Nchi ya Chad inaruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja kwa dini zote, Nusu ya wanaume wakristo wana mke zaidi ya mmoja, Je ukristo unawabana wanaume?

View attachment 2254348

Hali ndivyo ilivyo, Dini ya kikristo imekuwa ni kama gereza kwa wanaume wengi ambao wanahitaji kuwa na mke zaidi ya moja lakini hawana namna,

Nchini Chad, unaweza kuoa zaidi ya mke moja hata kama ni mkristo, hali hii imepelekea zaidi ya nusu ya wanaume wa kiksrito kuoa zaidi ya mke moja....kuna asilimia kubwa ya wanaume wakristo wenye mke zaidi ya moja kuliko waislamu.

Pia biblia haijawahi kukataza kuoa mke zaidi ya moja bali ni makanisa yaliyotengenezwa na wazungu yanayopotosha kwamba mwanaume inabi aoe mke moja ili kutimiza kauli ya "mwili moja", hilo neno halijawahi kumaanisha kwamba mwanaume asioe mke zaidi ya moja.

1 Wakorintho 6:16
Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.
Kwa huku kwetu wala tusijaribu,kama mke mmoja unajipiga risasi,ukiwa nao watano si itakuwa balaa...
 
Nchini Chad, unaweza kuoa zaidi ya mke moja hata kama ni mkristo, hali hii imepelekea zaidi ya nusu ya wanaume wenye imani ya kristo kuoa zaidi ya mke moja....kuna asilimia kubwa ya wanaume wakristo wenye mke zaidi ya moja kuliko waislamu.

Nchi kama zetu hizi ndoa za kikristo zipo kwa nadharia zaidi kuliko uhalisia, Mwanaume wa kiafrika kutosheka na mke moja ni nadra sana, ipo ndani enzi hadi enzi hata utamaduni wetu mababu zetu wameoa mke zaidi ya moja, hata kwenye biblia manabii kibao walioa mke zaidi ya moja na kufanya kazi za kinabii kwa baraka zote.

Matokeo ya hizi ndoa za mke moja michepuko imeshamiri sana ndoa za kikristo, Wanawake hujihisi wapo sawa na waume zao maana mume wake hana ujanja wa kuongeza mke, n.k.

Pia biblia haijawahi kukataza kuoa mke zaidi ya moja bali ni makanisa yaliyotengenezwa na wazungu yanayopotosha kwamba mwanaume inabi aoe mke moja ili kutimiza kauli ya "mwili moja", hilo neno halijawahi kumaanisha kwamba mwanaume asioe mke zaidi ya moja.

1 Wakorintho 6:16
Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.
Ni upuuzi tuu wa hapa Bongo
 
Propaganda.
Ina maana nchi ndo inapanga taratibu za dini?
Kama unatamani wake 6 wee oa tuu

Kwani cheti cha ndoa kinatoka wapi haujui Kua cheti cha ndoa ni mali ya serikali
 
kila mwanamke sasa hivi ana mwanaume, bila kujali uchache wao!
ndoa za wake wengi zitapelekea kuhalalishwa kwa mahuasisio ya pembeni.

kwamba iwe ni ndoa ya mke moja ni sawa, lakini sio mwisho wa mahusiano ya pembeni.Mara zote kinacho amua ni Muda.Ni suala la muda tu!
 
Kiuhalisia wanawake ni wengi kuliko wanaume popote pale. Kati ya hawa wanaume kuna: makasisi, mashoga, watoto wa kiume, mabachelor nk. Kundi ambalo lipo kwa ajili ya kuoa ni wachache sana, hivyo hata mie nashauri pia kanisa liangalie uwezekano wa kuruhusu sisi wakristu kuoa mke zaidi ya mmoja. Hata mie sitaki kuchepuka ikiwezekana nikaruhusiwa wake watatu nitafurahi sana. .
Kwanini Hadi uruhusiwe na kanisa?
Kanisa ndio mungu wako anaekupangia Sheria za dini?
 
hata hapa Bongo, wanaume wengi wa Kikristo wameoa na wanamiliki michepuko kadhaa ambao nao ni kama wake tu maana unakuta wamezaa na either wamejengewa nyumba au kupangishiwa..

Hata Waislam wengi unakuta ana mke mmoja halafu anamiliki michepuko kadhaa, sasa unajiuliza si ni bora aoe tu kadhaa ijulikane moja..

Genetically Mwanaume ameumbwa kuwa na wanawake zaidi ya mmoja tofauti na hapo ni kupambana na nature tu....
Akina mama nao wafike mahala wakubaliane na hili na wawe waungwana tu ili wengi wawe kwenye miji yao...

