Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Ni Imani yangu walioweka sharti kamati za Bunge: PAC, POAC na LAAC ziongozwe na Wapinzani, walijua umuhimu huo wakiamini wapinzani wana nafasi nzuri zaidi katika kuibana serikali kwenye suala zima la matumizi ya fedha za Umma na zile zinazotolewa na wahisani.
Kwa sababu hiyo, naamini mpaka sasa wahisani hawa watakuwa wanafuatulia, na hivyo wana taarifa zote za nini kinaendelea hasa kuhusu tuhuma/ madai ya NEC kupeleka majina ya Wabunge wa viti maalum wa CHADEMA huku CHADEMA wakikana majina hayo.
Katika hili sakata, ninachotarajia kukiona ni wafadhili kusita kutoa fedha zao iwapo watajiridhisha juu ya madai hayo na watakuwa tayari tu kutoa hizo fedha pale kamati hizo zitapoongozwa na watu wanaostahili na si vinginevyo.
Kama tungekuwa na Uchaguzi Huru na wa Haki, na CCM wakashinda viti vyote, basi hapo hata wafadhili wengeona umuhimu wa kutazama upya jambo hili au kuangalia kanuni zinasemaje iwapo itatokea wapinzani wanashindwa kihalali katika Uchaguzi, lakini sio kwa Uchaguzi huu na zaidi si kwa hizi tuhuma za kutaka kufoji majina ya Wabunge wa viti maalum kutoka Upinzani ili wakaunde hizo Kamati.
Huu pia, kulingana na mtazamo wangu, unaweza kuwa ni mbinyo wa awali wa kulazimisha tuwe na mifumo huru ya Uchaguzi na hata kukazia madai ya Wapinzani kutaka Uchaguzi urudiwe.
Muda utaongea.