Nchi isipotii amri ya viongozi wake kufika Mahakama ya Kimataifa ya ICC, huchukuliwa hatua gani kulazimisha?

Nchi isipotii amri ya viongozi wake kufika Mahakama ya Kimataifa ya ICC, huchukuliwa hatua gani kulazimisha?

Huwa wanasambaza arrest warrant kwa nchi zote duniani. Ukijiloga kutembelea moja wapo tu na wakakunawa unashangaa umekamatwa na unapakiwa kwenye ndege hadi Uholanzi

[emoji23][emoji23][emoji23]nani wa kusafiri sasa!!!!
 
ICC hawana mchango wowote kwa kilichomtokea Bashir huko Sudan

Labda hawana mchango...

Lakini nikuambie jambo moja, kwamba...

Rais wa nchi akishatuhumiwa tu na taasisi hii, ujue anguko lake liko mlangoni pake asubuhi tu..

Tena anguko lake ni kuu mno na huwa wanakwenda kufa na kufa moja kwa moja...

Maana cha kwanza kinachofanyika, unakuwa adui wa nchi za maana zote na wanakutenga...

Cha pili, wananchi wako wataanza kupigana nawe. Moto utachochewa toka nje mpaka utakuunguza na kukumaliza tu...

By the way, unaweza kinitajia Rais mmoja tu duniani ambaye amewahi kuwa charged na ICC kisha akaipiga chenga na kubaki madarakani akitawala...??
 
Naomba kujuzwa ni hatua zipi huchukuliwa na mahakama hii kuhakikisha watuhumiwa wanaotakiwa kufika mbele ya mahakama hii wanafika mahakamani.

Kwa mfano, Raisi wa nchi alieko madarakani anapotakiwa kufika katika hii mahakama na akagoma kwenda, ni utaratibu gani hufuata kuhakikisha anapanda kizimbani?

Je, nini nafasi ya International Criminal Police Organisation (interpol )katika kusaidia hii mahakama kutekeleza majukumu yake?

Mwenye majibu atusaidie.
JF member Salary slip umechagua njia hatarishi na mbaya sana ya kubweka kutishia kisichotishika hivi huwa unachuki na nani na kwa sababu zipi?
Wewe una uadilifu kiasi gani kujihisi ni msafi pasipo waa?

Wewe ni mwandishi wa habari, mfanyabiashara, dereva, mwanafunzi wa chuo asiye na ajira, mwanasiasa (mbunge/diwani aliyeshindwa), daktari, mwalimu au mstaafu?

Chuki na inda ulizonazo zimekusababishia athari ya kisaikolojia ambapo si mrefu utajidhuru mwenyewe kisha mkakati ulioutengeza na wenzio kwa kipindi kirefu utahamishiwa lawama zake kwa serikali eti ulikuwa mkosoaji mkubwa wa kiongozi wa nchi

Kwa kifupi elewa kwamba hiyo mahakama ambayo wewe na vipofu wengine wa kisiasa na kisheria inawaotesha maruweruwe usiku kucha haina mamlaka yoyote ya kumkamata mtu yeyote bila ridhaa na ushirikiano kutoka kwenye mamlaka ya nchi husika (There is no such arbitrary arrest as you may expect from the law enforcement agent save special permission authorization from UN council in compliance to convention artices)
 
Mbona unalia mkuu?
 
hii ishu itanfanya bwana jiwe kukataa kutoka madarakani kwa sababu akitoka tu anadakwa kama panzi,ila akiwa madarakani anaweza kujificha kwa muda
Ndoto za alinacha. Kwenye kura mmepigwa mkapanga kufanya ugaidi ikabuma sasa mnahangaika na ICC as if mmeolewa huko na ICC!
 
Navyojia mimi akikataa kufika mbele ya Mahakama hii ya kimataifa basi hati itatoka kwa nchi wanachama kusaidia kumkamata huyo bwana endapo atasafikiri basi nchi mwanachama husika inaweza kumkamata na kumkabidhi kwa ICC. kwa sababu ni jeuri basi atashikiliwa hadi kesi yake itakapokwisha.

Vinginevyo basi abakie nchini kwake kwa muda wote wa uongozi wake, ila akishatoka madarakani tu basi ananyakuliwa kama kuku bandani.
 
