Nchi ya Chad inaruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja kwa dini zote, Nusu ya wanaume wakristo wana mke zaidi ya mmoja, Je ukristo unawabana wanaume?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Ifike mahala jamii ikubaliane na uumbaji wa Mwenyezi Mungu na namna alivyomuumba mwanaume.

Nchini Chad, unaweza kuoa zaidi ya mke moja hata kwa ndoa ya kikristo, hali hii imepelekea zaidi ya nusu ya wanaume wenye imani ya kristo kuoa zaidi ya mke moja....kuna asilimia kubwa ya wanaume wakristo wenye mke zaidi ya moja kuliko waislamu.

Nchi kama zetu hizi ndoa za kikristo zipo kwa nadharia zaidi kuliko uhalisia, Mwanaume wa kiafrika kutosheka na mke moja ni nadra sana, ipo ndani enzi hadi enzi hata utamaduni wetu mababu zetu wameoa mke zaidi ya moja, hata kwenye biblia manabii kibao walioa mke zaidi ya moja na kufanya kazi za kinabii kwa baraka zote.

Biblia haijakataza Mwanaume kuoa mke zaidi ya moja ila ni viongozi wa dini za . kikristo wanajitungia mambo na kuyaita sheria za Kanisa, Manabii kibao karibu wote walioa mke zaidi ya mmoja

Matokeo ya hizi ndoa za mke moja michepuko imeshamiri sana ndoa za kikristo, Wanawake hujihisi wapo sawa na waume zao maana mume wake hana ujanja wa kuongeza mke, n.k.

kuna kupotoshana kwamba mwanaume inabidi aoe mke moja ili kutimiza kauli ya "mwili moja", hilo neno halijawahi kumaanisha kwamba mwanaume asioe mke zaidi ya moja.

1 Wakorintho 6:16
Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.
 
Ndoa za kikristo hupelekea pia vijana wengi wa kikristo kuchelewa kuoa, yani unakuta mtu ana miaka 33 bado hajaoa tu kwasababu ya kuhofia kuingia kwenye ndoa ambayo huwa ni kama gereza kwa jinsi Mungu alivyotuumba wanaume.

Vijana wengi wa kiislam huwa wanaoa kabla hata hawajafikia 25.
 
Propaganda.
Ina maana nchi ndo inapanga taratibu za dini?
Kama unatamani wake 6 wee oa tuu
Imani yako ndio itayokufanya ufate unachoona ni sahihi,

Na pia hakuna sehemu katika biblia iliyokataza kuoa mke zaidi ya moja
 
Kiuhalisia wanawake ni wengi kuliko wanaume popote pale. Kati ya hawa wanaume kuna: makasisi, mashoga, watoto wa kiume, mabachelor nk. Kundi ambalo lipo kwa ajili ya kuoa ni wachache sana, hivyo hata mie nashauri pia kanisa liangalie uwezekano wa kuruhusu sisi wakristu kuoa mke zaidi ya mmoja. Hata mie sitaki kuchepuka ikiwezekana nikaruhusiwa wake watatu nitafurahi sana. .
 
Kwani nchi gani iliyozuia wakristo kuoa zaidi ya mke mmoja?
 
Stori za vijiwe vya kahawa hizi ndugu
 
Yawezekana matatizo ya kijamii/kiusalama ya nchi hiyo yanachochewa na mambo kama hayo
 
Kwani mkiwa watatu inashindikana kiwa mwili mmoja? Kila mmoja kwa wakati wake?
 
Sio lazima uoe mke m'moja unaweza kuongeza ni wewe tu utaamua kuweza kuishi nao ama la.

Kwa tamaduni zetu inaruhusiwa. Babu yangu alikuwa na wake 5.
 
Sio lazima uoe mke m'moja unaweza kuongeza ni wewe tu utaamua kuweza kuishi nao ama la.

Kwa tamaduni zetu inaruhusiwa. Babu yangu alikuwa na wake 5.
Hapa zinazungumziwa ndoa za kikristo,
 
Mkuu ngoja nizame chimbo nipate maujuzi nije nikupe idea nyingine
 
Yawezekana matatizo ya kijamii/kiusalama ya nchi hiyo yanachochewa na mambo kama hayo
Hamna kitu hapo, Hao ni wakristo wanaojitambua vizuri kabisa, wanaoa kwa misingi ya kikristo vizuri tu.
 
Apataye mke amepata kitu chema, naye ajipatia kibali kwa Bwana.

Zingatia mke sio wake...
Wewe ni mwanamke najua utatumia nguvu kubwa sana usipandishwe cheo kuwa mke mkubwa...
 
Je ni dini au serikali inayoruhusu, kama ni serikali hata hapa kwetu inaruhusu hata 10
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…