunge wa upinzani hawezi kuizuia kufanya chochote serikali kwa aina ya katiba tuliyonayo. Kimsingi, Bunge haliwezi kuizuia serikali kufanya chochote.

Nikukumbushe tu, bajeti na sheria kwa katiba yetu hupangwa na kutungwa na serikali na kuja kujadiliwa na kupitishwa na Bunge. Nchi wa wenzetu, Bunge ndio huwa chanzo cha matumizi na sheria. Serikali hutekeleza tu!!

Siko katika siasa lakini hata Bunge likiwa ni CCM tu, hakutaboreka kitu. Sana sana utaudhiwa zaidi kuliko ulivoudhiwa na habari ya wabunge wa upinzani kutoka nje. Watch my words!!
Mkuu umeongea hoja ila pia inakosa kujisimamia imekua tegemezi sana hoja yako, tuache bla blaa nyingi upinzani tujirekebisha mambo ya kulialia ni kipuuzi sana , tunajitia huruma nyingi kwa CCM ili iweje, CCM inahitaji upinzani mahiri sio hii ya formality tuliozoea, tubadilike kulialia sijui ndiyo mtapata haki, CCM haitaji huruma au sijui hizo justification unazozitoa bali inahitaji mpinzani wa kweli.
 
Mimi CCM sipendi iendelee kutawala LAKINI wapinzani niliwatoa maanani pale walipotangaza kushiriki uchaguzi mkuu wakati mwaka jana waliwalazimisha viongozi wao wa ngazi za chini kujitoa uchaguzi wa serikali za mitaa. Ninavyojua hakuna kilichobadilika tangu uchaguzi wa serikali za mitaa mpaka uchaguzi mkuu. Wametupotezea viongozi wazuri tu mitaani ambao wangeweza kushinda uchaguzi wa mwaka jana.
 
Sasa mbona unatokwa na povu, hii ni dhahiri wewe unaonyesha ni namna gani umekengeuka, hoja hujibiwa kwa hoja pasipo kutia kashfa kwa mtoa hoja, tuachane na hilo sasa hizo hoja zako zina kaa kweli kwenye mzani ukilinganisha na matokeo tunayoyapata leo? Matokeo nchi nzima wamechukua ccm hata kama ni kuiba wameibaje majimbo yote kata zote, zinduka we kilaza, wananchi wanachoka kuona tunawatuma viongozi wa upinzani na kususia vikao, pia vyama vya upinzani kuna adhabu za kipuzi sana kwa wanachama wao, ndani vyama vya upinzani hakuna demokrasia
Acha ufala wewe kwanini hamtaki katiba mpya , kwanini hamtaki tume huru ya uchaguzi,usijitoe ufahamu
 
Mkuu umeongea hoja ila pia inakosa kujisimamia imekua tegemezi sana hoja yako, tuache bla blaa nyingi upinzani tujirekebisha mambo ya kulialia ni kipuuzi sana , tunajitia huruma nyingi kwa CCM ili iweje, CCM inahitaji upinzani mahiri sio hii ya formality tuliozoea, tubadilike kulialia sijui ndiyo mtapata haki, CCM haitaji huruma au sijui hizo justification unazozitoa bali inahitaji mpinzani wa kweli.
Katiba ,kAtiba kAtiba. Tunarudi nyuma .tujiandae vikwazo vinakuja
 
This is too much. Hata sisi wana-CCM hatujafurahia. Level ya ubunge ngoma ingeachwa fair at least tukawapata wabunge cream kutoka na upinzani. Ambao kwa ukweli wamekuwa na mchango mkubwa sana sana toka 1992. Leo hii tunaingia kwenye bunge ambalo wabunge wote ni CCM 100%kutoka bara. Labda wa ACT kutoka Pemba kuingia bunge wa JMT, ila napo it depends na kama watakubali au itakuwa kama last time.

Kwa hakika ni uzuni. na wananchi tusishangilie hili. Nchi imeingia katika majaribio makubwa sana. kwa wale slow learners mtaanza kuona madhara yake not even far just 2022.

Nidiriki kusema haijawa njia sahihi na sio afya kwa demokrasia. Mapungufu na wizi ulikuwepo wa kiwango cha juu sana sana. Anyway, tumerudi nyuma hatua 30 katika demokrasia aliyotuachia Baba wa Taifa na Mzee Kikwete.

Hata Mwalimu Nyerere alikuwa anarusu fairness na amekuwa na wabunge wa upinzani before Chama kimoja. Mwinyi naye. Mkapa naye na Kikwete naye. Ila hii ya wabunge wote kutoka bara kuwa CCM... Duuuuh!. kweli tunatofautiana fikra
Nataka kujidhulu mwenyewe sitaki kuongozwa na wezi majambazi bora tu nitoweke kuliko kuendelea kuzulumiwa na chama flani soon Nita jikataa
 
Hata CCM wakiwa 100% wapinzani ndani yake wenye uzalendo na sio kusema kila kitu ndio watapatikana na 2025 hakutakua na zile sababu za wapinzani wamekwamisha
 
CHADEMA imekufa rasmi..
Mipango ya Mungu hatuijui
 
Wameponzwa na kauli ya kuunga mkono juhudi..wananchi wameona hakuna mpinzani wa kweli Bora wachague ccm tu,.Mana wakipewa upinzani wanarudi Tena ccm
 
Suala si ilani bali suala ni utekelezaji wa Ilani. Yapo yaliyokuwamo kwenye ilani iliyopita ya 2015 lakini hayakutekelezwa mpaka sasa!