Ni hoja nzuri sana hii kwa ajili ya kujengeana ufahamu wa mambo haya...

Mimi nitajibu kwa uzoefu tu kwa namna nilivyoona imefanyika ktk mataifa mengine duniani...

Kwa kesi inayomhusu "a sitting president", utaratibu ni mrefu kidogo...

Ikishathibitika kuwa " kiongozi mkuu (Rais) wa nchi fulani aliye madarakani" ana kesi ya kujibu, kama kawaida atapelekewa "summon"..

Wengi huukataa huo wito wa kwenda mahakamani kwa visingizio kadha wa kadha ikiwemo kuwa " hatuitambui" mahakama hiyo..

Ilitokea kwa Rais wa Sudan - Khartoum Bw. Omar Al Bashir. Na mara zote wanaokataa hukingikiwa kifua na baadhi ya nchi zenye viingozi wenye tabia za kama huyu anayetakiwa ICC...

Shida moja kwa anayekataa kutii wito wa mahakama ya uhalifu wa kivita na ubinadamu (ICC), ni kuwa kuanzia wakati huo naye anakuwa ni "WANTED" na jumla anakuwa HAYUKO UHURU..

Kwa ufupi sana JIBU LA HOJA YAKO NI;

Hakuna kiongozi atakayetakiwa kwenda kujibu mashtaka dhidi yake kwenye mahakama hii anaweza kuukwepa mkono wa mahakama hii unless KIFO kimchukue kabla hawajamtia nguvuni..!!

Omar Al Bashir wa Sudan Khartoum alijaribu kukimbikimbia na kujificha ficha lakini mwisho wa siku, MBIO ZA SAKAFUNI HUISHIA UKINGONI tu...!!

Alikamatwaje? Bashir
 
Unajua kinachoendelea kati ya serikali ya Sudan na Icc juu ya huyo al Bashir sasaivi??
Unaongelea aftermath ya coup. Hoja mezani ilikuwa nini ICC walimfanya huyu wakati ni Mtawala. Tena alikuwa anasafiri tu.

Bottom line ni kwamba ICC haina meno marefu kama mnavyofikiria. Na pia huwa hawaprocess kesi kizembe.

Evidence inaweza kuwepo kuwa Zanzibar watu waliuawa lakini ICC wanaweza kuja kuchunguza na kusema hakuna evidence ya kutosha kuwaincriminate Rais wa sasa na watu wake wa karibu
 
Kwani mie nimesema je kuhusu nini wanaweza kumfanya???

Umesema pia evidence inaweza kuwepo alafu wao wanaweza kusema, kwa iyo unazungumzia probability au assumption.

Mimi ninachokwambia tukutane ICC
 
Kwa historia na muundo wa serikali yetu, haihitaji kumfungulia mashitaka 'Rais aliye madarakani' ili kubadilisha muelekeo wa kisiasa nchini, ingawa inaweza kuchukua muda kidogo.

Wakitajwa baadhi tu ya watendaji wa chini wa serikali na wa vyombo vingine, mfano RCs, DCs na RPOs, haitachukua muda athari zake kuanza kuonekana. Hii ni kwa sababu serikali inakuwa kwenye wakati mgumu, ukiwabakisha watuhumiwa kwenye utumishi inaonekana ni ukaidi, ukiwaondoa inaonekana unakubaliana na tuhuma hizo. Hapa ndiyo mnaanza kuitwa 'rogue nation' na majina kama hayo.

Hata kutangaza tu kuwawekea vikwazo au marufuku ya kuingia kwenye nchi zao kwa baadhi ya viongozi, huwa ina athari kubwa sana kwa viongozi wa Kiafrika. Hili suala linawaondolea 'credibility' mbele ya macho ya umma. Muulize Makonda au viongozi wa Zimbabwe watakwambia.
 
Huwa wanasambaza arrest warrant kwa nchi zote duniani. Ukijiloga kutembelea moja wapo tu na wakakunawa unashangaa umekamatwa na unapakiwa kwenye ndege hadi Uholanzi
Nakumbuka Omary Bashir aliponea chupuchupu kunyakuliwa kwenye mkutano South Africa
 
Back
Top Bottom