mimi nilivuta umeme kipindi cha JPM na nilitoa rushwa kiroho safi umeme ukawahi kufika, kwa sasa natafuta rushwa nivute na maji kabisa, nchi hii bila kuwawezesha watu hupati, fanya mahesabu uone
umeme upo kinondoni wewe unaenda huko mpiji Magohe ndani ndani ambapo hakuna umeme unajenga vyumba viwili, unanua sola then unaona haikidhi, huwezi kuhifadhi vitu kwenye friji, huwezi angalia TV kwa uhuru, huwezi kupiga pasi nguo zako, huwezi kutunza hata mtindi, huwezi sikiliza mziki, kwa sababu ya giza vibaka wanachora rada wanakuibia kila siku, hivi kujiongeza uchukue 500K watu wakuwahishie huduma unaona nongwa , kama hutaki kutoa kitu endelea kukaa hapo mkwajuni, moscow , manyanya mpaka serikali ikipeleka nguzo huko kibwegere kwako.
unahamia sehemu unanua maji dumu la lita 1000 kwa 15,000, kwa mwezi unatakiwa madumu 4 sawa na 60,000 kwa mwaka sawa na 720,000 kanakuja kajamaa ka survyor ka dawasco kanataka 200k kafanye mchakato upate maji uondokane na shida badala ya kutoa 720,000 kwenye ile bajeti yako ya maji ukape kapambane upate maji uokoe gharama zaidi wewe unakuja kumlilia Magufuli huku.
fanya cost benefit analysis wape watu chakula wakupunguzie future costs.
mkono utoao ndio upokeao, wape motisha ili nao waje wakuchangie kwenye duka lako