Nchi ya Chad inaruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja kwa dini zote, Nusu ya wanaume wakristo wana mke zaidi ya mmoja, Je ukristo unawabana wanaume?

Hao wanaume wa Chad kama kweli wanaoa wewe fahamu kwamba hao sio wakristo.
idadi kubwa ni waumini wa roma na lutheran...

kuna mambo wakristo wanaminywa kwa mukosea kutafsiri biblia maana hakuna sehemu Mungu kakataza kuoa mke zaidi ya mmoja.
 

Kwan Serikali inahusika vipi na dini ya ukristo hadi iingilie huko??
Serikali inatambua ndoa ya mke zaidi ya mmoja!!
sasa unapotaka serikali kuingilia dini kwene maamuzi ya imani unakosea
 
Kwan Serikali inahusika vipi na dini ya ukristo hadi iingilie huko??
Serikali inatambua ndoa ya mke zaidi ya mmoja!!
sasa unapotaka serikali kuingilia dini kwene maamuzi ya imani unakosea
Mimi kwenye hii hoja yako na mada kwa ujumla nina swali moja fupi tu. Je, sheria ya ndoa ya Tanzania (iliyotungwa na serikali) inaruhusu mwanandoa wa kiume aliyefunga ndoa ya kikristo na kupewa cheti cha ndoa (cha serikali) kuoa zaidi ya mke mmoja hasa inapotokea kwamba kwenye cheti hicho hakuna sehemu yoyote iliyobainisha kwamba ndoa iliyofungwa na kutajwa kwenye hicho cheti ni ya mke mmoja au wengi?
 
Je ni dini au serikali inayoruhusu, kama ni serikali hata hapa kwetu inaruhusu hata 10


Hakuna kitabu cha Kidini kinachokataza Mwanaume kuoa wake wengi.

Wakristo wanajitungia mambo na kuyaita sheria za Kanisa ambazo haziendani na Kitabu Chao.

Manabii kibao karibu wote walioa mke zaidi ya mmoja
 
Huu utaratibu wa ndoa ya mke mmoja nadhani unawafaa zaidi Mabeberu! Kwa sisi Waafrika, naamini ndoa ya wake wengi ndiyo inayofaa zaidi!

Dini ya Kikristo nayo ingeruhusu ndoa za aina hii, basi harakati za kutafuta nyumba ndogo zingepungua kwa kiasi fulani.
 
Nchi yetu haikatazi ndoa ya wake wengi hata kama we ni mkiristo.ukienda kuoa bomani unaruhusiwa kuchagua hii ndoa ni mke mmoja au utaongeza bdae hata kama we ni mkiristo,vivo hvyo ukioa kimila.
 
Kwa hiyo Mungu alipoanzisha ndoa Adamu alikuwa na wake wangapi?

Wewe kama unataka wake wengi silimu ili ukaoe wake wengi. Au kasajili dini yako binafsi yenye kuruhusu hilo. Ila kwa anayesoma Biblia anajua kuwa kwa Mkristo kuoa ni mke mmoja wa kike na mume mmoja wa kiume. Nukta! Hayo mengine yote yanatoka kwa yule mwovu!
 
Waambie wasilimu tu ili waoe haraka. Ya nini kutaabika na kuna alternative?
 
Hapa zinazungumziwa ndoa za kikristo,
“Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”
‭‭Mwa‬ ‭2:24‬

Hapa ndipo ndoa ya Kikristo ilipoanzia. Hao wake wengi unawapt wapi?

Kama vipi mtafute sheikh Mokaze akusilimishe ujitwalie wake wanne.

Acha kulazimisha yasiyolazimishwa. Jisalimishe kwa Allah utapata hao wake. Huku kwenye Ukristo hakuna hiyo kitu hata ukikaza misuli namna gani
 
Anao akiwa na 25 ila akigikisha miaka 30 anakuwa ameacha wake Zaid ya wa4 Sasa hiyo ni ndoa ama kudonoa.
 
Imani yako ndio itayokufanya ufate unachoona ni sahihi,

Na pia hakuna sehemu katika biblia iliyokataza kuoa mke zaidi ya moja
Kama hujui kitu kaa kimya chief. Wewe hayo ya kiislam hujaweza kuyatimiza yote unataka kusema nini? Yesu mwenyewe ndio alisema tangu mwanzo hakuwa hivyo inampasa mume mmoja awe na mke mmoja. We kama unatamaa hujakatazwa oa tu.
 
Apataye mke amepata kitu chema, naye ajipatia kibali kwa Bwana.

Zingatia mke sio wake...
Concept ya hili andiko walimaanisha jinsia na sio Idadi.Na ndo maana kwenye kitabu hicho hicho kuna andiko linasema natufanye mtu kwa mfano wetu,zingatia mtu sio watu.
 
Inaonekana hiyo biblia uisomi ukaielewa unaikariri.
 
Mwanamme mwenye wake 4 anakuwaga hana michepuko?( mwanamme ni mtu wa tamaa, hata wake 4 hawatamtosha , atachepuka tuu) Je wake wengi uwezo wa kutunza familia nzima upo?( kila mke atakuwa anazaa watoto)
 
yah na mpaka anafikisha 30 si ajabu kukuta kashatoa taraka kwa wanawake 4
 
Sijaelewa bado point yako!

Well mimi babu yangu mzaa mama alikuwa na wake saba na watoto mpaka wengine walifahamiana kwenye msiba wake sasa utaniambia na Tanzania ni Chad ama vipi?
 
Wakristo tunabanwa tuone Mke mmoja,,,halafu tena Kuachana nae tunakatazwa....

Wenzetu wa Allah wao wanaoa Wake wengi,, halafu na kuachana kupo wazi hawajakatazwa......na bado tena wana ahadi wakifika mbinguni wameandaliwa Vigoli.... Yaaani wao ni Full Maunono.

Ila kiserikali hata ukitaka kuoa kijiji kizima haizuiii...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…