Nchi ina wazee wawili tu kwa sasa?

Viongozi wote kutoka Kanda ya Ziwa wanajitambua!!

Huku pwani ni taarabu na uchawa!!
 
Uislam na uongozi ni vitu viwili tofauti
Unakosea mkuu!
1. Kikwete ni Muislamu! Ingawa aliboronga katika maeneo mengine, lakini kwenye demokrasia mpaka sasa hakuna Rais aliyemfikia

2. Magufuli alikuwa Mkristo! Ingawa alifanikiwa katika mambo mengine, lakini kwenye demokrasia, huenda akawa ndiye Rais aliyefanya vibaya kuliko watangulizi wake wote

Dini haiamui ubora au udhaifu wa kiongozi, bali kiwango cha "kuelimika" kwake!
 
Kiongozi mzuri ni aliyestaafu! Huyo ndiye anayeweza kushauri vyema huku akitumia kama rejea makosa yake na ya wengine pamoja na mafanikio yake na ya wengine!
 
Sahihi
 
Wazee wengine wameenda wapi?

Vijana tuache kutegemea wazee watutetee, huu ni wakati wetu siyo muda wa kutafuta atakaye tukomboa.

Nchi nyingi vimekombolewa kutoka kwa wakoloni au utawala gandamizi kwa vijana kuchukua hatima yao mikononi mwao kwa wakati wao wakiwa vijana.

Hawakusubiri wazee wawatetee, wazee walitumika tu kuwatia moyo vijana, lakini jukumu la mabadiliko vya vitendo ni letu kizazi hiki cha wengi kinachopitia madhila ya kugandamizwa, kupuuzwa na kuonewa .

KUTOKA MAKTABA:

VIJANA NA MABADILIKO, WAKATI HUU 2024 / 2025 NI SAHIHI KUINGIA KTK NAFASI ZA MAAMUZI IKIWEMO URAIS


Duniani ni vijana wa vyuo vikuu ndiyo wanaoongoza kuchagiza mageuzi, Vijana ni taifa la leo, watoto ndiyo viongozi wa kesho. Kauli za kilaghai kuwa vijana ni kwa ajili ya taifa la kesho siyo sahihi.

Vijana msihofu msuguano na wazee waliopo mamlakani, kusubiri kupewa ni kukubali kuwa tumejumuishwa na watoto chipukizi. Ni wakati wa vijana kuchagiza kwa mbinyo wa hoja kuwa uongozi wa nchi ni kwa ajili ya vijana.

Historia inaonesha mara baada ya uhuru wa kwanza kupatikana ktk mtaifa mbalimbalii iwe kwa mtutu wa bunduki au maandamano ya kuondoa wakoloni, baadaye kulifuatia msuguano wa wananchi wenyewe kwa wenyewe kwa kutoridhishwa na wale waliochukua utawala toka kwa wakoloni.

Sababu mbalimbali zilizua msuguano ktk nchi huru kama udiktekta, tawala kamdamizi ya chama kimoja kongwe, utawala mbovu, ubaguzi wa kielimu mfano mtoto aliyesoma shule za kata / st. Kayumba anadanganywa kuwa akihitimu chuo kikuu atakuwa na nafasi sawa na mwenzake aliyesoma St. Mary's akamaliza elimu ya chuo kikuu pia anayekimanya kiingereza vizuri zaidi na wajomba wake wapo ktk nafasi za kiutawala n.k

Hapo ndipo Wanafunzi waliopo ktk nchi kama Sudan, Chile, Cuba, Afrika ya Kusini, Kenya walishiriki kudai mageuzi ili kuondokana na tawala zilizomgoa mkoloni.

Tanzania vijana hawajishughulishi kuhoji mambo yasiyowaridhisha wananchi kama bandari kuchukuliwa kuwa vituo vya nchi ngeni, matumizi mabaya ya kodi za wananchi, tozo zilizokifu wananchi, demokrasia kubinywa, katiba kandamizi n.k

Huko Chile marekani ya kusini nchi iliyo viongozi wa vyama vya wanafunzi wenye kushiriki kikamilifu katika siasa pia maandamano imewezesha kiongozi kijana wa wanafunzi Gabriel Boric ambaye ndiye rais kijana kabisa wa kuchaguliwa amezaliwa 11 February 1986 ambaye alichukua madaraka ya urais tarehe 11 March 2022 baada ya kushinda uchaguzi mkuu nchini Chile tarehe 19 December 2021 kwa kupata asilimia 60% ktk uchaguzi wa urais.

