Nchi masikini haiwezi kuendelea ikiongozwa kidemokrasia

Nchi masikini haiwezi kuendelea ikiongozwa kidemokrasia

China mafisadi wananyogwa kwetu mafisadi na uhujumu uchumi ni kwa wale wasiotaka kuisujudia Sanamu

si ndo maaana tunatakiwa kuondokana na haya mademokrasia, kwan hujaelewa point ya thread ni nn?
 
sasa egypt si nchi ya tatu afrika inaenda ya pili kwa GDP! hakuna nchi yenye demokrasia iko kwenye izo level, kenya yenyewe wanafululiza kuchukua mahindi tanzania, una kingine mkuu?
Nimekuambia GDP PER CAPITA wewe kilaza.
 
Ili nchi iendelee inahitaji kiongozi mwenye maamuzi magumu na uthubutu. Maamuzi ambayo muda mwingine hayatapendwa na wananchi. Mambo kama haya hayawezekani chini ya demokrasia.

Hata wanaotuhubiria demokrasia kila siku wanajua kuwa haifai pale maamuzi magumu yanapohitajika. Ndiyo maana mataifa yenye nguvu yamejipa kura ya Veto umoja wa mataifa. Na pengine ndiyo maaana wanatuhubiria kila siku tuwe na demokrasia, wakijua kuwa tukiwa na demokrasia tutabaki maskini siku zote.

Demokrasia inabidi kuangaliwa upya
Ishi na huo udikteta kwenye familia yako!
Mpaka leo tunaambiwa Nyerere alituingiza chaka kwa misimamo yake aliyotulazimisha kuifuata bila kujaji wa kushirikishwa ipasavyo! Kuna wengine sasa hivi wanasema mtazamo wa kiuchumi wa Oscar Kambona ambaye Nyerere alikorofishana nae kwa kuwa na mtazamo tofauti nae ndio alikuwa sahihi, hii mana yake ni kwamba kama demokrasia ingechukua mkondo wake ipasavyo pengine leo tungekuwa mbali zaidi ya hapa!
Rejea pia utawa wa Mwendazake, baada ya kifo chake kuna madudu mengi sana ya kiuchumi yamefichuka ambayo kama demokrasia ingechukua mkondo wake tusingefika huko!
Aisee usitukumbushe hayo machungu, hakuna binadamu mkamilifu hivyo kiongozi yeyote anajiweka kuwa yeye ndiye know All, hapa ni lazima tu atalifikisha taifa lake mahala pasipo na njia! Njia bora ya kupata mafanikio ni kushirikisha mawazo ya watu wengi na si vinginevyo!
 
Ni nchi za kawaida sana they arenot countries you can aim to reach! yaaani ni kama mwaka mmoja tu nchi ikiwa serious inaruka that stage
Si waambie CCM waifikishe hapo kwa Huo mwaka mmoja , ukifika Oktober 2022 alau Tobo Yao tuwafike
 
Ili nchi iendelee inahitaji kiongozi mwenye maamuzi magumu na uthubutu. Maamuzi ambayo muda mwingine hayatapendwa na wananchi. Mambo kama haya hayawezekani chini ya demokrasia.

Hata wanaotuhubiria demokrasia kila siku wanajua kuwa haifai pale maamuzi magumu yanapohitajika. Ndiyo maana mataifa yenye nguvu yamejipa kura ya Veto umoja wa mataifa. Na pengine ndiyo maaana wanatuhubiria kila siku tuwe na demokrasia, wakijua kuwa tukiwa na demokrasia tutabaki maskini siku zote.

Demokrasia inabidi kuangaliwa upya
Kwani kiongozi mwenye maamuzi magumu hapatikani kwenye nchi yenye demokrasia? Nchi za magharibi zimewezaje? Na maamuzi magumu unayozungumzia ndiyo yapi?

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom