GE2025 Nchi yangu inafuka moshi, wazima moshi msitumie moto kuuzima moshi, Embu tumieni Meza ya mazungumzo!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

mkulimamiwa

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2025
Posts
2,591
Reaction score
5,315
Ukweli usiopingika, Nchi hujengwa na umma wa wote

Linapotokea tishio lolote aidha la kijamii au tishio la nchi na serikali, kubwa kabisa la kutizama, Ni kupima athari za jambo hilo kwa haraka na kisha kuchukua hatua, sijawahi kukubaliana na yeyote, eti anishawishi kwamba, iko faida katika kuanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe,

Vita vya wenyewe kwa wenyewe, mara zote ukiziangalia kwa jicho la tatu, huwa zinatokea kwa sababu tu, mtu aliyetakiwa awe mtatuzi, hakufanya kazi yake ipasavyo

Nchi yangu sasa, inafuka moshi, kabla moshi haujawa moto, ni vyema sana na tunawaomba viongozi wetu, wachukue maamzi mazito ya kuepusha hili lisitokee, kwani hasara yake haimlengi mtu aliyeko Nanjilinji pekee, bali hasara yake inalenga jamii nzima ya watanzania bila kujali vyeo na madaraja yao waliyonayo

Tafadhali sana, Huu wakati ambapo nchi ikiendelea kufuka moshi, wale wanaoukoleza kwa kutumia power waliyonayo, tunashauri pia kwa sasa waache

Kama kweli kipo kikundi maalumu kinachotambulika huko juu ambacho kazi yake ni kuteka na kupoteza watu, kwa kufanya hivi ni sawa na kuukoleza moto uwake

Cha kushauri, Ni viongozi wetu wakuu wa kiserikali, viongozi wa Dini, viongozi wa Kisiasa na watu mashuhuri, mkae meza moja ili kuleta suluhu ya jambo hili

Kuna msemo wa wahenga walisema, ni bora kuchelewa uendako ili ufike salama!

Endapo likatokea hili ambalo linafuka moshi likawaka moto, watu wakachinjana, wakuuwana n.k, historia itasema juu yenu viongozi mliopo na kwamba mliruhusu jambo hili la aibu na fedheha kutokea katika kipindi cha nyinyi mkiwa madarakani, majina yenu yoote yataingia kwenye kitabu hiki, Waziri mkuu, Makamu wa Rais, Rais, Katibu mkuu kiongozi, mawaziri, hata Wazanzibar mtaingia kwenye book hili la aibu

Je, kunafaida ipi iwapo maelfu na maelfu ya watu wakauwawa kisa tu walikuwa wakilalamikia sheria fulani fulani zinawakandamiza na ninyi hamkuchukua hatua?

Tutapata hasara gani kama nchi tukaamua kuwasikiliza hawa wanaolalamikia hayo kwa kusitisha baadhi ya mambo ili kukaa kitako kwa ajili ya kuwekana sawa?

Kwa mfano, Tukiahirisha uchaguzi kwa muda, na si kwamba tunaahirisha uchaguzi labda kwa faida ya watu wa nchi jirani, hapana, bado ni kwa faida yetu sisi wenyewe tukiwa na faida mikononi mwetu ya kuepusha moshi kuwa moto

Mungu, Bariki Tanzania, bariki viongozi wetu na uwape uvumilivu na hekima inayovuka viwango vya kibinadamu

Amina
 
Unfortunately aliyoyapanga Mungu siku zote lazima yatimie na si rahisi kujua. Na kama Mungu amekusudia kutuhadhibu kwa ajili ya uovu wetu njia pekee ya kuepuka ni kwa njia ya toba na sala peke yake. Hata hivyo Mungu ni wa rehema kwa sababu kuna watu wanaomba na kutubu kwa ajili ya nchi yetu usiku na mchana na Mungu atatuponya na kupita salama.
 
Mkuu,

Nchi za waliowahi kuchinjana kwa wingi, hakujawahi kuwepo watakatifu wa kuombea?