Gabriel Boric on the Chilean student movement 14 June 2017
Mwanafunzi wa chuo kikuu Tanzania toka familia masikini anazama ktk mkondo wa madeni ya fedha za mkopo wa elimu ya juu huku akiwa anaimani na matumaini potofu ya Ilani ya CCM imeandika ahadi ya mambo ya uongo ya kupata ajira, mazingira ruhani kuwa wataweza kupata vyeo vya ulaji vya kisiasa UVCCM, kuwa MNEC Halmashauri Kuu ya CCM, mbunge wa CCM n.k au kuwepo mazingira (hewa) ya kujiajiri.

VIJANA NI WAKATI WA KUACHA KUTEGEMEA CHAMA DOLA KONGWE

Picha maktaba : Vijana chawa wa Vyuo vya elimu ya juu Tanzania.

Vijana vyuo vikuu na mijini pia vijijini badala ya kumezwa na ukiritimba wa UVCCM na ahadi kuwa ni viongozi wa kesho huku watoto wa vigogo wa CCM wanapewa nafasi sasa na siyo kesho wanatakiwa kuunda chombo chao kipya cha kutambulika kama mdau muhimu anayehitaji kuonekana katika majukwaa ya siasa pia ktk vituo vya redio, televisheni na mitandao ya kijamii kuchagiza mabadiliko na mageuzi ikiwemo pia kupewa nafasi nje ya mfumo wa vyama ili wagombee nafasi za kuchaguliwa na wananchi.

VIJANA KULE CHILE BARA LA LATINO AMERIKA WAMEWEZA

Gabriel Boric - The 100 Most Influential People of 2022 - TIME

time.com › collection › gabriel-boric


23 May 2022 · He is making Chile the social, economic, and political laboratory of the world once again. Stiglitz is a Nobel Prize–winning economist
 
Mcheki kiongozi wa mapinduzi ya Cuba kamandate Fidel Castro hapa clip ikionesha kijana kiongozi wa nchi ya Cuba mwaka 1959 akiwa na umri wa miaka 33 akihojiwa kuhusu visheni ya uongozi mpya mwaka 1959

The young Prime Minister of Cuba comrade Fidel Castro rare interview conducted in English
On April 19, 1959, Fidel Castro appeared on “Meet the Press” for his first visit to the United States since the Cuban revolution, nearly three months earlier. When asked if he was a Communist, he said, “I am not a Communist.
 
Nakukumbusha hao wote wanakula kwa urefu wa kamba Acha kuwasumbua
 
Ammada siyo shida zake yuko anakula vyombo Salim ni mgonjwa
 
Mbona umemsahau Wasira, mzee wetu yupo toka enzi za Mwalimu😏
Nimewazingatia zaidi wastaafu walioshika nafasi kubwa kitaifa, hasa Urais, Umakamu wa Rais, Uwaziri Mkuu, Uspika, Ujaji Mkuu, n.k.
 
Hajafanya nini pumbavu??Mtu amewahi kuwa Makamu wa Rais kipindi cha Mwinyi na ndiyo wakati demokrasia ilipozaliwa Tanzania.Amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania,je wewe umewahi kuwa nani Tanzania zaidi ya kuwa chawa wa Mama Samiah?
 
Hajafanya nini pumbavu??Mtu amewahi kuwa Makamu wa Rais kipindi cha Mwinyi na ndiyo wakati demokrasia ilipozaliwa Tanzania.Amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania,je wewe umewahi kuwa nani Tanzania zaidi ya kuwa chawa wa Mama Samiah?
Gentleman,
kwani alisahau kufanya nini akiwa kwenye hizo nafasi serikalini, hata aanze kuwa na mawenge na mbwelambwela mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kama sio wivu uzeeni?

Najivunia kua mtumishi makini wa wananchi, mchapakazi, mtiifu na mnyenyekevu kwa chama, serikali na kwa waTanzania wote.

Na wala siringi, sijivuni wala kujivunga kusema ukweli kwamba Mzee huyo ni useless na anayozungumza ni nonsense 🐒
 
Hivi hakuna wakubwa kwenu?

Ulilelewa na watu wazima au ulijilea mwenyewe?

Wewe ni mtu wa kumtukana mzee Warioba?

Kama huoni mchango wake katika taifa hili, basi mheshimu kwa sababu ya umri wake!

Epuka laana ya kutukana wazee wastaarabu kama Warioba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…