Nchi imeanza kurudi nyuma kwa kasi ya ajabu, bila rushwa TANESCO hawafungi umeme

Nchi imeanza kurudi nyuma kwa kasi ya ajabu, bila rushwa TANESCO hawafungi umeme

Ndokeji

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
698
Reaction score
476
Nimekuwa nikiripoti Mara nyingi jinsi nchi yetu inavyokwenda kwa sasa tumeanza kurudi nyuma , Huduma zimekuwa mbovu ukiende kwenye ofisi kupata huduma customer care mbaya wahudumu wanakujibu ovyo.

Mfano Mzuri ni shirika letu la Tanesco Maeneo Mengi watu wanalalamika, likiwemo eneo letu, Tumekuwa tukifatilia kufungiwa umeme pale nyakato Tanesco Maeneo yetu ya kisesa lakini cha kushangaza sasa miezi mitatu bila kuona hata surveyor, Juzi kuna jamaa mmoja kafungiwa umeme Mtaa Mzima.

Kufatilia kwa karibu ilibidi jamaa atoe hela kampa surveyor umeme ukafungwa na kuwaka, Form zimewekwa kabatini ukitoa mtonyo umeme unawaka fasta, Kwa hali hii nimeamua kuwa mpolekwa kuwa nchi imerudi kule tulipokuwa basi hakuna namna nasubili na Mimi nijichange nimpe surveyor umeme uwake, nimefatilia umeme mpaka kazi zangu haziendi kila siku nipo nyakato Majibu gari zipo mbili na surveyor wawili.

Waziri kimya
Wananchi wanalia
 
Nani alikudanganya kuwa katika Awamu ya Tano ya Hayati Rais Dkt. Magufuli hiyo Rushwa ilikuwa imeshaenda Kaburini kwa Tanzania na Watanzania?
 
Nchi inatakiwa kuongozwa na mifumo imara isio tegemea utashi wa mtu mmoja. Mazuri aliyo yafanya mwenda zake tanaweza kua historia kwa kua hayakuingizwa kwenye mifumo inayo ongoza nchi
Hili nimeliona bila mfumo imara hii nchi tutakuwa tunaenda mbele na kurudi nyuma
 
Ukiacha Polisi , TANESCO ndio sehemu rushwa ilipo haswa Yani ni nyumbani, katika top 3 za rushwa tanesco wapo na wametapakaa kila Kona nchini, Mimi juzi nimetoka rushwa ya 150,000 Ili nifungiwe umeme niliolipa 27,000/=
 
Ukiacha Polisi , TANESCO ndio sehemu rushwa ilipo haswa Yani ni nyumbani, katika top 3 za rushwa tanesco wapo na wametapakaa kila Kona nchini, Mimi juzi nimetoka rushwa ya 150,000 Ili nifungiwe umeme niliolipa 27,000/=
Bila shaka ,Huku mpaka kuna jamaa anakaa na fomu surveyor akija nikukusanya formu na pesa na umeme unawaka, Nilishangaa mtaa wetu jamaa mmoja tu anapelekewa mita na kufungwa waya ndani nyumba nikamfuata jamaa akasema kaingia mfukoni
 
Back
Top Bottom