Au watakatifu wapo Tanzania pekee,

Samahani, naomba tu kujifunza kwako
 
Huu ushauri ni mzuri ila ubabe ukitumika kulazimisha mambo yaende bila muafaka ni hasara. Ni suala la busara na hekima tu kutumika ili kuepusha dhahma na fedheha kwa taifa
 
Ukweli usiopingika, Nchi hujengwa na umma wa wote

Linapotokea tishio lolote aidha la kijamii au tishio la nchi na serikali, kubwa kabisa la kutizama, Ni kupima athari za jambo hilo kwa haraka na kisha kuchukua hatua, sijawahi kukubaliana na yeyote, eti anishawishi kwamba, iko faida katika kuanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe,

Vita vya wenyewe kwa wenyewe, mara zote ukiziangalia kwa jicho la tatu, huwa zinatokea kwa sababu tu, mtu aliyetakiwa awe mtatuzi, hakufanya kazi yake ipasavyo

Nchi yangu sasa, inafuka moshi, kabla moshi haujawa moto, ni vyema sana na tunawaomba viongozi wetu, wachukue maamzi mazito ya kuepusha hili lisitokee, kwani hasara yake haimlengi mtu aliyeko Nanjilinji pekee, bali hasara yake inalenga jamii nzima ya watanzania bila kujali vyeo na madaraja yao waliyonayo

Tafadhali sana, Huu wakati ambapo nchi ikiendelea kufuka moshi, wale wanaoukoleza kwa kutumia power waliyonayo, tunashauri pia kwa sasa waache

Kama kweli kipo kikundi maalumu kinachotambulika huko juu ambacho kazi yake ni kuteka na kupoteza watu, kwa kufanya hivi ni sawa na kuukoleza moto uwake

Cha kushauri, Ni viongozi wetu wakuu wa kiserikali, viongozi wa Dini, viongozi wa Kisiasa na watu mashuhuri, mkae meza moja ili kuleta suluhu ya jambo hili

Kuna msemo wa wahenga walisema, ni bora kuchelewa uendako ili ufike salama!

Endapo likatokea hili ambalo linafuka moshi likawaka moto, watu wakachinjana, wakuuwana n.k, historia itasema juu yenu viongozi mliopo na kwamba mliruhusu jambo hili la aibu na fedheha kutokea katika kipindi cha nyinyi mkiwa madarakani, majina yenu yoote yataingia kwenye kitabu hiki, Waziri mkuu, Makamu wa Rais, Rais, Katibu mkuu kiongozi, mawaziri, hata Wazanzibar mtaingia kwenye book hili la aibu

Je, kunafaida ipi iwapo maelfu na maelfu ya watu wakauwawa kisa tu walikuwa wakilalamikia sheria fulani fulani zinawakandamiza na ninyi hamkuchukua hatua?

Tutapata hasara gani kama nchi tukaamua kuwasikiliza hawa wanaolalamikia hayo kwa kusitisha baadhi ya mambo ili kukaa kitako kwa ajili ya kuwekana sawa?

Kwa mfano, Tukiahirisha uchaguzi kwa muda, na si kwamba tunaahirisha uchaguzi labda kwa faida ya watu wa nchi jirani, hapana, bado ni kwa faida yetu sisi wenyewe tukiwa na faida mikononi mwetu ya kuepusha moshi kuwa moto

Mungu, Bariki Tanzania, bariki viongozi wetu na uwape uvumilivu na hekima inayovuka viwango vya kibinadamu

Amina
Nimewaomba sana lakini hawataki kuskia mbeleni sio kuzuri watu wenye akili Tanzania wanazidi kuongezaka
 
Umesahau kama tuliahidi kama sii kuapa kutosikiliza?
 
Uchumi inaporomoka kwa kasi
downloadfile-39.png
 
Mkuu,

Nchi za waliowahi kuchinjana kwa wingi, hakujawahi kuwepo watakatifu wa kuombea?

Au watakatifu wapo Tanzania pekee,

Samahani, naomba tu kujifunza kwako
Miji ya Sodoma na Gomora iliangamizwa kwa kukosekana waombaji. Wangekuwepo wenye haki angalau wachache Mungu angeiponya. Kwa madhara tunayopitia kama nchi ni rahisi sana tukajisahahu tukajikuta wote tuna hasira na hasira ni chukizo mbele za Mungu na wote tutahesabika ni wenye dhambi. Hata tukiomba Mungu hawezi kusikia kwa kuwa Mungu hawezi kuwasikia wenye dhambi. Na uovu ukifika mbele za Mungu ulinzi wa Mungu unatoweka na tunaweza kuchinjana sisi kwa sisi au kuruhusu natural disasters ambazo zinaweza kuondoka na watu wengi sana kama ilivyotokea Sodoma na Gomora. Serikali itajitahidi sana kuweka ulinzi lakini Mungu akiondoa ulinzi wake mengineyo hayo ni kazi bure. Ndiyo maana hata viongozi mara kwa mara wanahimiza wenye dini kuomba kwa kuwa wanajua kabisa kama Mungu hayupo katikati hata wao wenyewe hawako salama. Sasa ili wawe salama mbele za Mungu ni kujifunza kutenda haki maana wakitenda maovu pia Mungu huwa anawaadhibu. Kuna Mfalme mmoja alikuwa na kiburi aliyeitwa Nebukadreza yaliomkuta ni kwamba aliondolewa kwenye ufalme na akenda kula majani kama ngombe kwa miaka saba mpaka akili zilipomrudia. . (Zaburi 127:1 - Mwenyezi-Mungu asipoijenga nyumba, waijengao wanajisumbua bure. Mwenyezi-Mungu asipoulinda mji, waulindao wanakesha bure.)
 
