Nchi inahitaji mawakili wengi kama Kibatala

Nchi inahitaji mawakili wengi kama Kibatala

Matongee

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2023
Posts
1,056
Reaction score
2,729
Wakuu neno ukiukwaji wa haki unaweza kulichukulia kirahisi kama haijakutokea wewe. Ila ni kitu kinachoweza kukuvuruga mno kikitokea.

Hayati Lowassa ni miongoni wanajua ladha ya hilo neno kwa vitendo baada ya tukio la kukatwa jina lake mwaka 2015.

Ingawa sidhani kabla ya hapo kama alikuwa anajua ladha halisi ya ukiukwaji wa haki. Pia kuna wale wagombea waliokuwa wanaambiwa wamekosea kujaza fomu za tume huku wale wa chama tawala wote wakiwa wameweza kujaza vizuri. Wale wagombea wanajua ladha halisi ya haki ikikiukwa.

Katika kudai haki ndo tunapokutana na mawakili kwa msaada wa kisheria. Kuna mawakili wengi nchini ila wengi ni waoga wasiojiamini.

Mfuasi wa Mbowe aitwaye Joseph Mbilinyi (Sugu) alielezea kisa cha wakili aliyeogopa kumtetea alipikuwa akipigania haki yake.

Bahati nzuri kwa sasa nchi ina wakili Kibatala aliye mstari wa mbele sana kwenye kuhakikisha anafanya kazi yake kwa weledi bila uoga.

Mimi naona Kibatala anafanya vizuri. Nchi inahitaji kina Kibatala wengi zaidi ili kupunguza madhila ya watu kupoteza haki zao.
 
Very true mkuu na halina ubishi PLUS wakili Mwambukusi
Mwambukusi = Mwabukusi. Huyo Mwabukusi ni mwanasiasa... hapa naongelea watu waliosimama na taaluma zao bila kuegemea sana kwenye siasa. Hakuna mwanaCCM anaweza kumpa kazi Mwabukusi ila kuna wanaCCM kadhaa hadi muda huu wamempa kazi Kibatala
 
Wakuu neno ukiukwaji wa haki unaweza kulichukulia kirahisi kama haijakutokea wewe. Ila ni kitu kinachoweza kukuvuruga mno kikitokea. Hayati Lowassa ni miongoni wanajua ladha ya hilo neno kwa vitendo baada ya tukio la kukatwa jina lake mwaka 2015. Ingawa sidhani kabla ya hapo kama alikuwa anajua ladha halisi ya ukiukwaji wa haki. Pia kuna wale wagombea waliokuwa wanaambiwa wamekosea kujaza fomu za tume huku wale wa chama tawala wote wakiwa wameweza kujaza vizuri. Wale wagombea wanajua ladha halisi ya haki ikikiukwa.

Katika kudai haki ndo tunapokutana na mawakili kwa msaada wa kisheria. Kuna mawakili wengi nchini ila wengi ni waoga wasiojiamini. Mfuasi wa Mbowe aitwaye Joseph Mbilinyi (Sugu) alielezea kisa cha wakili aliyeogopa kumtetea alipikuwa akipigania haki yake. Bahati nzuri kwa sasa nchi ina wakili Kibatala aliye mstari wa mbele sana kwenye kuhakikisha anafanya kazi yake kwa weledi bila uoga. Mimi naona Kibatala anafanya vizuri. Nchi inahitaji kina Kibatala wengi zaidi ili kupunguza madhila ya watu kupoteza haki zao.
Inahitaji mawakili wenye udhubutu wa kuhoji
 
Back
Top Bottom