Aidha, mbali na tatizo la utekelezaji wa ilani ya Chama, pia tatizo lilopo ni huyo mliyempa ridhaa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama. Tangu alipopewa ridhaa 2015-2020 yapo mazuri na mabaya kama binadamu. Lakini mabaya yake yamezidi kipimo na ni mengi na unayafahamu sina haja ya kuyaorodhesha kwa sababu balil insaan alaa nafsihi baswiira! Binadamu anajifahamu hakika nafsini mwake yupoje!

Tukija kwenye uchaguzi wa sasa umechafuka kwa ushahidi wa wazi na hauna kificho!

Binafsi ni mtu wa "ilmul haal" nimechanganya elimu ya kisekyula na elimu ya dini. Nimefundishwa kuishi na watu kwa wema, kuipenda jamii na kuipenda nchi. Nimefundishwa kumuokoa anayedhuluma na anayedhulumiwa!

Siwezi kukitetea chama kwa sababu chama hakitonisaidia chochote mbele ya Mungu! Siwezi kumtetea mtu kwa mapenzi yangu binafsi hata kama anafanya uonevu kwa kuwa ni miongoni mwa watu wangu!

Uchaguzi huu imefanyika dhulma ya wazi na uhujumu kwa kuchaguliwa viongozi ambao hawakuwa mahususi kwa wapiga kura. Pia umejeruhi wengi na kuwaua baadhi ya raia, na sikuona makosa yao isipokuwa walikuwa ni wenye kulinda kile walichokipigia kura na hakikuwa na athari hasi yoyote kiutendaji hata kama walikiuka utaratibu.

Dini yangu inaniambia; ikiwa nitafanya dhulma tu hata kama si kwa vitendo hata iwe kwa kusapoti tu basi nami nimechangia hiyo dhulma! Kama waliyopiga kura 50,000 wakadhulumiwa haki yao nikihusika basi natakiwa niwalipe hao wote haki yao. Sasa nikiangalia majeruhi na waliyouliwa sina mema ya kuwalipa wote! Dhulma kwangu ni dhambi kubwa na kuua unapata laana kwa Mungu.

Licha ya hivyo tunaishi kwenye sayari tofauti na tuna dini tofuati. Kwa hayo kwa roho njema tena kwa moyo mkunjufu nimeazimia kutokuchangamana na wewe kwenye mijadala na kukukoti pia kuanzia sasa na hii ni koti ya mwisho kutoka kwangu kuja kwako rasmi!

Mungu atubariki.
Amina.
===
Pole sana, Mkuu. Ninashukuru sana kwa kuwa muwazi na kutoa maelezo yako kinagaubaga bila unafiki. Mkuu umekuwa mkweli na hili jambo ndiyo huwa nalipigania kadiri ninavyo weza yaani watu tusiwe wanafiki. Binafsi nimefaidika sana na ushiriki wako kwa pamoja hapa jukwaani.

Ninasikitika kama binadamu yeyote kwa kuwa sasa umenisusia hutaki kuchangamana nami hapa jukwaani. Hili naliona ni kama changamoto kwangu ya kunifanya niwe na bidii ya kijifunza mengi namna ya kushirikiana na wanajamii. Ukweli Mkuu, umenipa afya ya ubongo.

Nina imani umefanya hivi kwa wema ili shweitwan asije akavuruga uwepo wetu hapa duniani kwa kipindi hiki. Kwa hili Nakushukuru sana. Mkuu, Mwenyezi Mungu atupe heri na inshallah atatupa wakati mwingine wa kurudi meza moja. Amina.
 
Yaani nakosa amani ya nafsi kwa ajili ya kidude kimoja ?
Vilevile nataka kufanya jambo moja ila nafsi inasita. Kipato changu ni cha kawaida ila kuna watu wa CCM huwa wanakuja kunililia shida zao kuhitaji fedha. Nataka kuwapiga pin wakija kuanzia sasa ila nafsi inaniambia nisifanye hivyo.
 
Magufuli anakwenda kuwa Rais, Rais hadi kifo kimtenganishe na Urais.
Na Mungu alivyokuwa mwema kwa dhulma hii,hii mitano anaweza asiimalize!

Simuombei mabaya ila kujifanya uu mkubwa kuliko wote kwa 100% ni chukizo sana fikiria kwanza ni wangapi wanatirirka damu za uchungu mioyoni mwao?
 
Back
Top Bottom