Mkuu, asante sana kwa majibu mazuri

Hata hivyoo, kuna mambo Mungu huyaacha yafanyike ili yawe somo kwa wengine na yeye Mungu kujitwalia utukufu wake

Katikati ya njaa kali ya uvamizi wa jeshi la washami na wayahudi kupata ahueni ya njaa kupitia unabii wa Elia, haikuwa sababu ya wayahudi kupona peke yao, bali pia wakoma waliokuwa wametengwa na kusahaulika
 
Ukweli usiopingika, Nchi hujengwa na umma wa wote

Linapotokea tishio lolote aidha la kijamii au tishio la nchi na serikali, kubwa kabisa la kutizama, Ni kupima athari za jambo hilo kwa haraka na kisha kuchukua hatua, sijawahi kukubaliana na yeyote, eti anishawishi kwamba, iko faida katika kuanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe,

Vita vya wenyewe kwa wenyewe, mara zote ukiziangalia kwa jicho la tatu, huwa zinatokea kwa sababu tu, mtu aliyetakiwa awe mtatuzi, hakufanya kazi yake ipasavyo

Nchi yangu sasa, inafuka moshi, kabla moshi haujawa moto, ni vyema sana na tunawaomba viongozi wetu, wachukue maamzi mazito ya kuepusha hili lisitokee, kwani hasara yake haimlengi mtu aliyeko Nanjilinji pekee, bali hasara yake inalenga jamii nzima ya watanzania bila kujali vyeo na madaraja yao waliyonayo

Tafadhali sana, Huu wakati ambapo nchi ikiendelea kufuka moshi, wale wanaoukoleza kwa kutumia power waliyonayo, tunashauri pia kwa sasa waache

Kama kweli kipo kikundi maalumu kinachotambulika huko juu ambacho kazi yake ni kuteka na kupoteza watu, kwa kufanya hivi ni sawa na kuukoleza moto uwake

Cha kushauri, Ni viongozi wetu wakuu wa kiserikali, viongozi wa Dini, viongozi wa Kisiasa na watu mashuhuri, mkae meza moja ili kuleta suluhu ya jambo hili

Kuna msemo wa wahenga walisema, ni bora kuchelewa uendako ili ufike salama!

Endapo likatokea hili ambalo linafuka moshi likawaka moto, watu wakachinjana, wakuuwana n.k, historia itasema juu yenu viongozi mliopo na kwamba mliruhusu jambo hili la aibu na fedheha kutokea katika kipindi cha nyinyi mkiwa madarakani, majina yenu yoote yataingia kwenye kitabu hiki, Waziri mkuu, Makamu wa Rais, Rais, Katibu mkuu kiongozi, mawaziri, hata Wazanzibar mtaingia kwenye book hili la aibu

Je, kunafaida ipi iwapo maelfu na maelfu ya watu wakauwawa kisa tu walikuwa wakilalamikia sheria fulani fulani zinawakandamiza na ninyi hamkuchukua hatua?

Tutapata hasara gani kama nchi tukaamua kuwasikiliza hawa wanaolalamikia hayo kwa kusitisha baadhi ya mambo ili kukaa kitako kwa ajili ya kuwekana sawa?

Kwa mfano, Tukiahirisha uchaguzi kwa muda, na si kwamba tunaahirisha uchaguzi labda kwa faida ya watu wa nchi jirani, hapana, bado ni kwa faida yetu sisi wenyewe tukiwa na faida mikononi mwetu ya kuepusha moshi kuwa moto

Mungu, Bariki Tanzania, bariki viongozi wetu na uwape uvumilivu na hekima inayovuka viwango vya kibinadamu

Amina
Waangalizi wa EAC wameshafika kubariki uchafuzi wa kihistoria wa 2025
 
..shida ni kwamba wamevimbirwa, hawawazi kingine zaidi ya kupora dola mali na utajiri wa nchi hii
 
Back
Top Bottom