Nchi nyingi nilizotembelea mikate ni chakula ila huku kwetu ni kitafunwa

Nchi nyingi nilizotembelea mikate ni chakula ila huku kwetu ni kitafunwa

Kweli kila nchi na tamaduni zake, msosi pia ni sehemu ya tamaduni. Wakati bongo tunajivunia chipsi yai, au supu chapati usichukulie poa, Mrisho Ngasa na Kapombe walishindwa kucheza Ulaya kisa chipsi yai.

Turudi kwenye mada, nikiwa Cape town, nilishuhudia watu wakila soda na mikate kama mlo, Zimbabwe, Zambia, USA wataita hotdog Ila ndio huohuo, Ulaya ukipandisha bei ya mkate utapata shida Sana.

Kwa wakristo sala ya Bwana kuna ile phrase ya our daily bread imekuwa termed kama chakula, hata Yesu Alilisha watu elfu tano samaki na mkate. Mkate ni chakula sio kitafunwa Kwa wenzetu.
asa hii ya huku nayo mikate? au tunakula maboksi na chai tu
 
Tatizo la nguvu za kiume halipo ila wafanyabiashara wa mitishamba walitengeneza liwe tatizo ili wapige hela kwa kulitangaza sana.

Vilevile kama umenotice kitu currently kuna wahuni wana advocate" Mental Health" kwa kufanya ionekane kuwa ni tatizo kubwa linalohitaji intervention wakati hata halipo watu wanatafuta namna ya kupiga hela za watu.

Rejea namna mafuta ya wanyama yalivyopigwa vita na watengenezaji wa mafuta ya mimea enzi hizo utabaini trend ilivyo.

Usicheze na wajasiriamali.
Sasa kama halipo, kelele za majumbani ni za nini sasa?[emoji3] unakuta Baba mzima anamkimbia mke anashinda anazurura kama mbuzi wamtaani kule buguruni ha ha ha ha, sasa shida ni nini?[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Yani unakula mkate alafu unaenda shamba kulima 🤔🤔 ili nile mkate nitosheke ni mifuko miwili mikubwa tena hiyo ni chai tuu, tuache na ushamba wetu tuu, kula ugali ni utamaduni wetu
 
Watu wameaminishwa tu kuwa kuna tatizo hilo vichwani mwao na wanawake nao wameaminishwa hivyo inageuka kuwa psychological battle kwa kila upande ilihali hawana tatizo lolote.

Nguvu za kiume as a problem limeibuka 2010 jamii nzima inaweza kuugua ugonjwa unaofanana in a span of 12 yrs ?
 
Mmmm labda, sasa kama mke yupo tu Mme anamuona kama jinsia yake, sasa hapo mke atasema nini hapo?
 
Umenikumbusha mbali sana mkali. Nikiwa "nabeba box" miaka hiyo 2009 mitaa ya Hounslow TW6 1QG tulikuwa tunashindia mikate, maziwa ya kopo na siagi mimi na mshikaji wangu Jerry.

Tulikuwa wanafunzi, tukatafuta kazi ili kujikimh na kazi yetu ilikuwa ni kupanga bidhaa katika Supermarket tukilipwa kwa saa na tukipewa mikate, maziwa na siagi kama posho ya kazi
 
Yani unakula mkate alafu unaenda shamba kulima 🤔🤔 ili nile mkate nitosheke ni mifuko miwili mikubwa tena hiyo ni chai tuu, tuache na ushamba wetu tuu, kula ugali ni utamaduni wetu
Unaambiwa mikate isiyotiwa chachu na samaki.
 
Mayonnaise ndiyo vitu gani mkuu ?
hellmann-s-mayonnaise-400g.jpg

Hii ni sauce kama mfano tamoto sauce. Mayo unaweza tumia kwenye kula chips kama unavyoweka tomato sauce.
 
Bongo kuna vyakula vitamu sana. Ukienda kwa majirani utawaonea huruma vyakula vyao na jinsi wanavyovipika. Kenya wana ile githeri.

Uganda utachoweza ni zile Rolex zao tu vyengine ugusi haha wale watu hawajui kupika kabisa
 
Back
Top Bottom