Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Kuna shirika moja la kiutafiti liliwahi kufunga mjadala kwa kusema 3/4 au tuseme 75% ya Watanzania ni wendawazimu. Yawezekana ni zaidi ya 75% ila waliogopa tu kusema ukweli.
Mwaka wa uchaguzi mkuu Tanzania kuanzia JANUARI mpaka November kuna mambo mengi sana yanafanyika ambayo yanadhihirisha utahira wa Watanzania.
Kwa mfano suala la ugawaji gesi ya lita 6 kwa wananchi kama njia ya kupambana na uchafuzi wa mazingira huku mchakato wa kusafisha gesi asilia ukitiwa kapuni.
Suala la kuanzishwa kwa taasisi nyingi ndani ya mwaka huu zenye jina la Samia zikijinasibu kutatua kero za makundi mbalimbali. Kwanini huyo Rais Samia asiziimarishe taasisi za serikali ambazo takribani 450 ? Zikiimarishwa taasisi za serikali kero hazitakuwepo kabisa na zikiwepo zitatatuliwa na taasisi hizo za serikali na si hizi ambazo hatujui ni za binafsi au za namna gani. Hatujui fungu za pesa wanatoa wapi.