Nchi imeanza kurudi nyuma kwa kasi ya ajabu, bila rushwa TANESCO hawafungi umeme

Nchi imeanza kurudi nyuma kwa kasi ya ajabu, bila rushwa TANESCO hawafungi umeme

Nani alikudanganya kuwa katika Awamu ya Tano ya Hayati Rais Dkt. Magufuli hiyo Rushwa ilikuwa imeshaenda Kaburini kwa Tanzania na Watanzania?

Rushwa kwenye ofisi za umma haijawai kuisha toka enzi na enzi ,hata kipindi cha jiwe rushwa ilikuwa inatembea ,majambazi kina sabaya walikuwa wanafanya ujambazi wazi wazi....wasituchoshe na legasi hewa zao.
 
Kila siku tunawaambia bora mtafute umeme wa solar kuliko huu umeme wa tanesco. Watanyooka wenyewe.
 
Nchi inatakiwa kuongozwa na mifumo imara isio tegemea utashi wa mtu mmoja. Mazuri aliyo yafanya mwenda zake tanaweza kua historia kwa kua hayakuingizwa kwenye mifumo inayo ongoza nchi
Mifumo hiyo ni kama ipi mkuu?..

Kwani kuna mfumo unaoruhusu rushwa?
 
mimi nilivuta umeme kipindi cha JPM na nilitoa rushwa kiroho safi umeme ukawahi kufika, kwa sasa natafuta rushwa nivute na maji kabisa, nchi hii bila kuwawezesha watu hupati, fanya mahesabu uone
umeme upo kinondoni wewe unaenda huko mpiji Magohe ndani ndani ambapo hakuna umeme unajenga vyumba viwili, unanua sola then unaona haikidhi, huwezi kuhifadhi vitu kwenye friji, huwezi angalia TV kwa uhuru, huwezi kupiga pasi nguo zako, huwezi kutunza hata mtindi, huwezi sikiliza mziki, kwa sababu ya giza vibaka wanachora rada wanakuibia kila siku, hivi kujiongeza uchukue 500K watu wakuwahishie huduma unaona nongwa , kama hutaki kutoa kitu endelea kukaa hapo mkwajuni, moscow , manyanya mpaka serikali ikipeleka nguzo huko kibwegere kwako.
unahamia sehemu unanua maji dumu la lita 1000 kwa 15,000, kwa mwezi unatakiwa madumu 4 sawa na 60,000 kwa mwaka sawa na 720,000 kanakuja kajamaa ka survyor ka dawasco kanataka 200k kafanye mchakato upate maji uondokane na shida badala ya kutoa 720,000 kwenye ile bajeti yako ya maji ukape kapambane upate maji uokoe gharama zaidi wewe unakuja kumlilia Magufuli huku.

fanya cost benefit analysis wape watu chakula wakupunguzie future costs.
mkono utoao ndio upokeao, wape motisha ili nao waje wakuchangie kwenye duka lako
 
Nimekuwa nikiripoti Mara nyingi jinsi nchi yetu inavyokwenda kwa sasa tumeanza kurudi nyuma , Huduma zimekuwa mbovu ukiende kwenye ofisi kupata huduma customer care mbaya wahudumu wanakujibu ovyo.

Mfano Mzuri ni shirika letu la Tanesco Maeneo Mengi watu wanalalamika, likiwemo eneo letu, Tumekuwa tukifatilia kufungiwa umeme pale nyakato Tanesco Maeneo yetu ya kisesa lakini cha kushangaza sasa miezi mitatu bila kuona hata surveyor, Juzi kuna jamaa mmoja kafungiwa umeme Mtaa Mzima.

Kufatilia kwa karibu ilibidi jamaa atoe hela kampa surveyor umeme ukafungwa na kuwaka, Form zimewekwa kabatini ukitoa mtonyo umeme unawaka fasta, Kwa hali hii nimeamua kuwa mpolekwa kuwa nchi imerudi kule tulipokuwa basi hakuna namna nasubili na Mimi nijichange nimpe surveyor umeme uwake, nimefatilia umeme mpaka kazi zangu haziendi kila siku nipo nyakato Majibu gari zipo mbili na surveyor wawili.

Waziri kimya
Wananchi wanalia
yule waziri wa mwanga c msukuma au
 
Back
Top Bottom