Nchi imeanza kurudi nyuma kwa kasi ya ajabu, bila rushwa TANESCO hawafungi umeme

Nchi imeanza kurudi nyuma kwa kasi ya ajabu, bila rushwa TANESCO hawafungi umeme

Ndugu mteja,
Pole sana kwa usumbufu unaopata,
Tunaomba kufuatilia zaidi
Pia tutashukuru kupata taarifa zako pamoja na mawasiliano
Mfuatilie zaidi kwani kuna msichokijua? Rushwa ya kufungiwa umeme nyie, wizi wa umeme nyie hao hao ndo mnashiriki
 
Waziri Mkuu mwenyewe Kapoa, maana anaweza tumbua mtu kumbe mtu wa watu, ingekuwa JPM hufanyi kazi unatumbuliwa on the spot kalilie mbele wanajamii wapate huduma.

Ninachoweza kusema hii ni trela show kamili inakuka nchi inaenda kupoa zaidi ya kipolo cha barafu, maana JPM alitenda kwa vitendo, alifika site, wananchi walimuunga mkono hata penye kikwazo walimwambia kwa sababu muda wote anao wananchi wake! Aliwapunguzia tozo tozo za ajabu, walioneshwa nn hela zao zinafanya usiku na mchana na kweli matokeo yalionekana...ila kwa sasa hatujui hata miradi inaendeleaje vikao ni korona korona korona chanjo basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani stiglaz imefikia wapi? atakayetuletea tena umeme wa capacity charge, tutamnyonya macho aisee.....tena huyo gabachori asifikirie kurudi tena, angekuwepo mwalimu angemwambia asionekane tena east africa.....
 
kwa sababu watu wengi walisherekea kifo cha Magufuli acha tuteseke pamoja mimi natamani mambo yawe ovyo zaidi ya hapa ili siku nyingine MwenyeziMungu akitupatia zawadi tuwe na shukurani...
 
Ndugu mteja,
Pole sana kwa usumbufu unaopata,
Tunaomba kufuatilia zaidi
Pia tutashukuru kupata taarifa zako pamoja na mawasiliano
Acheni kumuhujumu Rais, hadi Tanesco pale Mbezi Raffia ni wapuuzi kabisa, mimi nimeomba umeme muda mrefu pia hadi leo kimiya
 
Nimekuwa nikiripoti Mara nyingi jinsi nchi yetu inavyokwenda kwa sasa tumeanza kurudi nyuma , Huduma zimekuwa mbovu ukiende kwenye ofisi kupata huduma customer care mbaya wahudumu wanakujibu ovyo.

Mfano Mzuri ni shirika letu la Tanesco Maeneo Mengi watu wanalalamika, likiwemo eneo letu, Tumekuwa tukifatilia kufungiwa umeme pale nyakato Tanesco Maeneo yetu ya kisesa lakini cha kushangaza sasa miezi mitatu bila kuona hata surveyor, Juzi kuna jamaa mmoja kafungiwa umeme Mtaa Mzima.

Kufatilia kwa karibu ilibidi jamaa atoe hela kampa surveyor umeme ukafungwa na kuwaka, Form zimewekwa kabatini ukitoa mtonyo umeme unawaka fasta, Kwa hali hii nimeamua kuwa mpolekwa kuwa nchi imerudi kule tulipokuwa basi hakuna namna nasubili na Mimi nijichange nimpe surveyor umeme uwake, nimefatilia umeme mpaka kazi zangu haziendi kila siku nipo nyakato Majibu gari zipo mbili na surveyor wawili.

Waziri kimya
Wananchi wanalia
Mgeni was umeme mkuu
Hakunaa surv..anakuja BURE kamwe
Kaziiiendeleeeee mkuu hizo n za vocha tu
 
Tuliwaambia subiri siku ziende mbele kidogo!
huyu dingi wa Chato mtamkumbuka huku mkilia
 
Nchi inatakiwa kuongozwa na mifumo imara isio tegemea utashi wa mtu mmoja. Mazuri aliyo yafanya mwenda zake tanaweza kua historia kwa kua hayakuingizwa kwenye mifumo inayo ongoza nchi
Hiyo mifumo itaongozwa na panya ama hawa hawa binadamu!!?
 
Wewe mchaga tulia dawa ikuingie
Vile mwendakuzimu amefurahia hii comment yako ya ukabila kutokea kuzimu😁😁😁
162869316286936.jpg
 
Nchi inatakiwa kuongozwa na mifumo imara isio tegemea utashi wa mtu mmoja. Mazuri aliyo yafanya mwenda zake tanaweza kua historia kwa kua hayakuingizwa kwenye mifumo inayo ongoza nchi
Hizi ni theory za vitabuni na kidogo nchi za ulaya.(maana hata raisi Trump alikuwa na uongozi ambao ni tofauti kabisa na raisi wa sasa)

Huku Afrika (kama sio dunia yote), asilimia kubwa ya viongozi wanaongoza kwa mbinu zao ambazo wengi ni kwa maslahi yao wenyewe.
 
Nimekuwa nikiripoti Mara nyingi jinsi nchi yetu inavyokwenda kwa sasa tumeanza kurudi nyuma , Huduma zimekuwa mbovu ukiende kwenye ofisi kupata huduma customer care mbaya wahudumu wanakujibu ovyo.

Mfano Mzuri ni shirika letu la Tanesco Maeneo Mengi watu wanalalamika, likiwemo eneo letu, Tumekuwa tukifatilia kufungiwa umeme pale nyakato Tanesco Maeneo yetu ya kisesa lakini cha kushangaza sasa miezi mitatu bila kuona hata surveyor, Juzi kuna jamaa mmoja kafungiwa umeme Mtaa Mzima.

Kufatilia kwa karibu ilibidi jamaa atoe hela kampa surveyor umeme ukafungwa na kuwaka, Form zimewekwa kabatini ukitoa mtonyo umeme unawaka fasta, Kwa hali hii nimeamua kuwa mpolekwa kuwa nchi imerudi kule tulipokuwa basi hakuna namna nasubili na Mimi nijichange nimpe surveyor umeme uwake, nimefatilia umeme mpaka kazi zangu haziendi kila siku nipo nyakato Majibu gari zipo mbili na surveyor wawili.

Waziri kimya
Wananchi wanalia
Ukweli rushwa ipo juu sn
 
Back
Top Bottom