Nchi inapochafuka Amani inatakiwa kutangulia ndipo ifuate HAKI

Nchi inapochafuka Amani inatakiwa kutangulia ndipo ifuate HAKI

Jamaa yng kama kuna mtu anakulipa ili uje uandke humu mambo haya aisee amekutoa kwny reli kbs. Rudi kwny ubora wako wa mada za kmaisha uko vzr sn uku umebagazwa rudi kwny mambo yako. Mo29 mo29 mo29..ila ila ila
Ana ubora UPI huyu tofauti na maandiko yake ya ngono? Acheni kumpa sifa azisizo stahili
 
Sio nyie mlikua mnasema TZ ni "kisiwa cha amani"? Hiyo amani ilipotea lini? Amani ipo miaka yote ila hakuna haki.
 
Careful,angalia wasianze na wewe
nasisitiza kujiepusha na magenge ya kigaidi na mamaluki wa vibaraka wa mabwenyenye ya magraribi,

ukipuuza,
basi jitie kiherehere kama hujapeleka zawadi ya huzuni kwa wazaizai wako :BillyApprove:
 
NCHI INAPOCHAFUKA AMANI INATAKIWA KUTANGULIA NDIPO IFUATE HAKI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Nimeulizwa swali; Mtibeli sijasikia ukitoa maoni yako kuhusu kati ya Haki na Amani kipi kinatangulia.

2. Mtibeli najibu; Kati ya Haki na Amani kuhusu kipi cha Kwanza au kinachotangulia. INATEGEMEA na Hali, wakati au mazingira.

3. Haki ndio msingi wa Amani. Hilo lipo wazi.

4. Lakini Katika Mazingira ya VITA, Vurugu, Maangamizi Haki itakaa nyuma kidogo kisha Amani itatakiwa kutangulia.

5. Hata hivyo lazima ieleweke kwamba Mpaka vita au Vurugu inatokea yaani uvunjifu wa Amani lazima HAKI iliondolewa. Kwamba ni ngumi Sana vita au vurugu kutokea eneo lenye HAKI.

6. Vurugu na machafuko ya Oct 29 ni kutokana na haki Fulani za watu kukandamizwa. Mfano Haki ya kuishi kwa baadhi ya watu ambao mpaka Leo haijulikani walipo. Haki za kisiasa ambapo vyama vya upinzani havipewi haki na usawa katika uwanja wa siasa kwenye uchaguzi. Mambo hayo na mengine yakawa sehemu ya sababu ya machafuko na vurugu.

7. Amani kwa watawala mara nyingi haihusishi HAKI. Hasa watawala dhalimu. Amani kwao humaanisha Utulivu hata kama kuna dhulma na uonevu, ukandamizaji na unyanyasaji.

8. Watu wote wenye tabia za dhulma, udhalimu, ukandamizaji, unyanyasaji na uonevu, hata kama sio watawala wao hawajali kuhusu HAKI(Za wengine) ilimradi wao mambo Yao yanaenda na kuna utulivu wao wanaona kuna Amani.

9. Wenye Haki, watu Wema, wenye Upendo. Kwao AMANI sio tuu utulivu Bali Amani ni mazingira ya Haki, upendo, kutetea wanaoonewa na kudhulumiwa hata kama wao hawafanyiwi matendo hayo.

10. Wenye Haki hawajali kuhusu uwepo wa vita kama lengo ni kukomesha dhulma, uonevu, ukandamizaji, ushenzi, ili Amani ya kweli ya kudumu ipatikane.

11. Mtu mwema haihitaji utulivu au Amani ya kishetani ambayo lengo lake ni uonevu, dhulma, na ukandamizaji. Na kamwe hawezi na huwezi ukamsikia akisema Jambo kama hilo.

12. Sisi kama Watibeli, tunajua Haki ndio msingi wa Maisha ya kiungwana na utu wa binadamu. Tunajua Haki ndio Amani na sio vinginevyo.

