Nchi nyingi nilizotembelea mikate ni chakula ila huku kwetu ni kitafunwa

Nchi nyingi nilizotembelea mikate ni chakula ila huku kwetu ni kitafunwa

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Kweli kila nchi na tamaduni zake, msosi pia ni sehemu ya tamaduni. Wakati bongo tunajivunia chipsi yai, au supu chapati usichukulie poa, Mrisho Ngasa na Kapombe walishindwa kucheza Ulaya kisa chipsi yai.

Turudi kwenye mada, nikiwa Cape town, nilishuhudia watu wakila soda na mikate kama mlo, Zimbabwe, Zambia, USA wataita hotdog Ila ndio huohuo, Ulaya ukipandisha bei ya mkate utapata shida Sana.

Kwa wakristo sala ya Bwana kuna ile phrase ya our daily bread imekuwa termed kama chakula, hata Yesu Alilisha watu elfu tano samaki na mkate. Mkate ni chakula sio kitafunwa Kwa wenzetu.
 
Kweli kila nchi na tamaduni zake, msosi pia ni sehemu ya tamaduni. Wakati bongo tunajivunia chipsi yai, au supu chapati usichukulie poa, Mrisho Ngasa na Kapombe walishindwa kucheza Ulaya kisa chipsi yai.

Turudi kwenye mada, nikiwa Cape town, nilishuhudia watu wakila soda na mikate kama mlo, Zimbabwe, Zambia, USA wataita hotdog Ila ndio huohuo,
Ulaya ukipandisha bei ya mkate utapata shida Sana.

Kwa wakristo sala ya Beans kuna ile phrase ya our daily bread imekuwa termed kama chakula, hata Yesu Alisha watu elfu tano samaki na mkate,
Mkate ni chakula sio kitafunwa Kwa wenzetu.
Unalosema ni kweli kabisa na ninashangaa inakuaje hapa bongo kunakuwa na tatizo la nguvu za kiume wakati tuna vyakula vyenye nguvu na virutubisho.

Sasa mfano SA nilifika nikakuta machakula hayaeleweki nikajiuliza hawa wanaishije. Nadhani kibongo bongo tuna tatizo la kukinai ngono lakini kwa nguvu siamini hata kidogo kwamba kwa kula chipsi yai ndio kufanye mtu asiwe na nguvu za kiume wakati zipo nchi hawajui wali na wakipika wali wao utakimbia.
 
Mkate ni chakula Bora Sana ukimiminia na Mayai
Mkate mwenyewe nakula na kulala vizuri kabisa ni uandaaji tu
Ila kama ni mkate tu na chai hiiiiiiiiii
Mkate ni ngano kinachotuchanganya wabongo ni namna ulivyotengenezwa mfano mimi naweza rudi home nikakuta watoto wanakula mkate na kitimoto na maziwa hapo hata aliekula wali haoni ndani.

Mkate ni chakula safi kabisa tumezieshwa tu kula kama kitafunwa ila wenzetu wanachanganya mkate na mboga mboga unaskia burger akiweka mkate na sausage unaskia hotdog ilimradi tu watuvuruge ila ni mkate kama mkate tu.
 
Back
Top Bottom