Kiongozi, ili Nchi iweze kuendelea LAZIMA watu wa Elimu ya kati wawe wengi sana kwani Elimu ya kati (Diploma, Veta nk ndiko ujuzi unakofundishwa
Ukishaona Nchi imeja vyuo vikuu, huku vyuo vya kati vikiwa vichache; ujue inaenda kuangukia pua.
Wawezekezaji wanahitaji watu wengi wenye Elimu ya kati/Ujuzi na sio madegree
Elimu ya kati ndio Engine ya Uchumi
Fikiria leo hii Muekezaji aseme anataka kuleta kiwanda cha Toyota hapa TZ
- Atahitaji wapiga rangi wenye ujuzi pengine 100
- Wenye Elimu ya mechanics pengine 1000
- Wenye ujuzi wa hydraulic nk pengine 200
- Wenye ujuzi wa umeme wa magari pengine 200
- General walkers (wenye ujuzi mdogo mdogo kama kujaza upepo, kufunga nut, nk pengine 200
Hao wa madegree nk atakuja nao kutoka kwao kwa ajili ya kusimamia; Pengine kwa hapa ataweza kuajiri kama 30 tu kati ya waajiriwa pengine 1500.