13. Katika mazingira ya Vita au machafuko nguvu kubwa itatumika kuleta utulivu ili kuhakikisha HAKI Inatendeka ili Amani ya Kweli na yakudumu ipatikane.

14. Kutuliza nchi bila kutenda Haki ni kuendeleza dhulma, ukandamizaji, udhalimu na uonevu. Ni kufukia hasira na mapigano kwa muda tuu.

15. Amani itatangulia kwa lengo la kumfanya Haki ambaye ni kama Mama kuku aweze kuatamia mayai ya Amani ili yaanguliwe.

16. Mayai ya haki na Amani yakianguliwa ndio tunaapata maendeleo endelevu na yakudumu.

17. Kama hakuna Haki hesabu hakuna maendeleo na kama yapo maendeleo unayoyaona basi sio endelevu na kamwe hayawezi kudumu kwani maendeleo yoyote ambayo ni matokeo ya dhulma na uonevu lazima yaharibiwe na yaangamizwe. Ndivyo HAKI ilivyo.

18. Sasa ili tusipoteze nguvu zetu. Ni lazima tuweke mambo sawa tungali tunanafasi. Tusije fikiri kwamba kutumia nguvu kutuliza nchi ndio kuiendeleza nchi.

19. Juzi October 29 mliona. Ilibaki kidogo nchi yote iunguzwe. Na ingeunguzwa. Ingechomwa. Ingeangamizwa.

20. Tusije jidanganya kwa vile hali Ile imedhibitiwa basi itakuwa hivyo Siku zote. Hapana! Ndugu zangu hapana. Haitakuwa hivyo Siku zote.

21. Kama tusipotenda HAKI ninakuhakikishia yote tunayoyafanya tunapoteza muda.

22. Huwezi ukaendelea kwa kudhulumu watoto, ndugu, na watu wako. Hayo hayawezi kuwa maendeleo. Kamwe!

23. Kwenye Dini kuna kitu kinaitwa Huwezi mkopesha ndugu yako kwa Riba. Hiyo no haramu
Wala huwezi muuza ndugu yako kama Mtumwa. Hiyo ni Haramu.

24. Wazungu na watu wenye akili wanajua na washanyukana na kupitia uzoefu wa kudhulumiana wao kwa wao. Soma historia ya uingereza, ufaransa, ujerumani n.k.

25. Ndio maana Kila mara nawaambia, Sera ya uvamizi haiepukiki. Kwani tusipovamia wengine tutajijuta tunavamiana na kudhulumiana Sisi kwa Sisi.

26. Na mwishowe tutaliangamiza taifa hili Sisi wenyewe.

27. Njia pekee ya kujilinda sio kupaki Bus. Ni kuvamia wengine.

28. Sisi watibeli tunajua kuwafanyia wengine ubaya ambao sio watu wako, familia yako, Jamii yako, taifa lako sio KOSA. Kwani lengo ni kujihami.

29. Lakini kuwafanyia watu wako ubaya ni kosa kwani unaathiri future yako na jamii yako.

30. Ndio maana Wazungu wao KAZI yao ni kukabiliana na jamii zingine na wao hawafikiri mara mbilimbili, hawasiti na hawajali.
Lengo lao ni kulinda mataifa yao.

31. Ulinzi sio tuu kujilinda Bali kushambulia na kufifisha nguvu za wanaokuzunguka ili uweze kujiimarisha.

32. Kushambulia watu wako ni kujishambulia mwenyewe. Kujiangusha.
Huwezi ukalinda taifa lako kwa kushambulia watu wako.

33. Kushambulia watu wako ni mbinu ya adui ili kuangamiza taifa lako.

34. Hata kwenye familia. Huwezi kulinda na kujenga familia yako kwa kumshambulia mke/mume au watoto wako.

Acha nipumzike sasa.

TaikonMaster
Kwa sasa Morogoro Mjini.
Hii ngonjera kamsomee Muuaji Samia na wenzake.

Uwajibikaji kwanza, akae pembeni ndipo amani hufuatia baada ya HAKI kutangulia
 
Back
Top Bottom