Nchi nyingi nilizotembelea mikate ni chakula ila huku kwetu ni kitafunwa

Nchi nyingi nilizotembelea mikate ni chakula ila huku kwetu ni kitafunwa

Mkate ni ngano kinachotuchanganya wabongo ni namna ulivyotengenezwa mfano mm naweza rudi home nikakuta watoto wanakula mkate na kitimoto na maziwa hapo hata aliekula wali haoni ndani.

Mkate ni chakula safi kabisa tumezieshwa tu kula kama kitafunwa ila wenzetu wanachanganya mkate na mboga mboga unaskia burger akiweka mkate na sausage unaskia hotdog ilimradi tu watuvuruge ila ni mkate kama mkate tu
Hata iweje mkate ni chakula kinachafaa kuliwa zaidi usiku, mtu katoka kupiga jembe au mpiga tofari umpe mkati na mchuzi mchana.
 
Kweli kila nchi na tamaduni zake, msosi pia ni sehemu ya tamaduni. Wakati bongo tunajivunia chipsi yai, au supu chapati usichukulie poa, Mrisho Ngasa na Kapombe walishindwa kucheza Ulaya kisa chipsi yai.

Turudi kwenye mada, nikiwa Cape town, nilishuhudia watu wakila soda na mikate kama mlo, Zimbabwe, Zambia, USA wataita hotdog Ila ndio huohuo,
Ulaya ukipandisha bei ya mkate utapata shida Sana.

Kwa wakristo sala ya Bwana kuna ile phrase ya our daily bread imekuwa termed kama chakula, hata Yesu Alisha watu elfu tano samaki na mkate,
Mkate ni chakula sio kitafunwa Kwa wenzetu.
Sijajua mtu anaishije na mkate, Mimi nikila inazalisha ( acid) kiungulia kingi tumboni
 
Bongo kuna vyakula vitamu sana. Ukienda kwa majirani utawaonea huruma vyakula vyao na jinsi wanavyovipika. Kenya wana ile githeri.
Huu sasa ni ulimbukeni. Unadhani wewe ndiyo bora kuliko wengine. Unachotakiwa kujua ni kuwa chakula ni utamaduni. Unachoona ni kizuri kwako kinaweza kuwa kibaya kwa mwenzako.
 
Back
Top Bottom