Nchi inaharibika kwa Kasi sana. Umeshawahi kumuona wapi mtoto wa kigogo anafikiria kusoma VETA?

Until that day tutakapoacha ku-equate maendeleo na Mavyeti na sijui umesoma nini tutaendelea sana kusubiri huku tunapamba ma-certificate ukutani....


If you ask me piga chini mfumo mzima wa Elimu ambayo imekuwa kama Desi ; Kama dunia we are so educated lakini maendeleo hayaendani na hio education zaidi ya madeni...

 
Darasa la saba kama wewe unapaswa kuwa na lowa thinking capacity huna analystical capacity ndo mana huwezi kukuta bank manager au C.E.O ni darasa la saba bank itafirisika ndani ya wiki
 
Darasa la saba kama wewe unapaswa kuwa na lowa thinking capacity huna analystical capacity ndo mana huwezi kukuta bank manager au C.E.O ni darasa la saba bank itafirisika ndani ya wiki

Darasa la 7 afu nina hela kuliko ukoo wenu wote combined 🤣
 
Darasa la 7 afu nina hela kuliko ukoo wenu wote combined 🤣
Pesa bila heshima is nothing. Prof anaheshimika sana kuliko Bakresa na anaweza kumwambia chochote bakhresa akatekeleza lakini kinyume chake haiwezekani
 

Mtu zwazwa kama Mkungunero hana comprehension skills kuelewa hilo.
 
Pesa bila heshima is nothing. Prof anaheshimika sana kuliko Bakresa na anaweza kumwambia chochote bakhresa akatekeleza lakini kinyume chake haiwezekani

Man, you can't be this dumb. Bakhressa la 7 ila kaajiri hao maprofessor na serikali inaloa Bakhressa akipumua tu. You're dumb as a brick 🤣🤣 I rest my case
 
Veta ingekuwa Kuna maarifa yanaparikana sawa ila elimu ya veta haiendani na wakatiufundi magari sasa hivi umejikita kwenye programing Kuna software zina detect tatizo wanazo Wachina,fundi wa vibatari siku hizi cm tu zina touch mafundi ujenzi bora hata saidia fundi anakuwa fundi umeme wa majumbani ungefundishwa primary school kila mtu anaetaka cherehani Haina Dili Tena Kuna mashine kibao zinaunda Nguo kila idara Wachina wamekuja na nyenzo rahisi kiasi kwamba vyuo havtoi elimu shindani.
 
umeongea kitu cha maana sana. Inabidi veta wabadilike kuendana na technolojia iliopo.
 
Dunia nzima kuna kozi za kujifunza na zinalipa haswa
Bahati mbaya bongo mtu ana maliza kozi yake hana hata hela ya kununulia vifaa
Anakuja kwako anakuuliza bro una nyundo ya karibu hapo

Wenzetu magharibi wana skills na wakianza kazi watasaidiwa labda na wazazi au serikali na wanakuwa na nembo kwenye magari kuwa wanatambulika
Tofauti pia ni bei wao kumuita tu anaanza kukuchaji hela
Sisi ukikaa vibaya anapitia na kuku 😄
 
Watu wanaenda veta ili wasiwe dependent mfumo wa elimu unatutengeneza tutegemee zaidi kuajiriwa ila VETA wanakutengeneza uweze kujiajiri , kwahiyo mtu unaona umemaliza miaka 5 mtaani huna ajira kwanini usijiendeleze upate ujuzi mwingine ambao ni marketable?

Kwenye maisha usimuangalie mtoto wa tajiri mbona hafanyi hivi yule kashapata neema ya kutokea familia inayo jiweza, we mtoto wa maskini inabidi ujiongeze ukitaka kushindana na mtoto wa kigogo huna unaemkomoa utaumia mwenyewe.
 
mjadala siyo sahihi huu, ni kama unajaribu kuchanganya pesa na ujuzi kwa wakati mmoja
 
Kiongozi, ili Nchi iweze kuendelea LAZIMA watu wa Elimu ya kati wawe wengi sana kwani Elimu ya kati (Diploma, Veta nk ndiko ujuzi unakofundishwa
Ukishaona Nchi imeja vyuo vikuu, huku vyuo vya kati vikiwa vichache; ujue inaenda kuangukia pua.
Wawekezaji wanahitaji watu wengi wenye Elimu ya kati/Ujuzi na sio madegree
Elimu ya kati ndio Engine ya Uchumi
Fikiria leo hii Muekezaji aseme anataka kuleta kiwanda cha Toyota hapa TZ
  • Atahitaji wapiga rangi wenye ujuzi pengine 100
  • Wenye Elimu ya mechanics pengine 1000
  • Wenye ujuzi wa hydraulic nk pengine 200
  • Wenye ujuzi wa umeme wa magari pengine 200
  • General walkers (wenye ujuzi mdogo mdogo kama kujaza upepo, kufunga nut, nk pengine 300
Hao wa madegree nk atakuja nao kutoka kwao kwa ajili ya kusimamia; Pengine kwa hapa ataweza kuajiri kama 30 tu kati ya waajiriwa pengine 1500.
 
Upo sahihi...yupo dogo alimaliza degree ya history hapo Udsm akakosa cha kufanya...dogo akajiongeza akaenda VETA akasoma refrigeration systems na AC repairs, sasa ni fundi ma AC...maisha yanasonga!
 
Wanaendekeza makaratasi vijana...huku mtaani it's all about your skills to survive...
 
Upo sahihi dada angu, lakini kwa bongo makaratasi yanalipa zaidi kuliko ujuzi, bunge la Tanzania limejaa ma-professor, PhD, Masters na degree kwa mbali lakini ufanisi wake bora hata baraza la kata.
Upo sahihi lakini ndiyo inabidi tutoke huko...si unaona wasomi wa makaratasi kibao lakini ufanisi zero?
Ili tutoke inabidi kubadilisha namna ya kufikiri, changes begins with yourself...!
 
Acha ujinga..unashauri watu wasisome?
Namshanga pia haujui kuwa Kuna watu Wana master Lkn wamerudi veta kuchukuwa ujuzi wowote

Mm Nina CPA t na Bado Bado Niko veta dodoma nachukuwa ufundi uwashi nataka niendeleze kampun ya mzee ya ujenzi Sasa Kuna shida gani Happ

Hapo Happ Pia nimemleta dogo asome ufundi simu nae kamaliza IT

Veta iko vzr jmn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…