GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Kutokana na umri wao, uzoefu wao, na majukumu ya kitaifa waliyowahi kuwa nayo nchini, baadhi ya wastaafu wa kisiasa wana hadhi ya kutambulika kama wazee wa Taifa! Lakini kwa miaka ya hivi karibuni, ni wazee wawili tu: Jaji Joseph Warioba na mzee Joseph Butiku ndiyo wamekuwa wakisikika wakishauri na kukemea pale wanapoona mambo yanaenda ndivyo sivyo!
Wazee wengine wameenda wapi?
Yuko wapi J. M. Kikwete, Rais mstaafu ambaye kipindi chake demokrasia ilishamiri kuzidi vipindi vya watangulizi wake na hata vya waliomfuatia?
Yuko wapi Amani Abeid Karume, ambaye pamoja na "kukulia" ikulu, hakushikwa na ugonjwa wa uchu wa madaraka?
Yuko wapi Dr. Salim Ahmed Salim, mbobevu wa siasa za kitaifa na kimatiafa?
Yuko wapi Dr. John Samwel Malecela, mwanasiasa msomi nchini?
Yuko wapi David C. Msuya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania?
Yuko wapi Pius Msekwa, msomi aliyehudumu kwenye chama na Serikali kwa miaka mingi?
Yuko wapi Dr. Mohammed Gharib Bilal, Mwanafizikia makini aliyewahi kuwa makamu wa Rais wa JMT?
Yuko wapi Fredrick T. Sumaye, Mtanzania wa kwanza kushika nafasi ya Uwaziri Mkuu kwa awamu mbili mfululizo?
Yuko wapi Mizengo Kayanza Peter Pinda, Waziri Mkuu asiyekuwa na makando kando ya rushwa?
Wako wapi wazee wengine?
Wameamua kuwaachia jukumu la kushauri na kuonya mzee Butiku na Warioba, pamoja na baadhi ya viongozi wa dini kama Dr. Shoo, Dr. Benson Bagonza, Shehe Ponda, na Dr. Charles Kitima?
Wanaridhishwa na yanayoendelea nchini?
Pongezi kwa mzee Butiku na Jaji Warioba kwa kutambua nafasi zao na kuzitumia kiufasaha kwa maslahi ya Taifa. Wameonesha kwa vitendo kuwa utaifa ni wa muhimu zaidi kuliko vyama vyao vya kisiasa!