Nchi inaweza kuendelea kwa viongozi kuzunguka Duniani kuomba fedha?

Nchi inaweza kuendelea kwa viongozi kuzunguka Duniani kuomba fedha?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Mjadala mkubwa ulipo mtaani sasa hivi ni kuhusu viongozi wetu kutamka kwenye majukwaa kwamba wanazunguka Duniani kutafuta pesa kwaajili yetu; wengi wanajiuliza hizo pesa tunazopewa huko nje zinatokana na nini? Kwamba wenzetu wafanyakazi kwa bidii kwa ajili ya kutupa fedha sisi? Je tunapopewa hizo fedha wao wanafaidika vipi?

Kwanini tumeamua kuishi kwa kuomba na siyo kwa kuboresha viwanda na nyenzo nyingine za uzalishaji?

Kwa miaka 60 ni kipi ambacho tunaweza tunajivunia kwa sababu ya kuomba fedha nje?
 
Ni Ujinga wa hali ya juu kuamini katika MISAADA.

Magufuli alitaka kututoa huko kabisa lkn elimu duni ya Watanzania ikatatiza hili...
 
Mjadala mkubwa ulipo mtaani sasa hivi ni kuhusu viongozi wetu kutamka kwenye majukwaa kwamba wanazunguka Duniani kutafuta pesa kwaajili yetu...
Si Kwa kubadilishana na Ardhi yetu, na rasilimali zingine
 
Yaani kodi inayokusanywa kwa mvuja jasho wa Ulaya au/na Marekani lije ligaiwe kizembe huku kwetu?

Wakati kwao ukikwepa kodi unaenda jela...

Kuna namna.

Huwa najiuliza, kwani wenzetu walianzaje? Kwanini sisi tusianze kama wao?
 
Nimesikitika sana kauli kama hii kutolewa na rais tena kwa kurudia rudia. Je hizo pesa tunapewa bure? Au ndio haya ya kuuza bandari na rasirimali zetu zingine kama mbuga?

Kwa umakini kabisa akasema madini yataisha, vingine vitaisha lakini ardhi yetu utabaki tulime😂
 
Nimetafakari iyo kauli siku nzima ya leo.kweli mtu unasema kbisa kwamba tunazunguka kutafuta pesa njee??mbona sisi tuna kila kitu??U.K pale hamna rasilimali yeyote...tuna mbuga,ardhi nzuri,madini,hali ya hewa nzuri....yaan mtu unashindwa kuelewa kwan hizi nchi za kiafrika zina shida gani jaman
 
Kama urais ni rahisi na kwamba kila mtu anauweza,omba na wewe uupate ili utuoneshe huo utajiri wa nchi uko wapi!Watu wakishavimbiwa matoke wanajiandikia hata ujingaujinga tu.
 
Hicho kila kitu kiko wapi?Omba urais utuoneshe.Hadi kuitwa ni nchi masikini,hohehahe ulidhani hawakupendi tu?Kafukue almasi,dhahabu,makaa ya mawe na tutakataka twingine utubadilishie tuwe matajiri kama USA.
 
Kama urais ni rahisi na kwamba kila mtu anauweza,omba na wewe uupate ili utuoneshe huo utajiri wa nchi uko wapi!Watu wakishavimbiwa matoke wanajiandikia hata ujingaujinga tu.
Mwaga pwenti zako basi

Utajiri pekee tuliobaki nao ni Ardhi tu vingine vyote wameshachukua wazungu na wanavimiliki na Ardhi pia wanaitaka sasa wakichukua Ardhi tumekwisha maana kuna mbwiga mmoja alieshiba mihogo mikavu na kuvimbiwa nilimsikia anasema wawekezaji na wageni wote waarabu na wazungu tuwauzie Ardhi wakihitaji
 
Pesa ziko humuhumu wanazigawa kwa waarabu na kulipa faini kwa mikataba ya kijuha.
 
.....Hapana !

..............................................................................Je kuwa ubaya gani shetani akisema kuwa nchi yetu ni tajiri tunaweza kuwa donor country?
 
Back
Top Bottom