Nchi imejaa ushabiki wa ajabu, sijui kama ipo siku tutasimama kama Taifa

Ni ushamba tu ila kuna muda utaondoka,Ata uko ulaya miaka fulani ilikua kama hivi ila kwasasa walisha sahau.
 
Huyu waziri hafai hata kuongoza mbuzi, sijui kwa nn akawa waziri wa michezo hapa bongo
Kipi cha kushangaza hapo? Ili upate cheo nchi hii lazima ulambe miguu ya watu.
Waziri ni mwanasheria by profession lakini anachoongea na profession yake haviendani.

Hilo chama limelaaniwa kila anayeingia huko akili zinamruka.
Hakuna hata mmoja aliye salama we chunguza zaidi.
 
Inaonekana wewe na ndumbaro vichwa vyenu mnavitumia kama kontena za kuhifadhia mate tu.
Aisee watu mna madongo. Akirudi kwenye uzi huu nitamuona kweli kidume.

Bado najiuliza nani alivujisha ile barua ya TFF au wamevujisha wenyewe ili kuzima soo na kuepuka kubadili amri zao
 
Kwa hiyo mpata utishie watu kukamatwa na Polisi ukionekana na jezi ya timu pinzani ndo uzalendo huo? Mmekosa utetezi mnawayawaya tu. Matamahi ya kibabe kwenye uhamasishaji yanasaidia nini?
 
Wamezoea kusukuma Watanzania kama Ng'ombe safari hii wamekutana na rungu la CAF, na bado FIFA.
 
Akili ndugu yangu. Watanzania wengi hawana akili.
 
Ni ushamba tu ila kuna muda utaondoka,Ata uko ulaya miaka fulani ilikua kama hivi ila kwasasa walisha sahau.
Huko ulaya shabiki wa Man U anashabikia Man city ikicheza na Bayern? Au ulaya gani unaongelea wewe? Huko ndo timu mwenyeji inampangia mgeni tiketi 5000 Kati ya 68000 au na Hilo hujui?
 
w
Wewe mwenyewe si chawa ndio maana hujaona makosa yake
-Mpira unachezwa wanjani au wanacheza mashabiki
-Kwanini waziri anaingilia uhuru wa watu kwani yeye ni mkoloni mweusi
-Yani mimi simba niwashabikie yanga watu waliotufunga goli tano kwa nunge
- Apeleke siasa zake bungeni kule akatetee serikali yanga haiwakilishi nchi na haitakuja kuwakilisha nchi wakifungwa wamefungwa yanga sisi tutawazomea tena naenda kununua uzi wa mamelodi
-Waziri baada ya kuhangaika kukuza vipaji umiseta kule na kutafuta wawekezaji wakuze michezo yeye anatafuta kiki kwenye timu iloanzishwa kabla hata yeye kuzaliwa aache sifa za ajabu
-Huyu waziri anaweza kuwa chanzo cha fujo tamko lake kuna vichaa wanaweza kuona ni amri watapigana watu kwa mkapa
-Hii kauli ya waziri inaweza kuathiri mapato ya uwanja unamlazimisha shabiki ashabikie timu unayoitaka wewe kaangalie mpira peke ako basi
-Mwisho yanga sio timu ya taifa muache shobo
 
Achilia mbali Huyo waziri CCM wanajulikana, Mijitu mingi Inayoshabikia SANA mitimu ya kibongo, akili haona, imejaa chuki na isiyo na hoja.

Bora hata wakiwa kwenye hii ligi ya mabingwa, lakini ligi kuuu?
 
Sema wewe ni mshabiki wa timu gani?
 
Hayati RAIS Mwinyi alihudhuria mechi ya Simba na Stella Abijan , kabla ya hapo alisisitiza sana uzaelendo lakini wakati Stella wanapata goli la pili mashabiki wa YANGA walianza kuimba na kuzunguka uwanja mzima wakisema Uzalendo umewashinda.
Yanga ama mashabiki wa Yanga wamekuwa vinara sana wa kukodisha Coasta na kwenda kupokea timu pinzani zinapocheza na Simba.
Hersi siku ya mechi ya Simba na KAIZER chief alivaa jezi ya Kaizer Chief.
Juzi Jwaneng walipokuja kucheza walifikia Avic Town mahali ambapo ni kambi ya Yanga.

Waziri anataka Uzalendo gani? Wewe mleta mada una timu unaishaibikia ambayo ni ya Uiengereza au Hispania lini waziri amekuzuia? Wenzetu Ulaya kila shabiki wa mpira ni shabiki wa timu inayotokea eneo analoishi, je wewe unashabikia timu ya mkoani kwenu?

Uzalendo ni timu ya Taifa si Yanga au Simba, kama mnataka uzalendo anzani sasa kuweka mikakati kila shabiki aingie uwanjani siku timu yake inacheza tu. Lakini utakuta kila Simba ikicheza mashabiki wa YANGA wamejaa uwanjani, kufanya nini? Kila mtu ashinde mechi zake.
 
Huyu waziri alipomfedhehesha karibu wa netball Hadi akajiuzulu alifikiri anaweza kuwapanda vichwani washabiki wa soka.
Uzalendo ni zaidi ya kusema Mimi mzalendo Bali matendo yako. Ndio yatakuonyesha wewe mzalendo
I'm
 
Hao wapuuzi si wa kuwasikiliza muda wote walikuwa wapi kuhimiza uzalendo.
Kila mtu apambane na Hali yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…