Genetically Mwanamke ameumbwa kuwa na mwanamme mmoja na ni heshima kuubwa mwanamke kuwa kwenye ndoa na mji wake haijalishi ni mke wa ngapi ila ni heshima kuubwa kwao..
 
Nchini Chad, unaweza kuoa zaidi ya mke moja hata kama ni mkristo, hali hii imepelekea zaidi ya nusu ya wanaume wenye imani ya kristo kuoa zaidi ya mke moja....kuna asilimia kubwa ya wanaume wakristo wenye mke zaidi ya moja kuliko waislamu.

Nchi kama zetu hizi ndoa za kikristo zipo kwa nadharia zaidi kuliko uhalisia, Mwanaume wa kiafrika kutosheka na mke moja ni nadra sana, ipo ndani enzi hadi enzi hata utamaduni wetu mababu zetu wameoa mke zaidi ya moja, hata kwenye biblia manabii kibao walioa mke zaidi ya moja na kufanya kazi za kinabii kwa baraka zote.

Matokeo ya hizi ndoa za mke moja michepuko imeshamiri sana ndoa za kikristo, Wanawake hujihisi wapo sawa na waume zao maana mume wake hana ujanja wa kuongeza mke, n.k.

Pia biblia haijawahi kukataza kuoa mke zaidi ya moja bali ni makanisa yaliyotengenezwa na wazungu yanayopotosha kwamba mwanaume inabi aoe mke moja ili kutimiza kauli ya "mwili moja", hilo neno halijawahi kumaanisha kwamba mwanaume asioe mke zaidi ya moja.

1 Wakorintho 6:16
Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.
Kwani kuoa mke mmoja au zaidi ya mmoja, serkali inahusikaje?
 
Sijapata jibu, nitajieni nchi yoyote duniani inayozuia wakristo kuoa zaidi ya mke mmoja
 
Ifike mahala jamii ikubaliane na uumbaji wa Mwenyezi Mungu na namna genetics zilivyo, kutofautiana na nature ni kutengeneza matatizo mengi ambayo jamii sasa inapitia...
 
hata hapa Bongo, wanaume wengi wa Kikristo wameoa na wanamiliki michepuko kadhaa ambao nao ni kama wake tu maana unakuta wamezaa na either wamejengewa nyumba au kupangishiwa..
Hao ni michepuko na hawatambuliki hata kisheria, hata watoto wa michepuko hawatambuliki kwenye mirathi.
 
Sijapata jibu, nitajieni nchi yoyote duniani inayozuia wakristo kuoa zaidi ya mke mmoja
Huenda hata barua ya posa huijui mkuu, ukioa ndoa ya kikrtisto, kanisa na cheti cha ndoa hakitakuruhusu kuongeza mke,
 
1 Wakorintho 7:1-2​

Na sasa kuhusu mambo mliyoniandikia. Ni vizuri mtu asioe. 2 Lakini kwa kuwa dhambi ya zinaa imeenea, kila mwanamume awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.
 
Oa hata kumi, kwa Tanzania hakuna sheria inazuia kuoa zaidi ya mke mmoja, ila kama ni mtu wa imani itategemea uko upande gani maana wengine unaweza kuoa zaidi ya mmoja (waislam) na wengine hawaruhusu kuoa hata mmoja ( Ukiwa padri wa katoliki huruhusiwi kuoa kabisa)
 
Huenda hata barua ya posa huijui mkuu, ukioa ndoa ya kikrtisto, kanisa na cheti cha ndoa hakitakuruhusu kuongeza mke,
Siamini kama kiswahili ni kigumu namna hii!! Nitajie NCHI MOJA TU inayozuia wakristo kuoa wake wengi. Sitaki kusikia habari ya kanisa, nadhani umenielewa vema. Mtoa mada anaongelea SERIKALI YA CHAD na sio KANISA LA CHAD. Read between lines, mnasumbuliwa na fallacy tu hapa. Habari hii ni uzushi mkubwa kwa kulihusisha kanisa, ni upuuzi endelevu kama ilivyozoeleka toka kwa watu wasioweza kudhibiti tamaa zao. Upuuzi mtupu
 
kwa ufupi ni kwamba, Chad unaruhusiwa kuoa mke zaidi ya moja kwa ndoa ya kikristo.

Sizungumzi ndoa za bomani ambazo kama utahitaji kuongeza mke siku za mbele, inabidi uweke wazi.
 
Unawashwa sana na maagizo ya biblia wewe kijana wa mudi. Oa hata 72 ili uwe sawa na mnyaazi hata kabla hujafika ahera.

Hao wanaume wa Chad kama kweli wanaoa wewe fahamu kwamba hao sio wakristo.

Halafu hata serikali ya Tanzania inaruhusu idadi yoyote.
 
Back
Top Bottom